SoC04 Kwanini Daftari la Kudumu la wapiga kura watanzania wasijiandikishie NIDA

SoC04 Kwanini Daftari la Kudumu la wapiga kura watanzania wasijiandikishie NIDA

Tanzania Tuitakayo competition threads

pute kitogo

Member
Joined
Apr 26, 2024
Posts
6
Reaction score
3
KWANINI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WATANZANIA WASIJIANDIKISHIE NIDA

Kubadilisha mavazi, Tabia, Magari, Nyumba na Majumba sio dhambi na sio kosa kisheria kama vitu vyote vyako hivyo kubadilika sio tatizo basi ni kheri tubadilishe Tanzania ya sasa kwa mafanikio ya baadae.

Kutangaza nafasi za ajira kwa kazi moja kila mara inachosha tunatakiwa kubadilika emu tubadilikeni kuna haja gani kila baada ya miaka 4 watu waombe kazi za kuwaandikisha watu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati kazi hiyo inaweza ikafanyika Nida na watu wakaondokana na usumbufu wa kupanga foleni kwenda rudi kwa sababu taarifa zake kutokamilika kwa wakati, kugombana na wafanyakazi kwa kutoelewana yani bado kuna usumbufu mkubwa ungeondoka kama kila kitu tungemaliza Nida.

Mtanzania akifikisha miaka 18 anasifa ya kuomba na kupatiwa vitambulisho vya Taifa, vya kupigia kura na kuandikishwa kwenye daftri la kudumu la wapiga kura vitu vyote mtu anaweza kupata sehemu moja na kuondoa gharama zingine mbalimbali

Aidha akipata namba ya Nida awekwe moja kwa moja kwenye daftari la kupiga kura na baadae apewe kitambulisho cha wapigia kura maana kwenye ofisi za Nida kazi zote zinaweza kufanyika na kukamilika kwa muda mfupi

Pia utaratibu wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga umetofautiana kidogo na taratibu za kuomba kupata kitambulisho cha Taifa kwa nini watu wasumbuke namna hiyo wakati tunaweza kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja na kwa wakati moja hahaha Tz hii kazi kweli kweli haya tuendelee labda ipo siku itabadilika

Ofisi za Nida (vituo vya Nida vya Wilaya ambazo watu wanaenda kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa) ziwe na kitengo cha Tume Huru ya Uchaguzi ambacho kazi yake kubwa ni kuwaweka watu kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura na mtu ataenda kwenye kitengo hiko baada tu ya kupata namba ya Nida na itafanyika siku atakayokuja kuchukua namba yake ya Nida kwenye kituo alichojiandisha

Nida watatuma taarifa zote za mtu husika kwenye kitengo cha Tume Huru ya Uchaguzi ambazo zipo kwenye kituo hiko tena taarifa zake zitatumwa baada tu ya mtu kupata namba yake ya Nida

Hata hivyo namba ya Nida mtu akipata maana yake mtu huyo taarifa zake ni sahihi ndiyo maana anapewa namba ya Nida, Kwa usumbufu aliyopata mtu huyo kwenye kupata namba ya Nida akitaka awepo kwenye daftari la wapiga kura basi lazima atapata tena usumbufu ule ule sio sawa muda ni pesa na mambo ni mengine.

Tunajua mtaka cha uvunguni sharti kuinama ila kuinama sana kunachosha sio kila mahali kuinama hahaha na furahi kidogo kwa sababu nimekumbuka mtaani wanapita wachekeshaji wanatumia msemo huo ila wao wasema ukitaka cha uvunguni betua kitanda na kama inawezekana basi sawa fanya hivyo tu

Hivyo basi mtu akipata namba ya Nida ni bora hapo hapo taarifa zake ziwekwe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura itasaidia kuondoa muda mrefu kujiandikisha pia tutakuwa na uwakika kuwa watu wote waliowekwa kwenye daftari hilo ni watanzania

Kuweka utaratibu huu utaondoa gharama kubwa ambazo zingesaidia kwenye shughuli zingine mfano kuwalipa posho/mishahara wafanyakazi watakaosaidia watu kujiandikisha ambao kwa siku wanalipwa 60,000/= ukipiga mara 7 unapata 420,000 zoezi likichukua wiki na zikiongezeka siku yingine basi hapo pesa inaongezeka wakati pesa hiyo angelipwa mtu kwa mwezi angefanya kazi kubwa na ukumbuke pesa hiyo ni kubwa zaidi ya mshahara wa baadhi ya walimu na watumishi wengine wa umma

