Kwanini bidhaa nyingi zinaandikwa neno halal kwa lugha ya kiarabu na imechorwa msikitini kwani nchi yetu ni ya kiarabu? Au nchi yetu ni ya kidini?

Kwanini bidhaa nyingi zinaandikwa neno halal kwa lugha ya kiarabu na imechorwa msikitini kwani nchi yetu ni ya kiarabu? Au nchi yetu ni ya kidini?

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
Yaani kwa bidhaa nyingi sana naziona zimeandikwa halal kwa lugha ya kiarabu na huku umechorwa msikiti kwa maana kwamba nchi hii ni ya kidini na ya kiarabu au nchi hii imeuzwa kwa waarabu mbona hata sielewi au nyingi wenzangu hamjawahi kukutana nazo?

Ila bidhaa za nguruwe sijawahi kuona kabisa naona nyama yao zile za viwandani hazijaandika kwamba sio halali na sijui kwanini tutaendelea kula kitu ambacho hata nchi haijadhibitisha kwamba sio halali na ni kweli nguruwe sio halali we endelea kula upate minyoo aina ya Ascaris lumbicodiea alisikika mlevi fulani
 
Halal maana yake nikuwa hiyo bidhaa imefata kanuni zote za kiislam, yaan kama ni nyama ya pakti basi huyo mnyama amechinjwa na sio mzoga , na hiyo bidhaa au nyama ni za aina ya wanyama ambao wameruhusiwa na sheria ya uislamu kuliwa, sio kama nguruwe nk.

Sio mbaya ni kwa usalama wa watumiaji,,
 
Usile usipate tabu watakulisha majini. Kula ambazo hazijandikwa hivyo.
 
Mnatawaliwa na juha unategemea nini?
Taratibu Mzee, tukikaa na simu au computer zetu vyumbani mwetu tunahisi kama tumejificha tunaweza kutukana tu vyovyote. Usijisahau sana haina haja kutumia lugha ya aina hiyo, sijawahi hata kusikia Mbowe, Lissu hat Lema wakitamka hayo.
 
Complain zingine!hata america zipo bidhaa za halai,tena hadi kuna migahawa inaandikwa halal na kawaida tu!
 
Bidhaa za halal au zilizoandikwa Halal kwa kiarabu zipo sehemu nyingi duniani na hakuna anaelalamika bali ni biashara zaidi

Hata Supermarkets za Ulaya zipo bidhaa hizo za Halal ili kuvutia wateja wa kiislam
Ni kawaida sana boss wala haina shida kabisa
Kwanza nikiona hiyo alama ninakuwa na amani
Kuhusu Kuku hapa UK wengi sana ni Halal mpaka mzungu anakuambia this is Halal 😄 🤣
 
Wewe kanunue zilizopigwa chapa ya kafir utuachie bidhaa zetu halal🐼
 
Yaani kwa bidhaa nyingi sana naziona zimeandikwa halal kwa lugha ya kiarabu na huku umechorwa msikiti kwa maana kwamba nchi hii ni ya kidini na ya kiarabu au nchi hii imeuzwa kwa waarabu mbona hata sielewi au nyingi wenzangu hamjawahi kukutana nazo?

Ila bidhaa za nguruwe sijawahi kuona kabisa naona nyama yao zile za viwandani hazijaandika kwamba sio halali na sijui kwanini tutaendelea kula kitu ambacho hata nchi haijadhibitisha kwamba sio halali na ni kweli nguruwe sio halali we endelea kula upate minyoo aina ya Ascaris lumbicodiea alisikika mlevi fulani
Serikali wanapenda kuchukulia poa mambo madogo madogo kama haya, wenzao wana maana yao kupenyeza upuuzi wao ndani ya nchi yetu isiyofungamana na dini yoyote ya kuletewa.
 
Back
Top Bottom