Uchaguzi 2020 Kwanini CCM imeweza kusalia madarakani kwa miaka yote?

Uchaguzi 2020 Kwanini CCM imeweza kusalia madarakani kwa miaka yote?

makindaOG

Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
11
Reaction score
14
Katika mojawapo ya mahojiano aliyowahi kufanya miaka ya nyuma, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alipata kuulizwa anadhani nini hasa ilikuwa siri ya Baba wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere, kudumu muda mrefu madarakani.

Bila kupepesa macho, Rais huyo alitoa jibu moja tu; He tamed the army (aliweza kulidhibiti jeshi). Hilo ndilo jibu lililokuja haraka kichwani kwake na pasi na shaka yoyote, atakuwa amejifunza mengi kiasi kwamba sasa yeye ndiye Rais aliyekaa madarakani kuliko mwingine yeyote miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki -akimzidi hata Mwalimu Nyerere aliyekaa miaka 24.

Nyerere alikuwa Rais wa Tanzania lakini hakuwa akiongoza kupitia mapinduzi ya kijeshi. Aliongoza kwanza kupitia chama cha TANU kilichopigania Uhuru wa Tanganyika na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoundwa kufuatia kuungana kwa TANU na Afro Shiraz (ASP) cha Zanzibar mwaka 1977. Kuunganishwa kwa vyama hivi kulitokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964 na nia ya kuwa na chama kimoja kinachotawala kupitia mfumo huo.

Endapo chama cha CCM kitashinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kitakuwa kimekaa madarakani kwa takribani miaka 60; na kuwa chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu kuliko kingine chochote miongoni mwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

CCM ni miongoni mwa vyama vichache vya ukombozi ambavyo bado vimesalia madarakani takribani miaka 50 baada ya nchi nyingi za Afrika kuwa huru.

Vyama vya aina yake ambavyo bado vimesalia madarakani ni kama FRELIMO cha Msumbiji, SWAPO cha Namibia, MPLA cha Angola, ANC cha Afrika Kusini. Miongoni mwa hivyo, hakuna ambacho kimekaa madarakani kuizidi CCM.

Washirika wa CCM katika harakati za ukombozi; vyama kama vile UNIP cha Zambia, UPC cha Uganda, KANU cha Kenya na vingine vya Afrika Magharibi na Kaskazini ama vimeondolewa madarakani na kugeuka kuwa vyama vya upinzani vilivyodhoofu au kuondoka kabisa katika ramani za kisiasa

_114073977_3dde75a8-28ce-4c8b-94a9-3c52149d397e.jpg
 
Kwa sababu imehakikisha ina akiba ya kutosha ya wajinga malofa na wapumbavu wengi kwenye taifa hili.
 
Mwaka huu kuna mtu mmoja ana nguvu kubwa ya umma na amesema akidhulumiwa na ccm hatamwachia Mungu.
 
Back
Top Bottom