Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Unajua mkuu umekerekwa na kitu ndio Maana umeziona Habari za Mungu hazikufurahishi.Japo kwa kuwa ulipata bahati ya kuhudhuria hata sunday school nawaomba wakristo wakukumbuke kwenye sala utaiona tena nuru.
Nikirudi kwenye maada hivi mtu akimuua mwanao hajakuadhibu,,hajakuumiza moyo,,Mbona ukiwa una bifu na mtu utawaambia wanao wasicheze hata kula kwake...Mungu kumuua mwanawe David ni adhabu tosha kwa David au ulitaka amuue David??
Labda naweza sema Umeamua tu kukosoa hio adhabu pasipo na kujua ilitolewa kwa haki na kuzingatia Mambo mengi tusioyajua.
Alipompeleka mstari wa mbele askari wake ili auliwe halafu amle mke wa huyo askari,adhabu ilitolewa kwa mtoto aliyezaliwa(at least ni hekaya tu hakijawahi kutokea kitu kama hicho)
Characters zote za kwenye yale maandishi ni za kufikirika tu..
 
Once again umenikosha sana kwa uchambuzi wako murua kabisa..... Ila mkuu ungetusaidia pia kwanini dhambi afanye mwingine alafu alaaniwe mwingine utakuwa umetusaidia kumaliza sintofahamu yetu humu
Nimemsikia muhibiri mmoja akisema kuwa huenda Caanan ndio alikuwa kipenzi cha baba yake, hivyo itamuuma zaidi kuliko angemlaani yeye, yaani ndio alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Ham na Nuhu alilijua hili.
 
Sisi Wengine hatupo ktk majukwaa ya dini ila tunafaidika na hii mada kwa hivo mods usiiondoe kabisa
 
K
Kwann haikusemwa alaaniwe Ham pamoja na vizazi vyake na badala yake akasema alaaniwe canaani? Hapo ndipo panatatiza.
 
K

Kwann haikusemwa alaaniwe Ham pamoja na vizazi vyake na badala yake akasema alaaniwe canaani? Hapo ndipo panatatiza.
Kasome vzr kuna kitu utakijua..kimefichwa...inasemwa hamu alimchungulia baba yake ( alimjua) baadae mbele kunatolewa maelezo kumjua baba ni sawa sawa na nini.......????
 
Vipi misri alipoua watoto wachanga wa kiume wote eti tu kumkomoa farao,..
Yani anashinda na farao kwa kuwapa mateso wengine!!!
Hivi kabisa hadi umri uliofikia unaziamini hekaya za kwenye biblia!!black men wake up
 
Watoto wa kiume wa kwanza wa kila mmisri.Kuanzia kwa farao hadi mtu alie ndani ndani kijijini misri.Kwa hio kufiwa watoto wa kiume ilikuwa kwa wamisri wote sio kwa farao pekee.

Zaidi pale ni somo hata kwa siku zijazo.Maana yako mapigo kumi mazito kwa ajili ya watu watakaopokea chapa ya mnyama.Damu iliopakwa milangoni ina maana,, ilikuwa ishara pia kwa mambo yajayo.....


Kwa hio hizi sio hekaya bali ni mambo ya kuaminika
Vipi misri alipoua watoto wachanga wa kiume wote eti tu kumkomoa farao,..
Yani anashinda na farao kwa kuwapa mateso wengine!!!
Hivi kabisa hadi umri uliofikia unaziamini hekaya za kwenye biblia!!black men wake up
 
Kuna mambo ukiyatizama katika sura ya kimwili huwezi kuyaelewa kabisa ua unaweza usipate picha halisi.

Mimi sikuzote nilikuwa najua sababu kubwa iliyomfanya Mungu aupasue mto jordan ni ili waisrael wavuke pale maana bila hivyo wasingeweza kuvuka huo mto, katika sura ya kibinadamu ndio, Ila ila katika picha ya ulimwengu wa kiroho inakupa picha tofauti na hii inapewa uzito kwa kuwa mbona wapelelezi wavuka huo mto kwenda na kurudi bila mto kupasuka.

Pamoja na kwamba unaweza kusoma biblia, Ila lli kupata tafsiri halisi ya kilichoandikwa nilazima uitazame bible katika sura ya ulimwengu wa kiroho.
 
Hiyo ni hekaya tu ndani ya novel inayoitwa biblia,it never happened historically
 
Unapolaani uzao inabidi unaanza na Lango la familia au ukoo
Sasa Kanaani ndo alikuwa Mzaliwa wa kwanza wa Hamu
Na Wazaliwa wa kwanza wa viumbe ndio milango ya Familia au Ukoo
 
Alimchungulia uchi ndo mana wale wenzake wakaja kinyumenyume wakamfunika shuka,,angelala na mamake wangekujaje kinyumenyume
 
Alimchungulia uchi ndo mana wale wenzake wakaja kinyumenyume wakamfunika shuka,,angelala na mamake wangekujaje kinyumenyume
Mkuu kama kumchungulia Baba kwa definition ya Torati ni kulala na mke wake inamaanisha wao kuja kinyume ni reverse ya alichofanya Hamu.... Yaani wao hawakushiriki hicho kitendo na walikipinga.
 
Hapana,,,haikuji kabisa,,,
Mkuu Biblia ndio ipo hivo ngoja nkupe mstari huu
Ufunuo 22:15
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya

Je ni kweli Mbwa wataenda kuzimu?? Je hao wanaoitwa mbwa ni mbwa hawa wa kawaida??

Na sio mimi nayesema Bible ni mafumbo bali Manabii na Yesu ndio walisema hivo soma Zaburi 78:2 na Mathayo 13:10-11.

Anyway kama hiyo sio definition ya kumchungulia Baba Je Nabii Hosea alimaamisha nini kusema unamlewesha jirani ili "umchungulie"?? Ina maana unampa mtu bia ili umuangalie uchi wake alafu umuache aondoke??? Does it make sense

Karibu kwa maoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…