Posho hizo ni kubwa ukipiga na hesabu za mshahara ndiyo usiseme achana na hilo gharama zinazotumika kuchukua barua kwa Mtendaji wa Kata na kuzipeleka kwenye sehemu husika, gharama za kutengeneza vitabu vya kusaini kwa watakaoleta barua za maombi na zile pesa za semina kwa watakawafundisha wale ambao waliochaguliwa baada ya kutuma maombi

Kuna zile gharama za kila mwaka watu wanaotuma maombi za kazi ni kubwa iwe kwa serikali au mtu moja moja sasa piga kwa kila baada ya miaka 4 halafu ajira zenyewe ni fupi sio ajira za muda mrefu
Kuondoa utaratibu huu pia utaweka ajira za kudumu na kuondoa ajira za muda mfupi ambazo zinamaliza hela yingi za watanzania kwa muda mfupi halafu kazi inafanyika kwa kiwango cha wastani kwa sababu sio watu wote wataandikishwa siku hiyo wakati kama tukisema tuondoe utaratibu huo watu wengi wataandikishwa ambao ni watanzania tutakuwa tunauwakika nao kwa sababu taarifa zao watapewa na Nida.

Serikali imejitahidi kuweka utaratibu ambao kila mtanzania kwa hiyali yake anaenda Nida kuomba kupatiwa kitambulisho ili asikwame kwenye jambo analolifuatilia hapa serikali imeweza hongera sana ndiyo maana watu wengi wanajiandikisha je kuna utaratibu wowote ambao unawezekana kuwekwa ili watu wengi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura??

Hapana kwa sababu mtu hawezi kudhuhuliwa kazini au jambo lolote akadhuhuliwa hadi ajiandikishe kwenye daftari hilo ni ngumu huku watu wanakuja kwa kupenda tu ndio maana ni bora waandikishiwe Nida kwa sababu watu wengi wanaenda Nida

Tuweke utaratibu huu ili vijana wa leo wengi wajiandikishe na kazi itabaki kwao wapige kura au wasipige, watu wengine wanashidwa kupiga kura kwa sababu taratibu za kupata kitambulisho cha wapiga kura ni ndefu zinachosha ila tukisema tuwapate Nida tutawapata wengi

Kuna rafiki yangu moja alienda mbali zaidi akasema kuwekwe utaratibu wa vitambulisho vya Taifa kwa waliochini ya miaka 18 maana yake mtu akizaliwa tu basi anaandikishwa na kupewa kitambulisho hiko halafu akifika umri wa miaka 18 anaenda kwenye Ofisi za Nida kufanya kuupdate hahaha tuache na mawazo hayo ya vijana wa sasa hivi

Nimemaliza sina cha kuongeza kama utaratibu mzuri basi ni kheri viongozi wanaona watanzania wanaona basi tufanye mabadiliko
 
Upvote 2
Mtanzania akifikisha miaka 18 anasifa ya kuomba na kupatiwa vitambulisho vya Taifa, vya kupigia kura na kuandikishwa kwenye daftri la kudumu la wapiga kura vitu vyote mtu anaweza kupata sehemu moja na kuondoa gharama zingine mbalimbali

Aidha akipata namba ya Nida awekwe moja kwa moja kwenye daftari la kupiga kura na baadae apewe kitambulisho cha wapigia kura maana kwenye ofisi za Nida kazi zote zinaweza kufanyika na kukamilika kwa muda mfupi

Pia utaratibu wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga umetofautiana kidogo na taratibu za kuomba kupata kitambulisho cha Taifa kwa nini watu wasumbuke namna hiyo wakati tunaweza kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja na kwa wakati moja hahaha Tz hii kazi kweli kweli haya tuendelee labda ipo siku itabadilika
Moja kwa moja katika pointi.

Mtu akifikisha miaka 18, anaandikishwa NIDA na inampa kila haki. Sahili kabisa!

Kuna wakati nilisikia kuwa utaanzishwa utaratibu wa namba ya jamii (social security) kwa ajili ya mambo hayo sijui ilifikia wapi. Lakini nadhani ndiko tunakoelekea kama Taifa.

Wazo zuri likitekelezwa hatutahitaji tena sensa kila baada ya miaka, kila kitu kitakuwa online mwanangu.

Nyongeza tu kwa vyombo vya usalama ni usalama wa taarifa hizo. Cybersecurity. Maana taarifa zote zikiwa katika kapu moja halafu ulinzi usuesue kwa kweli ni hatari sana kwa privacy/faragha. Itabakia kuwa ni bora tubakie zama za mawe
 
Back
Top Bottom