Kwanini binaadamu akifa hubebewa cloves?

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,646
Jana wakati nasafiri kuelekea mwanza tulifika maeneo ya usagala tukakuta kuna kundi kubwa la watu,watu hao walikuwa wanashangaa tukio la wafungwa walio ruka kutoka katika gari la polisi mmoja aalikufa hapo hapo wengine wawili waliumia vibaya sana,wale walio umia walibebwa kawaida tu ila yule aliye kufa walisubiri cloves ndio wakambeba. Sasa kwanini inakuwa hivyo,maana nilitegemea mzima ndio abebewe glove kwakuwa kama ni vidudu vinakuwa bado vina uhai ila alie kufa abebwe bila glove kwakuwa vidudu havina uhai kwani damu ya maiti imeacha kutembea
 
ngoja wataalamu waje! ntajifunza kitu hapa!
 
Sio waliokufa tu bali hata majeruhi wanatakiwa wabebwe ukiwa umevaa groves mikononi...kwa ajili ya kuepuka infection kwa magonjwa yanayoambukiza............
 
sio waliokufa tu bali hata majeruhi wanatakiwa wabebwe ukiwa umevaa groves mikononi...kwa ajili ya kuepuka infection kwa magonjwa yanayoambukiza............

ila mkuu imekuwa ni rahisi sana kwa majeruhi kubebwa kawaida asante nimepata mwanga hapo
 

Watu wote(hai/wafu wanatakiwa kushikwa si kubebwa tu na mipira ya mikono(Gloves).
Tofauti na wengi wanavyoamini/dhani kufa si tukio ni mchakato(haimaanishi mtu anapokufa vijidudu mwilini kama anavyo basi ndipo vinakufa).

Hata hivyo wengi wanaoshika maiti/wafu kwa mipira ya mikono(Gloves) hushika kwa sababu ya imani/saikolojia(myth) kwamba kuna vitu vibaya vinavyohusianishwa na mtu anapokufa!
 

Hapo kwenye nyekundu nadhani siyo sahihi japo si mtaalamu wa afya.
 
Labda waliigopa fingerprints kubaki kwenye mwili wa marehemu asijekufanyiwa uchunguzi ikaonekana labda alipigwa na watu ndio ikawa hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…