sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Elimu ya sasa inaonekana haina thamani ukilinganisha na zamani kwa jinsi zamani msomi alikuwa akiheshimiwa.
"shule ya msingi niliyosoma nakumbuka tulimaliza kama 80 lakini tuliofaulu kwenda kidato cha kwanza tulikuwa wanne. Nakumbuka kipindi hicho watu walikuwa wakitoka kanisani ile ibada ya kwanza wanapitia pale nyumbani kunipa hongera.
Kuna mtu mmoja wa same nae alinihadithia wakati huo anamaliza darasa la saba, kijiji kizima alifaulu mwenyewe kwenda kidato cha kwanza, akasema alikuwa akifungiwa ndani ili asilogwe hadi aliposafiri kwenda shuleni.
Kuna injinia mmoja nae alinisimulia wakati anasoma ILBORU sec, alikuwa anasindikizwa na kijiji kizima kutoka ngarenanyuki hadi usa river halafu wanarudi maana wakati huo magari hayakuwepo pia kwa usalama zaidi(ngarenanyuki to usa river ni zaidi ya km 50). Hiyo ndo tofauti ya elimu ya enzi hizo na sasa.
Kama na wewe una historia yako tupe tafadhali tuone tulikopitia!