Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ni nadra sana kusikia mwaka umeisha bila kelele, vurumai na sarakasi za kila aina kwenye biashara ya hizi bidhaa mbili za sukari na mafuta ya kula. Nini hasa kinasababisha haya yote ukizingatia ni bidhaa rahisi sana kuzalishwa, nchi nyingi tu wanazalisha na hata sisi wenyewe tukiamua na kuweka nia tunaweza kuzalisha hadi na ziada ya kuuza kwa majirani?
Nini hasa kinazifanya bidhaa hizi mbili kuwa keki au special hivyo kiasi kwamba lazima zilete zogo kila wakati?
Nini kinazifanya lazima zipande bei kila mwaka kwa kiasi kikubwa?
Nini kinapelekea wafanyabiashara kudaiwa kuzificha wakati mwingine hadi kupelekea wakuu wa wilaya na TRA wakisaidiwa na polisi kuzisaka kwa bunduki na watu kuwekwa ndani kwa sababu yake?