Kwanini biashara nyingi hazifikii malengo(hufa mapema)

Kwanini biashara nyingi hazifikii malengo(hufa mapema)

Rain brainy

Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
5
Reaction score
4
Watu wengi wanapo anzisha biashara huwa kuna baadhi ya mambo wanazingatia mfano;
-wateja
-Gharama za uendeshaji
-jinsi ya kukuza thamani ya bidhaa katika biashara n.k
# Lakini husahau kitu cha msingi Sana katika biashara ambacho ni namna ya kusimamia mzunguko au ktiririko wa fedha katika biashara.

USIMAMIZI WA MTIRIRIKO WA FEDHA KATIKA BIASHARA

Lazima uweze kufanya makadirio ya mzunguko wa fedha(cash flow forecast) kabla ya kuanza kufanya biashara.
-Hii inakuwezesha kuweza kujua kiwango cha fedha kinacho ingia na kinachotoka Kwa muda fulani
-Pia inasaidia kufahamu gharama za uendeshaji wa biashara yako.
-pia inasaidia kukupa taarifa za mapema kabisa kabla biashara haija anguka.
Vyanzo vya kukuwezesha uweze kufanya makadirio ya mtiririko WA fedha katika biashara.
Uzoefu wa mfanyabiashara.
Utafiti wa kimasoko.
Washauri mfano(wahasibu).
Vitu vya kuzingatia wakati wa kuaandaa makadirio ya mtiririko wa fedha.
Kuongezeka Kwa gharama za bidhaa.
Wacheleweshaji katika kufanya malipo.
Mabadiliko ya majira ya biashara.
Dharura.
Hatua kukuwezesha kufanya usimamizi mzuri wa fedha katika biashara.
1. Tambua mzunguko wa mauzo.
2.Rekebisha sela ya ukusanyaji fedha kutokana na mauzo.
3.Simamia vizuri Mali ulizonazo.
4.Tumia hela yako Kwa kiwango kikubwa.
5.Panga Kodi.
Vitu vingine vya kuzingatia ni.
-Angalia kiwango cha pesa kilasiku.
-Angalia mapato kila baada ya siku Saba.
-Angalia bidhaa zako na kuzihesabu mwisho WA mwezi.
-jaribu kukutana na washauri mbalimbali kila robo mwaka.
Naaam, natumaini watu wakisoma hiyo makala apo juu wanaweza wakatatua tatizo la kufeli Kwa biashara.
 
Janga la watu wengi ni kutunza kumbukumbu na matumiz kupitiliza
 
Kweli hasa kwenye matumizi kupitiliza
Wakati Wana fanya uandaaji wa biashara wanashindwa kupiga majumuisho /mahesabu ya gharama za ziada katika uendeshaji wa biashara
 
Back
Top Bottom