Kwanini CCM wanang'ang'ania Muungano wa serikali 2?

Kwanini CCM wanang'ang'ania Muungano wa serikali 2?

Tony Laurent

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Posts
5,606
Reaction score
7,032

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia malumbano yanayoendelea kuhusu Katiba mpya. Malumbano yaliyochukua sehemu kubwa hasa kwa wanasiasa ni kuhusu muundo wa Muungano kati ya nchi mbili za Zanzibar na Tanganyika. Na inaonekana kwamba karibu vyama vyote vya upinzani na wananchi walio wengi wameunga mkono mapendekezo ya tume ya Jaji Warioba ya kuwa na Muungano wa serikali tatu. Hoja za kupendekeza serikali tatu zimetolewa na zimeeleweka vizuri.

Mpaka sasa bado sijazielewa hoja za CCM za kutaka Muungano wa serikali 2 uendelee. Muda mwingi nawasikia watetezi wa hoja hii ya Muungano wa serikali 2 wakidai kuwa Muungano wa serikali 3 utaua Muungano. Je, utaua muungano kwa namna gani? Hapo bado sijazipata hoja zao vizuri. Vilevile hawatuelezi ni kwa jinsi gani wataziondoa kero za Muungano wa serikali 2 ambazo zimedumu kwa muda wa miaka 50 na zinazidi kuongezeka.

Ndugu wana CCM naomba muwe waungwana Tanzania ni zaidi ya CCM na ni zaidi ya maslahi binafsi ya watu wachache wenye uroho wa madaraka. Naomba muitangulize Tanzania mbele kwanza kabla ya chama chenu. Tanganyika na Zanzibar zimekuwepo kabla ya vyama vya siasa, na zitaendelea kuwepo hata bila ya CCM. Tafadhali nawaomba msituvurugie nchi zetu hizi, ambazo ni tunu alizotujalia Mwenyezi Mungu.

Najua CCM ni chama kikongwe, kina mtandao mkubwa ndani na nje ya serikali. Kwenye bunge la Katiba najua mtakuwa na wabunge wengi na mnaweza kutumia wingi huo kukwamisha muundo wa muungano wa serikali 3 kupita. Lakini kumbukeni kuwa wananchi walio wengi wamechoka na muundo wa muungano uliopo. Mkiukwamisha muungano wa serikali 3 mjue mnajimbia kaburi lenu. Na mkianguka sijui kama mtakuja kuinuka tena.

Mwisho nawakumbusha wanaCCM wote wanaong'ang'ania muundo wa Muungano wa serikali 2 kuwa "Wakati ni ukuta. Ukijaribu kupigana nao utaumia mwenyewe" Wakati tulionao ni wa Muundo wa Muungano wa serikali 3, msithubutu kupigana na WAKATI huu, mtakuja juta; na " Majuto ni Mjukuu"

Mwenye masikio ya kusikia na asikie na mwenye macho ya kuona na aone"
 
Muungano wa Serikali mbili ndio ulioifikisha Tanzania hapa tulipo. Tunaheshimika kwenye jumuiya za kimataifa kutokana na muungano huu imara
 
Wanaiogopa Tanganyika maana nayo itadai irejeshewe uhuru wake kamili kama ilivyo Zanzibar sasa. Zanzibar ina katiba yake inayoitambulisha Zanzibar kama nchi, pia una wimbo wake wa Taifa pamoja na Bendera. Nahisi hawa wanaodai serikali mbili labda wanataka muungano usiwepo (yani kuwe na Tanganyika na Zanzibar tu?). Mpaka leo baada ya zanzibar kuwa na mfumo wake kama nchi, sasa huo muungano ni wa zanzibar na nchi gani kama hatutakubali serikali 3???
 
Jenga hoja siyo kuwalaumu wenzako eti kwa nini wanakomalia muundo wa serikali mbili na wewe kwa nini unakomalia serikali unazotaka wewe.
 
Back
Top Bottom