Kwanini bei ya mafuta isiwe moja nchi nzima?

Je bei ya Bia si moja ya Dar na katavi,hizi bia hazisafirishwi?
NI HIVI JE ITAKUBALIKA MUUZAJI na msambazaji wa mafuta awe mmmoja tz nzima bei inaweza kupangwa moja kama ya bia..muuzaji anasafirisha mpaka kituoni kwako kwa bei kadhaa anakuachia faida bei kadhaa unauza bei aliyopanga inchi nzima..kama jambo azam na bia.. sasa mafuta yanauzwa dsm kila mfanyabiashara mwenye kibali anabeba na kwenda kuuza anapojua gharama za usafirishaji zimepangwa kwa kila lita kila eneo...muuzaji ana top up kwenye bei...na ikitokea yakauzwa bei moja inchi nzima kuna mahala watafidia bei ya usafiri ya kigoma na kwingineko...
 
Serikali inafahamu bei ya kusafirisha lita moja ya mafuta kila pembe ya nchi. Pia serikali inafahamu kiwango cha matumizi ya mafuta kwa kila eneo la nchi kwa mwezi. Kwa hiyo serikali inafahamu bei ya kusafirisha mafuta kwa kila eneo la nchi.

Kwa kuwa gharama za usafirishaji inafahamika kwa nchi nzima kwa mwezi kinachotakiwa kufanyika ni kuiweka katika gharama ya mafuta ya mwezi husika na kuigawa kwa lita zote za mafuta ya mwezi huo na ku-standardize bei kwa nchi nzima.

Jambo hili si geni na limefanyika katika utawala wa Nyerere na Mwinyi!
 
EWURA kuna kitu wanapata kutokana na hili kwani hakuna kisingizio cha kutokuwa na pan-territorial price!
 
Wanaita soko huria mkuu
Soko huria kwa bidhaa za viwandani sawa lakini si kwa mafuta ambayo yananunuliwa kutoka chanzo kimoja na kuuzwa nchi mzima kwa ajili ya matumizi yanayofanana!
 
Ewura hakuna wachumi makini.
Bei ya bia zote na soda Ni moja nchi nzima.
Bei ya chips mayai au kuku Ni moja nchi nzima. Bei ya sukari, sabuni etc Ni moja.
EWURA HAKUNA WATU MAKINI WA KUFANYA MAHESABU.
 
Haiwezekani, gharama za usafirishaji hazifanani...
 
Ukitaka ufanye bei iwe moja nchi nzima, itabidi bei ya Dar ipande, na itakuwa na faida kubwa, wafanyabiashara either watashusha kwa ajiili ya ushindani au watu hawatapeleka mafuta vijijin kwa sababu kutakuwa hakuna faida kama mjini hapa
 
Kigoma,bukoba mafuta bei inakwendaje huko???

Ova
 
Jinsi unavo zidi kuwa mbali na Dsm ndo jinsi utakavo ona moto
 
Zamani bei zilikuwa zinafanana nchi nzima, usafirishaji haukuwepo? Sasa hivi bei ya bia ni sawa nchi nzima hakuna usafirishaji?
Hii ina maana wananchi wa Dar walikuwa wanawafidia wananchi wa mbali, bei ya mafuta Dar ilikuwa kubwa kuliko ilivyotakiwa. Ukifanya hivyo zama hizi nafikiri mafuta yote yatabaki Dar , wauzaji watapata faida kubwa Dar kuliko kupeleka Kigoma au Tunduma. Nyakati zile za Ujamaa - hakuna hasara,ndio maana mashirika mengi yalishindwa kujiendesha.
 
Ukitaka ufanye bei iwe moja nchi nzima, itabidi bei ya Dar ipande, na itakuwa na faida kubwa, wafanyabiashara either watashusha kwa ajiili ya ushindani au watu hawatapeleka mafuta vijijin kwa sababu kutakuwa hakuna faida kama mjini hapa
Zamani bei ilikuwa moja na petro-stations zilikuwa zinajengwa! Kwa hoja yako una maana hakutakuwa na vituo vya mafuta mikoani kitu ambacho si kweli!
 
Hongera EWURA kwa kuanza kufikiria kuwa na bei moja ya mafuta nchi nzima. Ni vema mkajifunze kwa wenzetu kama Ghana na Ethiopia wamewezaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…