Pre GE2025 Kwanini CHADEMA Wanamuogopa sana David Kafulila?

Pre GE2025 Kwanini CHADEMA Wanamuogopa sana David Kafulila?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Nimefuatilia mijadala mbalimbali ya kisiasa inapokuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali, iwe ni mitaani au kwenye mitandao ya kijamii. Nimekuja kugundua kuwa CHADEMA na wana-CHADEMA wanamuogopa sana Mheshimiwa David Kafulila linapokuja suala la kushindanisha na kujenga hoja juu ya masuala mbalimbali hususani ya kiuchumi.

Hoja za Mheshimiwa Kafulila zimekuwa zikiwatoa sana jasho na kuwakimbiza kama Mwenge wa Uhuru, na hakuna anayeweza wala kufanikiwa kupangua hoja zake kwa hoja na akaweza kueleweka kwa watu. Mfano mdogo ni juu ya hoja nzito ambazo Mheshimiwa David Kafulila amekuwa akieleza na kuitetea serikali juu ya ukopaji na uchukuaji wa mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa na matokeo chanya kwa uchumi wetu.

Mheshimiwa Kafulila ametoa elimu pana sana kuanzia masuala ya Marshall Plan ya Marekani ilivyozisaidia nchi za Ulaya, na namna nchi mbalimbali hata zilizoendelea kama vile Japan ambavyo zina madeni makubwa. Akaenda mbali zaidi kuelezea kwa hoja na ushahidi kuwa Tanzania siyo miongoni mwa nchi zenye madeni makubwa na kwamba uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kiwango kikubwa sana ndani ya muda mfupi wa uongozi wa Rais Samia kutoka takribani dola bilioni 66 mpaka zaidi ya dola bilioni 85. Akaelezea pia ongezeko la watalii ambalo limefikia zaidi ya watalii milioni 1.8, ambapo imepelekea kuongezeka kwa mapato mabilioni kwa mabilioni.

Mheshimiwa Kafulila akaelezea pia maana ya ujenzi wa huduma za kijamii kiuchumi zilizojengwa awamu hii ya Rais Samia. Akaelezea mfano, kwa kipindi hiki kumekuwa na mapinduzi makubwa sana katika sekta ya afya, ambapo sasa wananchi wanapata huduma za afya karibu kabisa na maeneo yao. Ambapo sasa, badala ya mtu kutumia nauli kubwa kwenda umbali mrefu kupata huduma za afya, sasa anaokoa pesa ya nauli na kuitumia kwa mahitaji yake mengine.

Mheshimiwa Kafulila ameweza na kufanikiwa kwa uhodari na umahiri mkubwa sana na kwa takwimu kuelezea mwenendo wa kiuchumi wa dunia na hali ya mikopo na madeni kwa nchi mbalimbali duniani. Jambo ambalo limewapa elimu na ufahamu mkubwa sana wananchi. Hali hii imewaacha CHADEMA hoi bin taabani hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa wao huongea kiujumla jumla tu pasipo kuwa na takwimu za aina yoyote ile, hali inayotokana na kukosa uelewa na watu wenye uelewa na elimu ya masuala ya uchumi na namna uchumi wa dunia unavyokwenda.

Ndio maana kuna wakati walikuwa wanapiga kelele kuwa mafuta ya petroli yanauzwa bei juu sana na kwamba hali hiyo inasababishwa na serikali ya CCM. Lakini walikuja kuishiwa nguvu na kupata aibu ya karne pale walipoona Wakenya mbalimbali wanakimbilia Tanzania kununua mafuta kwa kuwa bei yetu ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na nchini kwao. Hii ni baada ya serikali ya Rais Samia kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku ya bilioni mia moja kila mwezi katika mafuta na hivyo kupelekea bei ya mafuta kuwa chini ukilinganisha na majirani zetu.

Ikumbukwe bei ilikuwa imepanda kutokana na kupanda katika soko la dunia, kulikokuwa kumechochewa na kuchangiwa na vita vya Ukraine na Urusi. Ila wao CHADEMA wakawa hawaelewi kitu chochote kile maana wao hawawezagi kuangalia na kujua hali ya dunia inakwenda vipi, na kwamba wao huona kama Tanzania ni kisiwa hapa duniani.

