Kwanini bei ya mafuta isiwe moja nchi nzima?

Kwanini bei ya mafuta isiwe moja nchi nzima?

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Zamani bei za bidhaa zote zilizopangwa na Serikali zilikuwa zinafanana nchi nzima. Mtu aliyepo Kilombero alinunua sukari kwa bei ile ile na mtu aliyepo Tandahimba, bei ya petroli Dar ilikuwa sawa na Kigoma.

Sasa wasomi wetu wamepatwa na nini kutofautisha bei ndani ya nchi moja? Kwamba sisi watu wa Rukwa tugharimie zaidi kununua dizeli kuliko watu wa Dar?

Kwanini kusiwe na standardization ya bei? Kwamba kuishi mbali na Dar ni dhambi?

EWURA embu fikirieni kwa makini jambo hili! Kumbukeni Tanzania ni nchi moja wananchi wote wanapaswa kufaidi au kuumia kwa usawa!
 
Zamani bei zilikuwa zinafanana nchi nzima, usafirishaji haukuwepo? Sasa hivi bei ya bia ni sawa nchi nzima hakuna usafirishaji?
Bia. Soda zinatengeneza kwa zones ili kuweza kukabiliana na hilo
 
Tatizo hiyo sekta imekamatwa na wafanya biashara wenye nguvu sana, na wasio na uzalendo wala huruma kwa mwananchi masikini kama mimi na wewe.
 
Kuna jamaa nilimuaona amejipenyeza kwenye ziara ya mama kule Qatar, pamoja na kwamba amekua akituhumiwa kwa mambo mbalimbali ya uhujumu na ufisadi mkubwa
 
Zamani bei zilikuwa zinafanana nchi nzima, usafirishaji haukuwepo? Sasa hivi bei ya bia ni sawa nchi nzima hakuna usafirishaji?
Zamani ni nn kilikuwa kinafanyika na saizi ni nini hakifanyiki mkuu
 
Tatizo la Nchi hii akili ndogo zipo madarakani, akili kubwa zipo mtaani.
 
Zamani ni nn kilikuwa kinafanyika na saizi ni nini hakifanyiki mkuu
Zamani kulikuwa na Tume ya bei ambayo ilikuwa ina - standardize bei ya bidhaa zote, kwa maana kuwa gharama za usafirishaji zilikuwa zinabebwa na wananchi wote. Biashara huria ilipoanza Tume ya bei ikavunjwa na ndipo maumivu kwa mikoa ya pembezoni ilipoanza!

EWURA wanapaswa kukokotoa bei ya usafirishaji wa mafuta nchi nzima na kuisambaza katika mafuta yote yanayonunuliwa mwezi huo!
 
Back
Top Bottom