Alichowaza mleta mada sicho alichoandika maana hakuna mahusiano yoyote ya mada na mfano wa kumuwazia mtu kifo. Ila tusimlaumu sana mleta mada. Huenda tatizo ni background ya alikofundishwa kuandika insha!
Haya, nitakupa mfano mdogo uelewe.
Tuseme ulikuwa na kazi nzuri. Mshahara mnono.
Kwenu unaonewa wivu sana.
Ghafla unapoteza kazi. Unarudi kwenu. Mawazo mengi, msongo wa mawazo mkali sana.
Ni wazi majirani wamefurahi, lakini wanajifanya kukupa pole ya kinafiki.
Pembeni wananong'ona: "Aaa huyu hana mwaka mmoja tutakuwa tumempoteza. Si mnaona alivyokonda?"Jambo hilo unalitambua, unavumilia. Na ulikuwa unawafadhili sana! Hawakumbuki fadhila.
Kumbe unahangaikia sehemu nyingine nzuri zaidi. Baada ya miezi nane hivi, unafanikiwa, unaondoka pale kwenu kimyakimya.
Unarudi baada ya mwaka hivi, uko vizuri zaidi ya pale mwanzoni.
Ukiulizia walipo wabaya wako waliokuwa wanasubiri " hatma yako" wengi wameondoka(wamekufa) au hali zao sio nzuri.
Waliobaki wanakuonea aibu saaana hadi huruma.(True story)