Kwanini Congo DRC?

Umekazania cobalt cobalt kama vile Congo pekee ndio inahodhi hayo madini
Cobalt yenyewe ina alternatives, sio kwamba hata isipokuwepo kwamba smartphones, computer, betri havitatengenezwa.
 
Mnawasingizia tu hao wazungu. Mbona hata Mugabe na Dos Santos walimsaidia kabila dhidi ya kagame ila bado wakagawana dhahabu zote na mafuta!! Tuseme tu uongozi mbovu sababu jamii zetu hazina uwajibikaji wala maadili zaidi ya wizi tu.
 
Wale waasi wa congo niwa kutokea nchi gani ya magharibi?
waasi hao ni watu wachache wenye urafiki wa karibu na mataifa ya magharibi, watu hao wanatumiwa na wamagharibi,huku wao wakipewa na kuahidiwa maisha mazuri,wakati nyie wakongomani wazarendo mnafanya jitihada za kuwamaliza waasi wamagharibi wanapora mali kupitia hawa waandishi wa habari wasio na mipaka,vikosi vya misaada nk.
 
Ndio namshangaa wakati kila siku tunaona vita za EVs batteries kwa mataifa makubwa kwa makampuni yao
 
Sio kweli, Tanzania mbona tuna rasilimali na hakuna waasi. In fact wazungu wanajichotea almasi tu dhahabu kwa mikataba mibovu ndio sembuse watake vita.

Unataka kuniambia DRC bila vita hao viongozi hawahongeki?

Tuache kusingizia wazungu, hata Mugabe aliachiwa kila kitu ila bado nchi ikamshinda kwa kunuka ufisadi.
 
Nyie wapuuzi sana.

Races hizi mbili waarabu na sisi waafrika ni wapuuzi wapuuzi kila aina ya ujinga wetu tunatafuta wa kumtupia lawama
 
Tokea Kagame aingie madarakani, Rwanda imetulia mithili ya maji kwenye mtungi.

Unafikiri Kagame angelikuwa ni Rais wa Congo DRC hayo machafuko yangelikuwa bado yapo?
jibu ni ndiyo,hata ashuke malaika aitawale CONGO vita havitaisha mpaka pale rasilimali zote za nchi hiyo ziishe.
 
Kumbe!! Mbona Mugabe na Dos Santos walipomsaidia kabila dhidi ya Kagame waliyedai katumwa na wazungu, wakaishia kutapanya rasilimali za Katanga? Yaani Mugabe walichota mabilion ya dola kwenye dhahabu kama "marejesho" kumsaidia kabila.

Kwahiyo naweza kusema wote ni wale wale tu, hata waafrika wenyewe kwa wenyewe tunaibiana tusisakizie wazungu
 
Sahihi.

Tanzania hapa kila siku tunaibiwa kwa mamikataba ya kipuuzi tuliyo saini wenyewe kwa 10% na hatuna hayo mambo ya vita vita kama Congo
 
Japo hatuifikii Congo, lakini hata sisi utajiri tulio nao si haba! Lakini mbona sisi tuna "amani"?

Huoni kama na Wacongo nao wamechangia hayo yanayoendelea nchini kwao?
tuna amani ila hatuna akili "wajinga" wamagharibi watatumia mgongo wa waasi kivipi ktk nchi kama hii,bandari,mbuga za wanyama,mikataba ya madini na wafadhili uchwara wanafanya yao pasipo wananchi kushtuka au kugomea.
 
Boss tuongee kwa ushahidi, speculation na cheap politics hazifikishi popote. APPLE na west wanaiba its a fact, wanatumia Rwanda it's a fact, kuna mkataba wa EU na Rwanda kusupply it's a fact japo Rwanda hana any meaningfull material. China anashirikiana na Serikali ya Congo it's a fact pia.

Kama China Anaiba si kitu kizuri ila atleast anaingiza hela serikalini na ana Contribute kwenye Uchumi, ila wanachofanya west ni kutolipa Chochote serikalini, kushirikiana na serikali nyengine kununua kitu ambacho sio Chao, kununua bidhaa toka kwa waasi kwa kuwapa silaha na kupokea Madini etc.
 
