KWANINI Dola yetu inawaabudu sana wawekezaji wageni?

KWANINI Dola yetu inawaabudu sana wawekezaji wageni?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Kwanini DOLA yetu inawaabudu sana wawekezaji kutoka nje?


Katika kampeni za JK za Uraisi za mwaka 2010 alisisitiza ya kuwa bila ya misaada nchi haiendesheki! Kwa lugha nyingine ni kuwa nchi hii siyo ya kujitegemea kama katiba inavyotamba bali ni nchi inayoendeshwa kwa huruma za wageni.



Wanasiasa wote hudai kuamini ya kuwa nchi hii itajengwa na watanzania wenyewe. Lakini inapokuja utekelezaji imani hii huwekwa kando na wageni kutukuzwa kama miungu wadogo hususani kwenye maeneo yafuatayo:-



1) Hupewa misaada na dola ya misamaha ya kodi ambayo ni ya kibaguzi na hivyo katiba ya nchi hukiukwa. Misamaha hiyo hufifilisha dhana nzima ya ushindani na hivyo kuondoa makali ya nguvu za soko na kukatisha tamaa wawekezaji wa ndani kwenye fani husika ambao hawakupewa misamaha tajwa.

Dola inayojiheshimu na ambayo ingependa iheshimiwe kwenye sheria zao hukataza misamaha ya kodi ya aina zozote na kuhakikisha misamaha kama ipo inufaishe walengwa wote waliowekeza kwenye sekta husika.



2) Sera ya “mwenyeji mpishe mgeni” huchachamaa sana kwa hoja zisizo na mashiko ya kuwa mwekezaji mgeni atazalisha ajira, kuleta kasi ya maendeleo wakati ukweli ni kuwa kazi ya kuamua hilo lilikuwa lifanywe na mwenyeji ambaye serikali badala ya kumwezesha kwa sheria inamdumaza na kumfilisi kwa sheria hizo hizo kwa fidia kiduchu na kusukumwa maeneo ambayo hayana rutuba au mbali na mvuto wa kisoko.



3) Dola kwa kutupiwa “peremende” ambazo hufichwa kwenye akaunti za ughaibuni za baadhi ya wanasiasa na watendaji waandamizi serikalini basi huwa ni kichocheo cha kumdhulumu raia na kuhakikisha mwekezaji mgeni ndiye mwenye haki na raia mwenyeji kuonekana ni msumbufu na anachelewesha maendeleo.


4) Jitihada zinafanyika hata kuwawezesha wazawa ambao waliukana uraia na kujiandikisha uraia wa nchi nyingine kwa kuwavika vilemba vya ukoka kama “Balozi maalumu” ili kuwasaidia waandamizi tajwa katika kujenga mazingira ya kuwafilisi wenyeji raia hata kila kidogo walichonacho.


5) Mwekezaji mwenyeji anaonekana ni mnyonge sana na hivyo hastahili kuwezeshwa zaidi ya kuandaliwa awe manamba wa kulipwa kiduchu na mwekezaji mgeni.

6) Pamoja na mwekezaji mwenyeji kuonekana si mali kitu inapokuja dhana nzima ya kujitawala wenyewe waandamizi tajwa huwa wakali wanaposhurutishwa kukabidhi dola kwa hao wageni kwa sababu kwa kufanya hivyo watakuwa wamesalimisha mkate wao.

Swali langu huwa hivi yawezekana kweli tuwe huru kisiasa bila ya kuwa huru kiuchumi? Kama uhuru wa kiuchumi tunawamilikisha wawekezaji wageni ni kwa sababu ipi inatuzuia tusiwamilikishe na dola pia? Kama hatuwezi kwenye nyanja ya kiuchumi yawaje tuweze nyanja ya kisiasa?


7) Nguvu ya kiuchumi ya vyama vya siasa na wagombea kwenye nafasi za juu za taifa hivi sasa kimyakimya zinategemea sana ruzuku kutoka kwa makampuni makubwa kutoka nje. Kwa vile tumefikia hatua kuwa gharama za kampeni za kupata uhalali wa kusimamia dola zinatoka kwa wawekezaji hao wakubwa hivi uhuru wetu hata huo wa kisiasa sasa uko wapi?



8) Jitihada za kumwezesha mwekezaji wa ndani zinadhoofishwa na viwango vikubwa vya kodi, urasimu wa kuanzisha na kuendeleza biashara ikiwa na pamoja na mtazamo wa serikali kuwa mwekezaji wa ndani siyo mwekezaji bali mbabaishaji tu.

 
Mkuu, kwenye aya yako ya kwanza ukisoma neno kwa neno utakuta kila kitu kimejieleza na jibu tayari liko ndanimwe.

Labda kwa kuongezea tu ni kwamba kuna msemo usemao kua "Historia ni mwalimu" na mwingine husema "Historia hujirudia".

Tukitumia msemo wa kwanza tunarudi nyuma miaka ya 1800 (samahani mtanirekebisha kama nimekosea) enzi za chifu Mangungo wa Msovero aliyedanganywa kwa vijizawadi vya bure na Carl Peters kisha kuachia ardhi ya wazawa kwa taifa la Ujerumani. Mambo yalianza taratibu kama mvua za rasharasha kisha yakaja masika hatimaye wazawa wakajikuta wako chini ya mkoloni wakitumikishwa kama manamba mchana kutwa tena kwa ujira mdogo usiokidhi mahitaji. Mambo yaliendelea kwa mtindo huo hadi ukoloni ukaenea Tanganyika yote kupitia watemi na machifu wa koo na kabila mbalimbali hapa nchini.

Tukitumia msemo wa pili utaona wazi kuwa sasa tumeanza kurudi kulekule enzi za kina chifu Mangungo ila hapa tofauti ni kua kina Mangungo wa leo ni wasomi na wana shahada za uzamili mpaka wengine za uzamivu.

Mbaya zaidi kina chifu wetu wa zama zetu wanatumia dola zetu kusaidia kupokonya mali zetu huku wakitumia kila njia na namna wawezayo ili mradi kina bwana Carl Peters na kina bwana Edward Twinning waweze kujichotea rasilimali zetu.

Kwa hiyo ndugu mleta mada mimi naona tunazitukuza dola za kigeni na kupuuza dola zetu pamoja na utu na thamani yetu kwa kua kina Mangungo wetu wameacha kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ili kutuletea maendeleo na badala yake wameamua kufuata matakwa ya kina bwana Carl Peters kwa kugombea vijikanga vya kusitiri miili yao, viatu vya kuvaa miguuni na shanga za kuvaa shingoni bila kujua kua wanatutia vitanzi sisi akina manamba (au manamba watarajiwa).

Narudia tena, "Historia ni mwalimu" na "Historia hujirudia".
 
Tanzania kuna sera nzuri za uwekezaji tatizo ni watendaji wenu wana njaa sana na wabinafsi wapenda rushwa.
 
umenikumbusha mwandishi Dambisa Moyo aliyewahi kusema kwamba anatamani nchi za Afrika zijitegemee 100%
 
Back
Top Bottom