Sasa Pasaka na mimba ya Yesu wapi na wapi? Halafu una uhakika Yesu alitungwa mimba mwezi wa 6? Nenda kasome upya, ule sio mwezi wa sita like June, ni miezi 6 since malaika Gabriel alipomtokea Zakaria na mkewe Elizabeth kuhusu mimba ya nabii Yohana mbatizaji; in other words, Yesu na Yohana mbatizaji wanatofautiana miezi 6 kuzaliwa.
Now back to the topic (yote haya ni kwa mujibu wa mtazamo wangu baada ya kuisoma Biblia ). Nadhani hiyo pasaka, ulitaka kusema Christmas na sjo Pasaka; kwa ufupi hata mimi siamini kama Yesu alizaliwa tarehe 25 December. Hi siku ni ya kubuni, sio siku sahihi. Ninazo sababu kubwa 2, moja ambayo ni ya uhakika ni hi, sherehe zote za Kikristo zina mizizi agano la KALE, Pasaka, Pentecost, Ijumaa kuu nk zote zilianza kwenye agano la kale; yaani matukio yote ya Yesu na kanisa, misingi yake iliwekwa kabla Yesu hajazaliwa, kwasababu ya muda sitazifafanua hizo sherehe maanake zipo wazi sana kwa Biblia, Kristmas haipo, sio miongoni mwa hizo sherehe. Sababu yangu ya pili ni ya kutokuamini kwamba Yesu hakuzaliwa mwezi December ni ya Kijiografia na kihistoria. Biblia inasema, wakati Yesu anazaliwa, kulikua na baadhi ya wachungaji wako porini wakichunga wanyama wao (you may put kondoo hapa ) ilikua usiku or alfajiri; kwa mujibu wa majira ya kijografia na kihistoria, mwezi December ni kipindi cha baridi kali sana and hence wasn't possible kwa watu kua nje usiku or alfajiri; kipindi hicho wachungaji walikua wanawalisha mifugo yao akiba ya chakula ambacho walikiandaa miezi ya joto. Kwasababu hizo 2, Yesu hakuzaliwa December, possible ilikua kati ya September or August.