Rasilimali gani Tanzania zenye thamani ya zaidi $24 trillion? Nyie Acheni Utani hatuna Madini yenye hata thamani ya 1% ya Madini ya Congo. Tuki Export 1.4B Madini humu tunapongezana.
 
Mnawasingizia tu hao wazungu. Mbona hata Mugabe na Dos Santos walimsaidia kabila dhidi ya kagame ila bado wakagawana dhahabu zote na mafuta!! Tuseme tu uongozi mbovu sababu jamii zetu hazina uwajibikaji wala maadili zaidi ya wizi tu.
So kama wamegawana mafuta does that make wazungu innocent? Siku Kenya wakichukua Dhahabu Tanzania automatic vinafanya mikataba yote ya Madini Tanzania iwe sawa?
 
Rasilimali gani Tanzania zenye thamani ya zaidi $24 trillion? Nyie Acheni Utani hatuna Madini yenye hata thamani ya 1% ya Madini ya Congo. Tuki Export 1.4B Madini humu tunapongezana.
Rasilimali gani? Si mradi wa gesi ya LNG huko kusini investmest will be over USD 30B.

Anyway hata Hizo hizo chache mbona mabeberu wanazikomba bila kurusha risasi
 
Rasilimali gani? Si mradi wa gesi ya LNG huko kusini investmest will be over USD 30B.

Anyway hata Hizo hizo chache mbona mabeberu wanazikomba bila kurusha risasi
$30B ni 0.125% ya $24 Trilioni, hata nusu asilimia huja fika, see?
 
So kama wamegawana mafuta does that make wazungu innocent? Siku Kenya wakichukua Dhahabu Tanzania automatic vinafanya mikataba yote ya Madini Tanzania iwe sawa?
Ndio nasema issue sio wazungu issue ni mtambuka. Hata leo DRC isiwe na vita unadhani Viongozi wake watatoa mikataba mizuri ya rasilimali?
 
Vita vya DRC vina mambo mengi sana yanayochangia kama mchanganyiko.

Ukianza na ukoloni, aina ya wakolini imekuwa na athari za muendelezo katika nchi nyingi. Wafaransa, Wareno na Wabelgiji walikuwa wakoloni wabaya zaidi kuliko Waingereza, Wajerumani na Wahispania. DRC ilikuwa kama shamba tu la mfalme Leopold wa Ubelgiji, hakuwa na mpango wowote wa mbeleni zaidi ya kuchuma rasilimali. Waingereza wao walikuwa wanachuma rasilimali huku wakiamini wana mission ya kuwapa ustaarabu raia wanaotawala pia ndio maana walikuwa wanafanya hata na maendeleo na hata kuondoka kwao kulikuwa kwa mpangilio na utaratibu unaoeleweka. Congo haikuwa hivyo na watawala wao Wabelgiji.

Ukabila pia ni tatizo kubwa sana kwa mataifa karibia yote ya Africa, unapokuwa na taifa kubwa kama DRC lenye makabila zaidi ya 250 hali inakuwa ngumu zaidi. Viongozi wengi wa Africa wako tayari kuzungukwa na watu wajinga mradi tu ni makabila yao kuliko watu smart kutoka makabila mengine.

Jiografia ya DRC nayo ni matatizo kwake, inazungukwa na nchi 9 ambapo nchi 2 ndizo haziajawahi kuwa na vita vya ndani, nchi kubwa sana kuwa landlocked bila access ya bahari ni changamoto, madini yanapitakana mipakani mwa nchi jirani, sehemu kubwa ya nchi ni ikweta inafanya vigumu sana kupigana vita misituni.

Mwisho ni kwamba mataifa mengi ya Africa hayakujitafuta yenyewe kuwa mataifa, yalipatikana kwa watu kukaa mezani tu na kuchora mistari kama mipaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…