Kwanini biashara ya madawa ya kulevya inafanyika sana kwenye nchi za Kiislamu na Kikristo?

Kwanini biashara ya madawa ya kulevya inafanyika sana kwenye nchi za Kiislamu na Kikristo?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
Hakuna data zinazokubarika kimataifa za kiwango cha uzalishaji wa madawa ya kulevya siyo kwa Tanzania tu bali duniani kote. Kitu kinachojulikana ni mtikisiko na madhara yake yanayoonekana na huku wengine wakihuswa moja kwa moja kwa njia moja au njingine.

Katika pekua pekua yangu kwenye makabrasha na majarida mbali mbali nimepatwa na butwaa baada ya kugundua kuwa uzalishaji na usambazaji wa haya madawa unafanyika sana kwenye nchi ambazo wananchi wake na serikali zao zinajinasibisha kama ni wacha Mungu katika imani ya kikristo na kiislamu, kwa lugha nyingine, wanamwogopa sana Mungu katika maisha yao (conservative).

Katika pekua pekua hiyo, nikagundua kuwa watumiaji wengi wa madawa haya ya kulevya ni jamii ambayo iko kwenye nchi ambazo zinajinasibisha sana kama siyo wacha Mungu au kwa jina jingine ni dormant believer (liberal).

Kama tunavyofahamu mazao ya poppy, coca na cannabis ndiyo huzalisha opium, heroin, cocaine na hashish ambapo mashamba makubwa ya mazao hayo yanapatikana katika nchi Afghanistan, Colombia, Peru, Burma, Mexico, Bolivia, Pakistan, Iran na Morocco na usagirishaji wake ukipitia kwenye nchi za West Africa ambazo ni Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Nigeria, Ghana na Senegal huku watumiaji wakubwa wakiwa ni kwenye nchi za ulaya na Marekani.

Ukiangalia katika majarida na makabrasha utaona kuwa hizi nchi zinazojihusisha sana na biashara hii asilimia kubwa ya wananchi wake ni wa dini za kikristo na Kiislamu. Kama jedwari linavyoonyesha hapa chini,

Afghanistan===> Islam (Sunni 80%, Shiite 19%), other 1%

Colombia====> Roman Catholic 90%

Bolivia======> Roman Catholic 95%, Protestant (Evangelical Methodist) 5%

Peru=======> Roman Catholic 81%, Seventh-Day Adventist 1%, other Christian 1%, unspecified or none 16%.

Mexico=====> nominally Roman Catholic 89%, Protestant 6%, other 5%

Pakistan====> Islam 97% (Sunni 77%, Shiite 20%); Christian, Hindu, and other 3%

Iran=======> Islam 98% (Shi'a 89%, Sunni 9%); Zoroastrian, Jewish, Christian, and Baha'i 2%

Morocco=====> Islam 99%, Christian 1%

Argentina====> Roman Catholic 92%, Protestant 2%, Jewish 2%, other 4%

Hata ukiangalia nchi ambazo biashara hii chafu hupitia nazo zinaangukia kwenye kundi lile lile la nchi ambazo zina wakristo wengi wa madhehebu ya Roman Catholic au Waislam na hasa Sunni.
Guinea=====> Islam 85%, Christian 8%, indigenous 7%

Liberia=====> traditional 40%, Christian 40%, Islam 20%

Nigeria=====> Islam 50%, Christian 40%, indigenous beliefs 10%

Ghana=====> Christian 63%, indigenous beliefs 21%, Islam 16%

Senegal====> Islam 94%, Christian 5% (mostly Roman Catholic), indigenous 1%

Ukiangalia kwenye trends ya Tanzania kwa sasa, kadri makanisa na misikiti inavyoongeza kila siku kwa sasa na pia biashara hii chafu nayo inaongezeka kwa kasi nchini.

Tanzania====> mainland: Christian 30%, Islam 35%, indigenous 35%; Zanzibar: more than 99% Islam

Ninashindwa kuelewa kama hii biashara inahusisha imani ya dini au chanzo chake kiko ndani ya religious value kwa sababu haiwezekani kukawa ni coincedence kuwa na nchi ambazo wananchi wake wengi ni "wacha Mungu" wa dini za kikristo au kiislamu wakati huo wakati ni vinara wa biashara hii ambayo katika macho ya mafundisho ya dini zao ni dhambi.

Kwa nini dhambi hii ya kuzalisha madawa inawapenda sana Wakiristo na Waislamu na huku utumiaji mkubwa unakuwa kwa jamii ambayo inalijua tu jina la Mungu lakini haifuati mafundisho yake.

Kama tatizo ni ukosefu wa serikali madhubuti, kwa nini kwenye jamii yenye kumuogopa Mungu ambayo imeambiwa katika vitabu na misahafu kuzitii mamlaka duniani zinashindwa kuwa na mamlaka ya kiserikali imara!.

