Kwanini Comedians wa MIZENGWE wanapotezewa sana?

Azarel

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
28,916
Reaction score
40,479
Habarini Wadau,

Mbona waigizaji wa Mizengwe ni wazuri sana na wana vipaji ila hawapewi recognition sana kama comedians wengine?

Japo kipindi chao cha jumapili kinachorushwa na ITV ni kifupi ila watu kama SUMAKU, MKWERE, MARINGO 7 na wengineo ni waigizaji wazuri kweli, haswa Sumaku.

Pia michezo yao ina mafunzo kwa jamii.

Kwanini wanasahaulika?
 
Majibu yake ni marahisi kama siyo mepesi sana Mkuu....

Hawa ' Jamaa '....

  1. Hawajui ' kujipendekeza ' wala ' kujikomba ' kwa Mtu na hawaendekezi sana ' njaa '.
  2. Wanapambana sana na kujituma mno wenyewe.
  3. Hawataki kujihusisha na kuwa ' mabegi ' ya Drugs barons wa Tanzania kama wanavyofanyiwa wengine.
  4. Wanaridhika na kumshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa chochote kile anachowapa kwa ' Jasho ' lao na kamwe hawapendi ' magumashi ' kama wenzao wengi.
  5. Tungo zao nyingi tena 100% ni za ukweli mtupu na usisahau kuwa 100% ya Watanzania hatupendi kuambiwa ukweli.
 
Nimekuelewa vizuri sana Mkuu.
 
Mimi nashauri waongezewe muda kwenye kipindi maana robo saa wanayopewa haitoshi.
Lingine comedy yao haichoshi na nawasifu wanaigiza ktk uhalisia wao, mfano kama sehem inahitaji mwanamke basi atacheza mwanamke sio wale wengine midume inavaa wigi na kupaka lipshine kama unaangalia huku unakula ni kichefu chefu tosha.
 
Kashkash group ndio kipindi pekee cha vitimbi kilichomakinika isivyomithirika,waigizaji wake wanajua nini wanafanya na anaewaandalia anajua kazi
 
Habarini Wadau,

Mbona waigizaji wa Mizengwe ni wazuri sana na wana vipaji ila hawapewi recognition sana kama comedians wengine?

Japo kipindi chao cha jumapili kinachorushwa na ITV ni kifupi ila watu kama SUMAKU, MKWERE, MARINGO 7 na wengineo ni waigizaji wazuri kweli, haswa Sumaku.

Pia michezo yao ina mafunzo kwa jamii.

Kwanini wanasahaulika?
hawa jamaa ni mafundi wakali, toka mizengwe ya max na zembwela, baada ya max kufariki ikaitwa mizengwe.. hiyo ndio comedy ninayoipenda na kuikubali zaidi Tanzania kila jumapili wanaleta kitu kipya, kizuri, kifupi, na chenye mafunzo mahususi.
 
Kwani tanzania kuna Comedian?
hahaaaaa wajifunze kwa wenzao basi
sio kuchekesha maneno bali vitendo. kama maneno kwa asiejua lugha hiyo je?
hawaoni wanavochekeaha wenzao kina Mr Bean kina Chaplain au Kelvn Hart...
ndomaana me siangaliagi utumbo huo wa Mizengwe nk.
 
Sasa kama huangalii, umejuaje kuwa wanahitaji kujifunza kwa hao uliowataja? Na haitwi Kelvn Hart, ni Kevin Hart.
 
Back
Top Bottom