Sasa Mheshimiwa Kafulila amekuwa akiwatwanga kwa hoja nzito na zenye ushahidi wa kutosha na takwimu sahihi, jambo linalowafanya wamuogope sana na kumuona adui wao wa kuwaumbua udhaifu wao na uongo wao na upeo wao mdogo wa masuala mbalimbali hususani ya kiuchumi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Atakapojibu hoja za Tundulisu tutamuamini
Tundu Lissu hana hoja za kustahili kujibiwa .Maana Lissu hoja zake ni za uzushi ,uongo na ubaguzi tu. Mheshimiwa Kafulila sizani kama anaweza kuwa na muda huo mchafu wa kujibu hoja zisizo na mashiko wala maslahi kwa Taifa letu.
 
Tundu Lissu hana hoja za kustahili kujibiwa .Maana Lissu hoja zake ni za uzushi ,uongo na ubaguzi tu. Mheshimiwa Kafulila sizani kama anaweza kuwa na muda huo mchafu wa kujibu hoja zisizo na mashiko wala maslahi kwa Taifa letu.
si mbaguzi ni wewe tu umeshindwa kumuelewa, hata mama alisema yeye ni mzanzibar na Tundulisu kamuita mzanzibar Mbona unapingana na mama mwenyewe anajikubali yeye ni mzanzibar?
 
si mbaguzi ni wewe tu umeshindwa kumuelewa, hata mama alisema yeye ni mzanzibar na Tundulisu kamuita mzanzibar Mbona unapingana na mama mwenyewe anajikubali yeye ni mzanzibar?
Kwani wewe huonagi anaanza kuuliza kwanini huyu anafanya kazi huku watu ni Mzanzibari? Hukuona na kusikia alichosema na kuzungumza alipokuwa Morogoro?

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere amewahi kusema kuwa dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana na ni sawa na kula Nyama ya Mtu ambapo huwezi kuacha. Lissu ni mtu Mwenye ubaguzi,chuki na roho mbaya sana.
 
Majibu ya swali lako nimeeleza vyema kabisa katika andiko langu.labda kama wewe ni wale CHADEMA wanaokimbiliaga kujibu jambo bila kuelewa hata hoja inahusu nini.
Mimi bado hujanijibu kwann mbaguzi wakati mama anakiri yeye mzanzibar Tundulisu kamuita mzanzibar, ubaguzi wake Upo wapi?
 
Kinyago wakichonge kisha kiwatishe?? Kweli

KAZI ni kipimo cha UTU
Uwezo wa Mheshimiwa David Kafulila ni uwezo wake binafsi . Na Kama ingekuwa ni hivyo kuwa CHADEMA ndio wamemtengeneza,sasa kwanini mmeshindwa kutengeneza wengine aina ya Mheshimiwa Kafulila? Mbona hakuna mwenye uwezo na uelewa mkubwa kama alionao Mheshimiwa Kafulila? Ni nani ndani ya CHADEMA unaweza kumpeleka katika mdahalo akapambane na Chuma Kafulila?
 
Yaani CHADEMA inawapa kihoro Sana. Kila siku mnaweweseka kuhusu CHADEMA.
Alleni embu niambie ni nani ndani ya CHADEMA unayeweza mfananisha au mweye Uwezo kama alionao Mheshimiwa Kafulila?

Mwisho japo siyo kwa umuhimu nijibu swali hili ambalo huwa unakimbia. Wewe ndiye yule Alleni wa kwenye kile kipindi cha Ebon Fm kilichokuwa kinakuwa kila siku ya jumamosi kukichambua masuala mbalimbali na kuongozwa na mtangazaji Neema Msafiri a.k.a Mama John?
 
Zanzibar ina ardhi yenye ukubwa kiasi gani?
Kama ni ndogo kwanini unaendelea kuutetetea muungano? Yaani unaweza kutupa faida mbili za muungano?

Kwanini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hana Usemi Zanzibar?

Kwanini waziri wa Afya wa JMT hana usemi Zanzibar?
 
Lucas Mwashambwa umesikia uteuzi wa Jana...😜😜😜

Kazi yako kujipendekeza wenzio wanateuliwa... Anza tena kuweka namba zako za simu...🏃🏃🏃
Ni uteuzi mzuri sana uliogusa mioyo ya watu wengi sana. Lakini ambao umeendelea kuiwasha na kuonyesha namna Mheshimiwa Kihongosi alivyo na Nyota kali kama ile iliowaongoza Mama Jusi kwenda alipofichwa Mtoto yesu kristo
 
Back
Top Bottom