Kwanini Congo DRC?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kuna nchi zilishawahi kuingia katika misukosuko ya kisiasa lakini hatimaye zilikuja kutukia. Rwanda ni mojawapo.

Kwanini imekuwa tofauti nchini Congo DRC?

1. Tatizo ni uongozi? Angepatikana huko kiongozi kama NYERERE, au KAGAME au MAGUFULI angeweza kuituliza?

2. Wasababisha machafuko ya Congo DRC wana nguvu kuliko wazuiaji?

3. Hulka ya raia wa Congo DRC inachangia?
 

..Ni kwasababu waasi wa DRC wanasaidiwa na Uganda, na Rwanda.

..waasi wanapokuwa na support ya nchi majirani basi ni vigumu sana kuwamaliza.

..Jonas Savimbi alikuwa moto kwelikweli Angola, lakini misaada toka Afrika Kusini na Zaire/DRC ilipokatika Savimbi aliisha makali.
 
Sababu wana Mali, leo hii Congo ikifungwa hakuingii hakutoki Kitu nchi nyingi za west zitakua katika hali ngumu sana.

Congo ndio wana run Dunia kwenye mambo mengi sana na Madini yao ni crucial kwenye Technology za sasa. Mabwana wakubwa hawataki wajitawale na kujielewa ili mambo yao yaende.
 

..sio kweli kwamba nchi za magharibi hazitaki Wacongo wajitawale.

..nchi za magharibi hazijali mateso ya Wacongomani kwasababu supply ya madini kwenda kwao haijakatishwa kutokana na vita na mauaji yanayoendelea DRC.

..siku vita hivyo vikisababisha nchi za magharibi zikakosa madini muhimu toka DRC ndipo utakapoona wanaingilia kati na kutaka vita iishe.
 
Wale waasi wa congo niwa kutokea nchi gani ya magharibi?
 
Jibu nzuri kabisa hili mkuu,wengi wetu ni watu wa kutoa lawama kwa wazungu kuhusu mgogoro wa DRC na kuzipa kisongo sababu za ndani ambazo ni chanzo Cha matatizo ya Congo.
 
Jibu nzuri kabisa hili mkuu,wengi wetu ni watu wa kutoa lawama kwa wazungu kuhusu mgogoro wa DRC na kuzipa kisongo sababu za ndani ambazo ni chanzo Cha matatizo ya Congo.

..nchi za magharibi zitakuingilia ikiwa utafanya mambo yafuatayo.

1. uwa au chukua mateka raia wao.

2. kata supply ya rasilimali ambazo ni muhimu kwa uchumi wa nchi zao.

..mtawala asipofanya hayo mawili, hata awe muuaji, au ale nyama za wananchi wake, nchi za magharibi hazitamuingilia.
 
Tokea Kagame aingie madarakani, Rwanda imetulia mithili ya maji kwenye mtungi.

Unafikiri Kagame angelikuwa ni Rais wa Congo DRC hayo machafuko yangelikuwa bado yapo?
 
Tokea Kagame aingie madarakani, Rwanda imetulia mithili ya maji kwenye mtungi.

Unafikiri Kagame angelikuwa ni Rais wa Congo DRC hayo machafuko yangelikuwa bado yapo?

..Rwanda imetulia kwasababu majirani zake hawana nia mbaya ya kuwasaidia maadui zake.

..Ukumbuke kwamba bila msaada wa Uganda Kagame asingeweza kuingia madarakani.

..jiulize kwanini mpaka wa DRC na Tanzania, Angola, Afrika ya Kati, Sudani ya Kusini, au Zambia, hakuna matatizo.
 
Japo hatuifikii Congo, lakini hata sisi utajiri tulio nao si haba! Lakini mbona sisi tuna "amani"?

Huoni kama na Wacongo nao wamechangia hayo yanayoendelea nchini kwao?
 
AU yenyewe "hainaga" msaada?
 
Wale waasi wa congo niwa kutokea nchi gani ya magharibi?
Hao wanaoiba Madini ni kutoka nchi za Magharibi, in short vifaa vyote tunavyotumia kutype hapa vimejaa damu za Wacongo. Bila cobalt hutengenezi battery na circuit za motherboard, na Congo ndio ina supply Asilimia zaidi ya 70 ya Cobalt duniani, wanaochimba hio cobalt ni watoto wadogo mno na ni kama serikali ya Congo haifadiki na chochote.

Kukiwa na Congo imara ina maana watakuwa na say na Cobalt yao. Bei itapanda na wanaweza wakamuuzia yoyote, China, Urusi na wengineo, na tukiwa tunaelekea ulimwengu wa Magari ya Umeme umuhimu wa cobalt unazidi kuwa Mkubwa.

So solution ni hio ku distabilize nchi ili watu wajichotee hizo Mali,

Mwanajeshi halimi, hafanyi biashara wala haingizi kipato chochote na ana Gharama kubwa mno, kuanzia kumvisha, kumlisha, kumnunulia Silaha, kumtrain etc hakuna popote pale Duniani ambapo kuna muasi asiye supportiwa na nchi nyengine, hakuna, huwezi endesha jeshi kwa ulimwengu wetu wa sasa bila Supply na Logistic za hao mabwana wakubwa.
 
Nchi nyingi zina mali lakini zina utulivu, why DRC? Shida ni uongozi na hulka ya Wacongo wenyewe.
 

..wanaoiba ni wacongo, wanyarwanda, na waganda, halafu wanauza kwa nchi za magharibi, china, na kwingine.

..wanachojali nchi za magharibi na china ni kupata madini. Hawajali aina ya mtawala aliyepo Congo, na kama kuna amani, au la.

..Congo ingekuwa na amani bado kungekuwa na option ya rushwa kama njia ya nchi za magharibi na China kuendelea kufaidi rasilimali za Congo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…