Why only in active Christian and active Islam countries?. Kuna kitu gani hapa!!!!!

Hizi data zinapatikana hapa, World Religions | Infoplease.com

Ramani kuonyesha trends and route za biashara hii chafu ambayo ni "Immoral" kwenye macho ya Mungu wao wa kila siku.
attachment.php

attachment.php



NB:
Hili ni jukwaa la kuelimishana na kupashana habari na siyo jukwaa la kurumbana kuhusu dini.

Ningependa wana JF wenye michango inayojenga badala ya kubomoa na wale wasio na mlengo wa kidini dini ndiyo wakijike kwenye kuboresha akili yangu naya member wengine wanaopenda kufahamu kilichoko nyuma ya pazia hili.

Hii ni topic inayojikita kwenye maisha ya kijamii. Thanks
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    17.7 KB · Views: 824
  • image.jpg
    image.jpg
    21.3 KB · Views: 816
Kwel inashangaza, ila tujiulize kitu, soko si linafuata population? Na population kubwa hapa dunian ndo hyo ya christian and muslim!

pia nature inachangia, mf. Nchi kama pakistan, iran, bolivia ni kwamba ziko favourable kwa ustawi wa hayo madawa.
 
Hebu mkuu tuwekee na data ya huko yanapotumika ili tujue picha halisi!!!!
 
Kwel inashangaza, ila tujiulize kitu, soko si linafuata population? Na population kubwa hapa dunian ndo hyo ya christian and muslim!

pia nature inachangia, mf. Nchi kama pakistan, iran, bolivia ni kwamba ziko favourable kwa ustawi wa hayo madawa.
Mkuu una maana gani unasema population wakati nchi kama China na India population yao jumla ni 2.6 billion wakati dunia nzima ina kadiriwa kuwa na watu 7.1 billion.

Una maana gani unaposema hizo nchi ziko kwenye hali inayoruhusu uzalishaji wa madawa ya kulevya.

Vipi na nchi ambazo madawa huwa yanapita kwa wingi ikiwemo Tanzania?
 
Hebu mkuu tuwekee na data ya huko yanapotumika ili tujue picha halisi!!!!
Mkuu sijakuelewa vizuri. Data gani unahitaji kwa sababu kuna uzalishaji na matumizi zikichagizwa na imani za dini kwa watu wa eneo hilo.
 
ni ngumu kujua takwmu za uzalishaji kwa kuwa ni biashara ya siri sana mkuu capturing ya data inakuwa ngumu sana!ila wanaokamatwa ni wachache kuliko wanaofanikiwa mkuu.
 
Unganisha dots kati ya vatican na mafia na taliban na wazalishaji wa hizo dawa.tatizo letu hizi dini mbili zimetublind kabisaa hatutak kuona wala kusikia ila ukweli kulikoshamiri ukatoliki na uislam wenye msimamo mkali ndio haswa sehemu kuu za uzalishaji na usafirishwaji.unadhan taliban wanapata wapi pesa za kununulia silaha na latin america boom ni oil peke yake?ushawah jiuliza wale drug traffickers wa brazil,colombia na mexico where do they launder their money??ndicho kinachopush economic boom ya nchi hizo that's why wanawafurahisha tu USA mdomoni ila moyon wanajua drugs ni sehemu ya export yao to USA
 
Mkuu una maana gani unasema population wakati nchi kama China na India population yao jumla ni 2.6 billion wakati dunia nzima ina kadirwa kuwa na watu 7.1 billion.

kwa takwim za kidin ni kwamba wakristo na waislam ndo dini zenye watu wengi duniani. Na pia china na india pia kuna watumiaji watumiaji wa hayo madawa so soko lipo pia..hao wanaokamatwa ni wachache kuliko wanaofanikisha biashara hizo.

Una maana gani unaposema hizo nchi ziko kwenye hali inayoruhusu uzalishaji wa madawa ya kulevya.

hilo la uzalishaji liko wazi mkuu, manake kila zao linahitaji hali ya hewa na attitude tofauti ili lipate kustawi na kutoa mazao mengi. So hizo nchi hata wangekaa wapagani wangezalisha tu as long ni mazao yanayowaingizia kipato. Ndo mana kuna nchi huko latin amerika wameruhusu bangi kabisa manake iko nyingi hadi kuzuia ni ngumu.

