Kwanini biashara za mastaa wa bongo hazidumu?

Namba 3 siyo vyake yeye ni balozi tu.
Anaye kula hasara mwenye product siyo balozi.
 
Tatizo hawapendi partnership.. Kiba na Mondi wakitoa bidhaa pamoja unafikiria itafail?
 
Sabuni za nandy niliwahi ona tangazo!

Sema tatizo wabongo hawana ushabiki ule wa kununua bidhaa za msanii wao!
Sapoti kubwa ni kucomment tu kwenye page yako ya Instagram na kuangalia video YouTube!
 
Biashara inahitaji umakini mwingi,ujuzi mwingi mdogodogo na mchanganyiko.Si kama ilivyo kipaji cha uigizaji tu n.k.,japo hata hivi navyo pia,vyahitaji nidhamu ya kuvikuza na kuvilea n.k..

Jina la mtu maarufu peke yake haliwezi kuuza au kusukuma mauzo (hasa kwa mda mrefu) kama huna ufuatiliaji makini,kulijua soko lako,wateja wako na vionjo vyao (vinavyobadilika badilika sometimes ili uendane nao),washindani wako (wana nini kinachowavuta wateja kwa washindani wako zaidi na si kwako.Na hata wanaokuja kwako,nini kinawavuta),uweke wasimamizi wa namna gani/kiwango gani na kwa mfumo upi ili biashara isiumizwe,wateja wasikwazike au kuchoka 'bidhaa' yako au huduma yako na ikue n.k.

Nadhani,umaarufu unadanganya baadhi yao kuwa atauza tu kwa jina lake n.k.,japo pia yawezekana wana sababu zingine za maana zaidi.Kuwa mwanamziki mzuri haikupi uhakika wa kuja kuwa, (mfano) injinia au tabibu (bila kujsomea au kujifunza kwanza).Biashara yahitaji kupeleleza kabla ya kuivamia.Na ikibidi,kuwa karibu sana na walioiweza na kufanikiwa-Hao wanajua mapito ya biashara husika,ugumu wake na changamoto zake,na hatimae namna ya kuifanikisha.Yataka unyenyekevu na usikivu.Sina hakika haya wanayo.

Kingine,ni labda hatimae kuja kutingwa na yaliyowapa umaarufu na kuona afadhali wapunguze majukumu ya biashara zingine na kukomalia walichopata mafanikio nayo.
 
Sabuni za nandy niliwahi ona tangazo!

Sema tatizo wabongo hawana ushabiki ule wa kununua bidhaa za msanii wao!
Sapoti kubwa ni kucomment tu kwenye page yako ya Instagram na kuangalia video YouTube!
Wanao comment wenyewe maisha ya mlala hoi Hawana shughuli yoyote tu maisha yetu hayo
Unaleta sabuni kipande 3000 Wakati huo huo sabuni ya Jamaa kipande 500 tunatumia familia nzima
 
ukiwa star haimaanishi kuwa...ndio unayo maarifa...mastar wengi wamekosa maarifa ndio maana unaona biashara zao zina buma
 
Wanao comment wenyewe maisha ya mlala hoi Hawana shughuli yoyote tu maisha yetu hayo
Unaleta sabuni kipande 3000 Wakati huo huo sabuni ya Jamaa kipande 500 tunatumia familia nzima
Ni kweli! Ila angalia Wasafi.com ilivyoanza kwa mbwembwe leo iko wapi? Na wimbo mmoja ilikua 200 tu ila ilishindikana!
 
Ni kweli! Ila angalia Wasafi.com ilivyoanza kwa mbwembwe leo iko wapi? Na wimbo mmoja ilikua 200 tu ila ilishindikana!
Ana download mmoja tunatumiana whatsapp
Waangalie namna ya kutukamata walala hoi
Haji manara anakuja perfume Bei ya mwisho 25000 Kisa ana followers 1M
Wakati hao Watu wanam follow 500k hata mafuta ya kupaka Hana mwingine anafuata tu kuona mizaha yake dhidi ya yanga
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Wana amini wakisha tumia instagram na media ndio biashara inatembea na unaaanza kula faida..watembee field kujionea , sa unakuta msanii yeye huyo huyo anataka awe director ,market man anger,mtu wa finance
ni ngumu sana,atleast diamond kwa upande flan ana win sababu ya kutochanganya usanii wake na biashara,ila kwingine km pafyum amefeli sana
 
Ebana eeeh πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Sawa tumewasikia wana Jf huu ushauri wenu nitaufikisha kwa wenzangu tuufanyie kazi
 
Zile ndala za kidoti zilikimbiza sana but nyumbani lounge jaydee kaiua kusudi kumkomoa gadna
 
ni ngumu sana,atleast diamond kwa upande flan ana win sababu ya kutochanganya usanii wake na biashara,ila kwingine km pafyum amefeli sana

Perfume kafeli maana ndio product yake kwa percent zote ,ila izo karanga ziko under smart industry ..so yeye ni kama anatumia jina lake kufikisha bidhaaa
 
Shishi food is doing fine
 
Lack of middle class inafanya biashara nyingi bongo zistruggle sio wasanii pekee yao
 
poor business management..we mtu hujawahi kuuza hata pipi,leo from no where unakuja na ideas za biashara za mamilion,utawezea wapi?
Biashara unaanza kidogo kidogo kwanza ili kulisoma soko na kuwajua washindani wako..
 
Naomba muelewe kuwa bidhaa nyingi sio za kwao ila wao ni mabalozi tu wakuzitangaza na wanalipwa chao. Management zinakuwa chini ya watu wengine wenye makampuni yao mfano Diamond Karanga, mofaya, pepsi kubwa, wasafi radio, chibu perfume, maji ya lady jaydee n.k. Biashara zao moja kwa moja ni kama shishi food, nyumbani lounge, wasafi records, kings records na zingine zingine

Kufa kwa biashara ni jambo la kawaida sana na sio la kumbeza mtu. Kila biashara ina changamoto zake na inabidi kukabiliana nazo. Hakuna biashara inayoenda moja kwa moja bila changamoto. Muhimu ni kuinuka baada ya kuanguka na kujaribu ni funzo kubwa sana katika biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…