Kwanini CCM wameshindwa kumfukuza Humphrey Polepole?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Wapigaji au tuwaite 'wahuni' kama alivyowabatiza Camarada Polepole ni watu wamejijenga CCM kwa maslahi binafsi. Wako na mtandao ambapo kwao CCM ni kama kampuni ya kujinufuasha kufuatana na mtu anavyokua na hisa nyingi.

Tulimsikia yule mwenyekiti wa wazazi mstaafu anayedaiwa kuuza mali za taasi hiyo kwa watu binafsi bila kufuata utaratibu kwa lengo la kujinufaisha akimdharau Polepole kwamba ni sisimizi ndani ya CCM. Akajidai eti yeye na Magufuli wakati wa kampeni ya Urais walikua wanabadilishana mashati kuonesha yeye ni mzito ndani ya chama.

Watu wenye mentality ya hivyo wakiwa ndio wanasikilizwa lazima kutakua na matatizo ya ccm kutengwa tena na wananchi tofauti na Magufuli alivyoweza kufanya CCM kuwa chama cha wanachama wote na kutumika kwa maslahi ya wote hasa wanyonge wenye kuhitaji ulinzi na kuinuliwa kiuchumi.

Magufuli alifanya mengi kupunguza gharama kwa kuhakikisha vikao vinakua na wajumbe wanaohitajika tu kwa kila vikao. Sasa tunasikia CCM kutaka kurekebisha tena katiba ili kuleta tena watendaji wa CCM kwa wingi badala ya wawakilishi waliyochaguliwa kwenye vikao kwa nia ya kupeana ulaji tu. Hapo kama nimekosea mtu anisahihishe, ila nia ni kuongeza ukubwa wa vikao bila ulazima.

Jambo lingine kubwa CCM ya Magufuli ilifanya ni kurejesha mali zote za CCM hasa majengo na viwanja ambavyo viliporwa na vigogo. Sio hivyo tu CCM ya Magufuli ilirejesha hadi kituo cha television na kituo cha radio mali ya ccm viliyokua vimeporwa na 'wahuni'

Polepole ni magufulist. Pamoja na aliyekua katibu mkuu mahiri sana walishirikiana na Magufuli kutekeleza hayo yote.

Magufuli alifanya kazi na kamati kuu ya CCM kwa uzuri na uelewano mkubwa ila sasa wahuni wenye hasira wanapotosha na kujipendekeza huku wakizua fitna na uongo ili warejeshewe ulaji na kukivuruga chama. Tumeona baadhi yao wakipewa tena madaraka makubwa kwenye chama na Serikali.

Tungependa kumtahadharisha mwenyekiti kuwa ushindi wa CCM 2020 haukutokana na hewa ila ni uongozi bora wa Magufuli kama rais wa jamhuri na mwenyekiti wa CCM. Ikiwa atawasikiliza 'wahuni' ategemee CCM kupoteza imani kwa wananchi.
 
CCM kama chama dola hakitegemei huruma ya wapiga kura, ondoa shaka mlamu.
 
Pablo Escobar alikuwa anawapa wanasiasa na wana usalama uchaguzi, ama ukubali rushwa ama ufe.
Muda mwingine huhitaji kutumia nguvu kubwa kupambana na mtu, hapa wanamtupa huko malawi basi kwisha maneno. Kama kweli ni msafi akatae uteuzi arudi mtaani aendelee kuongea
 
Anajihami kubaki chamani kwa ajili ya kesho. Kesho anaweza kupata nafasi yenye nguvu kutekeleza yaliyo sahihi. Ujue hawakuweza kumfukuza kwa sababu yuko sahihi kufuatana na katiba sera na itikadi ya ccm.
 
Haaa wapi mchumia tumbo tu. Hakuna aliye msafi wote wale wale.
Anajihami kubaki akila mema ya nchi. Angemfukuza mngemfanya nini kama aliweza watengua tengua na hakuna mlichomfanya angetaka angemtimua tu sema hana visasi wala mihemko ya hivyo.
 
Wapigaji au tuwaite 'wahuni' kama alivyowabatiza Camarada Polepole ni watu wamejijenga CCM kwa maslahi binafsi. Wako na mtandao ambapo kwao CCM ni kama kampuni ya kujinufuasha kufuatana na mtu anavyokua na hisa nyingi.

Tulimsikia yule mwenyekiti wa wazazi mstaafu anayedaiwa kuuza mali za taasi hiyo kwa watu binafsi bila kufuata utaratibu kwa lengo la kujinufaisha akimdharau Polepole kwamba ni sisimizi ndani ya CCM. Akajidai eti yeye na Magufuli wakati wa kampeni ya Urais walikua wanabadilishana mashati kuonesha yeye ni mzito ndani ya chama.

Watu wenye mentality ya hivyo wakiwa ndio wanasikilizwa lazima kutakua na matatizo ya ccm kutengwa tena na wananchi tofauti na Magufuli alivyoweza kufanya CCM kuwa chama cha wanachama wote na kutumika kwa maslahi ya wote hasa wanyonge wenye kuhitaji ulinzi na kuinuliwa kiuchumi.

Magufuli alifanya mengi kupunguza gharama kwa kuhakikisha vikao vinakua na wajumbe wanaohitajika tu kwa kila vikao. Sasa tunasikia CCM kutaka kurekebisha tena katiba ili kuleta tena watendaji wa CCM kwa wingi badala ya wawakilishi waliyochaguliwa kwenye vikao kwa nia ya kupeana ulaji tu. Hapo kama nimekosea mtu anisahihishe, ila nia ni kuongeza ukubwa wa vikao bila ulazima.

Jambo lingine kubwa CCM ya Magufuli ilifanya ni kurejesha mali zote za CCM hasa majengo na viwanja ambavyo viliporwa na vigogo. Sio hivyo tu CCM ya Magufuli ilirejesha hadi kituo cha television na kituo cha radio mali ya ccm viliyokua vimeporwa na 'wahuni'

Polepole ni magufulist. Pamoja na aliyekua katibu mkuu mahiri sana walishirikiana na Magufuli kutekeleza hayo yote.

Magufuli alifanya kazi na kamati kuu ya CCM kwa uzuri na uelewano mkubwa ila sasa wahuni wenye hasira wanapotosha na kujipendekeza huku wakizua fitna na uongo ili warejeshewe ulaji na kukivuruga chama. Tumeona baadhi yao wakipewa tena madaraka makubwa kwenye chama na Serikali.

Tungependa kumtahadharisha mwenyekiti kuwa ushindi wa CCM 2020 haukutokana na hewa ila ni uongozi bora wa Magufuli kama rais wa jamhuri na mwenyekiti wa CCM. Ikiwa atawasikiliza 'wahuni' ategemee CCM kupoteza imani kwa wananchi.
Ndiyo kafukuziwa Malawi hivyo Mkuu.
 
Back
Top Bottom