Vipi na nchi ambazo madawa huwa yanapita kwa wingi ikiwemo Tanzania?

kwa madawa kupatikana kwa wingi kama apa kwetu ni ulegevu wa system na sera mbovu tu za kuyadhibiti. Na pia hapa bongo ni dnjia tu ya kusafirisha kwenda nchi nyingne kutokana na huo ulegevu wa udhibiti. Kikubwa ni ufatiliaji tu mkuu..hata nchi ya wapagani wakiwa lege lege kwenye udhibit madawa yatapita tu kawaida.

kwa kuhusu nchi kuwa favourable kwa uzalishaji mbona hilo liko wazi kabisa mkuu, kila zao linahitaji hali ya hewa na attitude ambayo iko favourable ili kuweza kustawi. Kwahiyo kwakuwa ni mazao yenye pesa nyingi ni kuwa pale bolivia hata wangekaa wapagani wangezalisha cola tu kawaida kupata fedha!

Kwa population ni kwamba uislam na ukristo ndo dini zenye watu wengi zaid dunian so ukiweka refference lazma utawapata wengi.

inshort any crime or illegal business haichagui dini ya mahali au mtu. Ni udhaifu tu na sera mbovu zinazosababisha hayo kutokea.
 
Ng'wamapalala, mbona dunia karibia yote waumini hao wote wamo nchi nyingi wanazidiana tu idadi unaweza kuta nchi hii waislamu ni wengi nyingine wakristo ni wengi

sasa huwezi kutoa takwimu za namna hiyo wakati dunia nzima ipo hivyo au umefanya hivyo ili ku balance?

Labda useme nchi zenye wakristo wengi kama hizo za America ya kusini na baadhi ya nchi zenye waislamu wengi...
 
Last edited by a moderator:
ng'wamapalala upo sahii, na ulinganisho wa dini na madawa ya kulevya. ninachoona hapa ni kuwa.,kimsingi kwenye nchi za afghanistani wanayatumia kuendesha mikakati yao ya uenezi wa dini na vita vya kuuana ili wapate madaraka na utajiri. lakini kwenye nchi za kolombia ni uraibu tu., wanayatumia kutengeneza pesa(utajiri) na kupata ridhimu(starehe),na ni kwakuwa wao ni drug addicts hivyo hawawezi kuishi bila madawa.ila hayana uhusiano na imani ya ukristo kwa namna yoyote. pengine sio wakristo wa dini zaidi ya kuishi kiutamaduni wa ukristo tu wa juu juu. pia inawezekana katika nchi hizi za colombia, kilimo hichi cha madawa haya yanamanufaa kitabibu, na pengine ndipo walianza kuzalisha kwa manufaa ya soko la ki-utabibu,na hivyo hatimaye wakaishia kutumia kama ulevi wa kupata ridhimu kichwani(drug abuse).
japo nchi za jamaica inasemekana rastafari wanatumia marijuana kama sehemu ya dini yao ya kirastafari, sina uhakika kwa hili japo nafahamu bob marley aliwahi kuutetea mmea huu.one:drum::majani7::drum: love
 
suala la madawa ni la kibinadamu zaidi na halihusiani na dini fulani. Ktk research yako kuna taasisi yoyote ya kidini yenye kumiliki mashamba ya mimea hiyo?
 
ng'wamapalala upo sahii, na ulinganisho wa dini na madawa ya kulevya. ninachoona hapa ni kuwa.,kimsingi kwenye nchi za afghanistani wanayatumia kuendesha mikakati yao ya uenezi wa dini na vita vya kuuana ili wapate madaraka na utajiri. lakini kwenye nchi za kolombia ni uraibu tu., wanayatumia kutengeneza pesa(utajiri) na kupata ridhimu(starehe),na ni kwakuwa wao ni drug addicts hivyo hawawezi kuishi bila madawa.ila hayana uhusiano na imani ya ukristo kwa namna yoyote. pengine sio wakristo wa dini zaidi ya kuishi kiutamaduni wa ukristo tu wa juu juu. pia inawezekana katika nchi hizi za colombia, kilimo hichi cha madawa haya yanamanufaa kitabibu, na pengine ndipo walianza kuzalisha kwa manufaa ya soko la ki-utabibu,na hivyo hatimaye wakaishia kutumia kama ulevi wa kupata ridhimu kichwani(drug abuse).
japo nchi za jamaica inasemekana rastafari wanatumia marijuana kama sehemu ya dini yao ya kirastafari, sina uhakika kwa hili japo nafahamu bob marley aliwahi kuutetea mmea huu.one:drum::majani7::drum: love
Mkuu wangu, ninashukuru sana kwa mchango wako.

Umenigusa kwa maneno yako kuwa hawa watu tunaowaona wacha Mungu ni kwa nje tu lakini kwa ndani ni mashetani kulingana na maandiko kwenye misahafu ya dini.

Kwa ini isiwe China, Japan au India ambako population ni kubwa harafu wana imani ya dini tofauti na Ukiristo na Uislamu au Russia.
 
Back
Top Bottom