Kwanini Diamond Platnumz anavaa msalaba?

Jibu ni rahisi sana. Walioandika vitabu vya Agano Jipya walikuwa Wayahudi lakini waliandika kwa Kigiriki sababu ndiyo lugha kuu iliyokuwa inatumika kipindi hicho eneo lote la mashariki ya kati.

Mfano ni kama sisi Watanzania, tunaongea Kiswahili lakini sheria zetu zote zimeandikwa kwa Kiingereza.
 
Wewe bado una safari ndefu sana ya kujifunza.

Vitabu vya Agano la Kale viliandikwa kwa Kiebrania (Hebrew) na baadhi viliandikwa kwa Kiarameiki (Aramaic).

Vitabu vya Agano Jipya vyote viliandikwa kwa Kigiriki (Koine Greece).

Huo ndiyo UKWELI na hakuna ubishi katika hilo.
 
Unabishana na KJV haya.. [emoji38]
Ninajua ninachokiongea na nina uhakika wa asilimia 100% wala sibahatishi.

KJV= King James Version hii ni Biblia iliyotafsiriwa mwaka 1611 huko Uingereza. Kabla ya hapo kulikuwa hakuna KJV bali ilikuwepo Biblia ya Kwanza ya Kiingereza iliyoitwa The Geneva Bible ambayo ilitafsiriwa mwaka 1557 na kuchapishwa mwaka 1560.

Kabla ya hapo maandiko yote matakatifu yalikuwa katika lugha ya Kiebrania na Kigiriki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…