Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Ukifuatilia kwa makini siasa za Tanzania zimeingia kwenye mtego wa ushabiki badala ya malengo chanya ya Kitaifa.
CCM imekuwa ikitumia makada wake wa uenezi kufanya siasa za kishabiki zisizo na uzamivu wenye mantiki. Hoja kubwa za wanaCCM ni namna wanavyoweza kudhibiti mihemko na kushangilia unyama unaofanywa na dola dhidi ya CHADEMA. Agenda za Vijana, uchumi, afya, diplomasia, ulinzi na usalama ziliisha miaka mingi nyuma. Leo CCM ni ushabiki, timu na kubeba mabegi.
CHADEMA, kwa upande wao wanademka na ngoma ya CCM kupitis dola. Ushabiki, kujifariji, ramli za kisiasa na hoja za kuhurumiwa hurumiwa. Kuna wakati wanakuja na hoja makini kama Katiba Mpya, Uhuru wa maoni na masuala ya haki za kijamii lakini hawana mikakati zaidi ya kutumia wanaharakati ambao hawana uanagenzi kwenye siasa za kimkakati.
Kwenye vyama vyote hivi tulivyonavyo kuna jambo kubwa wanalimiss. Kinachokosekana kwenye hoja ama mikakati yao ni WATANZANIA. Watanzania ni hoja inayopigwa chenga na vyama vingi vya siasa ikiwemo CCM na CHADEMA.
Mwaka huu tunafunga miaka 60 ya tangu tupate uhuru kama Taifa (Tanganyika). Lakini chama tawala mpaka sasa kinasimama na agenda za
Maji
Umeme
Miundombinu
.....
Wakati huo huo miaka hiyo yote tumeshuhudia anguko kubwa la
Elimu
Ajira
Ukwasi wa wananchi
Amani
Haki
Mtego ambao CHADEMA na vyama kinzani wamenasa ni kushindwa kujikita kwenye kujenga matumaini ya Watanzania kwenye agenda zao muhimu za maisha hivyo kila tunapofikia uchaguzi mkuu, wananchi wanaona bora kuibiwa kura zao kuliko kulinda ushindi halali. Wanaona heri zimwi likujualo kuliko zimwi jipya wanalohisi linaweza kuwatafuna mpaka roho zao.
Viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikwepa kuwa na tahadhari kwenye kauli zao kwa umma. Taarifa zao nyingi zinasibdikizwa na mvumo wa damu kumwagika. Hakuna mtanzania anayependa hilo.
CCM imetumia nafasi hiyo kueneza hofu na vitisho kwa wananchi dhidi ya vyama.vya upinzani. Hili ni kosa kubwa kisiasa. Ni ubaguzi mbaya kabisa kufanywa na chama kilichoongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini.
RAI
CHADEMA na vyama vya upinzani wajikite sasa kuweka mikakati ya namna watakavyotibu majeraha yaliyotokana na utendaji wenye mashaka wa serikali ya CCM.
CHADEMA na vyama vya upinzani viwapelekee wananchi matumaini ya uongozi bora, uliotukuka na kidemokrasia kwa mifano hai kutoka ndani vya vyama hivyo.
CCM inapaswa kubadilika au watajikuta wametupwa nje ya ulingo wa kisiasa kwa namna ya ajabu kabisa.
Ni wakati wa kila upande kubadilika au la waendelee na midemko wanayokwenda nayo sasa.
View attachment 1982742