Kwanini Black people wanapenda sana Socialism/Communism?

Kwanini Black people wanapenda sana Socialism/Communism?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Hili jambo linanishangaza sana, Black people karibia Dunia nzima wanapenda sana Communism badala Capitalism, kuanzia black Amerika, latin black amerika, Caribbean mpaka kwetu Afrika communism /socialism ndo inavutia wengi klk capitalism.

Ukiangalia watu kama akina Martin Luther King USA ni communist/socialist, Mandela socialist/communist hata Chama cha ANC ni Communist hapa kwetu Tanzania hivyo hivyo Socialism/Communism.

Sasa ni kwanini? Wakati Capitalism ndiyo ina-create wealth? Nchi zote zilizoendelea Duniani ni Capitalist, Capitalism ndiyo inayoweza kupunguza na kuondoa umaskini, lakini kwa nini tunavutiwa na Communism?
 
Ni kwa kuwa watawala au wakoloni wao walikuwa mabepari.kwa hiyo baada ya kupata uhuru wakaona wafuate socialism ili kuwakwepa watesi wao kumbe wanaingia shimoni.
 
Hamna watu wavivu kama watu wanaopenda socialism, wavivu wa kufikiri na kutenda.

Anajua hata asipofanya kazi atakula, asipofikiri kuna mtu anamsaidia kufikiri.

Ujamaa ni janga linalorudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na nchi kwa ujumla.
 
simple, capitalism ni ya kinyonyaji!..na hakuna true capitalism in this world!
 
Ujamaa ni mfumo wa kipumbavu ambao huathiri nia binadamu kufikiri akidhani kuwa wanaomzunguka wanafikiri kwa niaba yake kumbe wote wameingia katika mkumbo huo.
Watu weusi wameathirika kwasababu ya mapokeo ya hovyo na kuamua kuishi katika njia yenye mfumo rahisi ili kukwepa kuwajibika kufikiri katika chanya.
 
asili yetu ni ya hovyo Sana unakuta juma akimaliza la saba ataenda kwa mjomba yake kumsalimia then mjomba ataanza kumsomesha juma kama mjomba wake.mjomba akimkatalia juma Dada atamuona anaroho mbaya. mifumo yetu ya maisha imetuandaa kuwa tegemezi kufanyiwa mambo na wengine. #MF

kuomba kwa ajili ya roho na nafsi zetu tunaamini ni jukumu la wachungaji

Tunazaa watoto wengi tukiamini ndugu zetu watatusaidia kusomesha

hatujitumi kwa bidii kwa sababu mbele yetu tunaona kuna mtu atatupush somewhere.

hakika ukitaka kuchukiwa na ndugu na marafiki ishi hiyo capitalism system
 
Back
Top Bottom