Kwanini biashara nyingi za Wasafi/Diamond hazidumu sokoni?

Kwanini biashara nyingi za Wasafi/Diamond hazidumu sokoni?

Last Seen

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
229
Reaction score
566
Mambo vipi wanajamvi?

Nimewaza Mara kadhaa kuhusu bidhaa zinazoletwa sokoni na Bwana Chibu Dangote kwa nini hazidumu katika soko?

Chibu ni kijana mpambanaji mwenye uchu wa mafanikio makubwa na amethubutu kuwekeza ndani na nje ya Muziki wake, ametoa ajira kwa vijana kadhaa. Lakini swali moja ninalijiuliza ni kwa nini bidhaa zake zinakufa na kupotea katika soko baada ya muda mfupi?

Tumeshuhudia akizindua Diamond Karanga, wasafi.com, Chibu perfume na zote hizi hazipo sokoni au hazalishi tena bidhaa hizo (biashara imebuma).

Na miaka kadhaa nyuma amefungua Kituo cha Runinga na Redio ambavyo vilipokelewa kwa hamasa kubwa na wafuasi wake, lakini kwa upande mwingine wamekuwa wakilalamikiwa kurusha maudhui yasiofaa na mara kadhaa wamekutana na rungu la TCRA. Je, Wasafi Media itapotea kama biashara zake zilizopita?

Wasafi bet ni biashara ingine aliyoitambulisha hivi karibuni je, itahimili ushindani dhidi ya kampuni zingine za kubashiri?

Mwisho, Mimi sio mtalamu wa biashara na nngependa kujua nini inachangia kufeli kwa bidhaa zake nyingi, nini ushauri wako kwa Baba

Tiffah.
 
Wasanii wengi tu biashara zinakwama wanakua na OVEREXPECTATION yani anahisi kupitia umaarufu wake akifungua biashara wateja watafurika ambapo baada ya kufungua inakua kinyume na matarajio wasanii wengi tu ata Alikiba kinywaji cha mofaya alikipiga chini.

Konde nae na mgahawa wake chali. Vanessa Mdee alikuja na viatu vyake nae chalii. Whozu anaduka lake la nguo ila linataka kumshinda nafkr wengi wanakua hawana akili/plan za biashara ukiona biashara ya msanii imesimama mheshimu aswaa maana sio kazi ndogo S/O to nengatronix & Shishifood wanajitadi sanasana
 
Kwa hiyo we ukiona tu jina la Wasafi au picha ya Diamond unajua biashara ni yake?
 
Mimi naona mwisho wa siku, mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe. Au nasema uongo ndugu mtoa mada?
 
Back
Top Bottom