SoC01 Kwanini ELIMU ya juu haitoi mchango kikamilifu kukuza uchumi wa nchi?

SoC01 Kwanini ELIMU ya juu haitoi mchango kikamilifu kukuza uchumi wa nchi?

Stories of Change - 2021 Competition

Kilenzi Jr

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
13
Reaction score
245
Pamoja na kuongezeka kukubwa kwa wanafunzi wanaojiunga na elimu
ya juu, vyuo vyingi vikuu vya Kiafrika havitoi wahitimu wengi, na wengi
wao hawana stadi zinazohitajiwa kuinua maendeleo ya kiuchumi ya taifa
katika karne ya 21.

Kwa hiyo kizuizi kimoja kikubwa katika kukuza uchumi ni maamuzi
yanayofanywa na vyombo vinavyotunga sera na taasisi zenye kujenga
uwezo ambazo zinajukumu la maendeleo ya juu ya maliasili watu. Kwa
namna gani juhudi za vyuo hivyo zimekosa mwelekeo? Sababu zifuatazo
zinaweza kuchangia.

Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, uingiaji wa wanafunzi katika
vyuo vikuu uliongezeka kwa haraka zaidi kuliko bajeti iliyotengwa kwa
elimu ya juu. Kwa kweli uingiaji ulikuwa mara tatu katika miaka ya 1991
na 2005, imeongezeka katika miongoni mwa viwango vikubwa kabisa
duniani (asilimia 8.7). lakini wakati huo huo fedha zilizotengwa ambazo
ni wastani wa dola za Kimarekani 6,800 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka
zimeshuka hadi dola za Kimarekani 981 katika mwaka 2005 kwa nchi 33
za Kiafrika zenye kipato kidogo. Kadri idadi ya wanafunzi inavyoongezeka,
fedha zinazopatikana kwa kila mwanafunzi zinapungua. Ubora na uhalisia
wa elimu vyote huathiriwa na hali hiyo. Kukosekana kwa umakini wa jumla
wa kuhakiki ubora, mwitikio wa soko la ajira, ukichanganya maswala ya
14 Kuongeza kasi ya Maendeleo

kiuongozi na ukosefu wa uwajibikaji, inamaanisha kuwa haya maendeleo
hasi yalikuwa hayajawahi kuzungumzwa.

Ongezeko la haraka katika uandikishaji wa wanafunzi umesababisha
ukosefu wa uwiano katika masomo ya gharama nafuu na kumega
(kutumia) fedha zinazotolewa kwa ajili ya utafiti ili kuwasomesha
wanafunzi wengi zaidi. Mwaka wa 2004, ni asilimia 28 tu ya wanafunzi
waliosajiliwa katika fani ya sayansi na teknolojia. Aidha, shughuli za tafiti
zilipungua kwa kuwa Afrika ilitenga asilimia 0.3 ya pato la taifa kama
bajeti ya utafiti na maendeleo, jambo ambalo lilisababisha wataalamu wa
tafiti kushindwa.

Idadi ya wahitimu ni ndogo ukilinganisha na idadi ya
wanafunzi wote wanaosajiliwa na hivyo kupunguza idadi ya wahadhiri
na watafiti wa baadaye wakati ambapo idadi yao ingetakiwa kuongezeka
maradufu. Mwelekeo huu unazidisha ugumu katika utoaji wa maarifa
husika na ujuzi unaotakiwa kwa ajili ya mataifa ya Kiafrika katika kuinua
ushindani na kuendeleza ukuaji.

Taasisi za elimu ya juu zinakosa mamlaka ya kutoa maamuzi na kukubali
kuendana na mabadiliko katika soko la ajira. Mara kwa mara taasisi hizi
zimekuwa zikiandaa upya mitaala na kuanzisha kozi mpya za kusoma bila
uwekezaji wa rasilimali toshelevu kutoka kwa mwajiri katika ufanisi wa
wahitimu katika soko la ajira, hali inayosababisha pengo baina ya ugavi
na mahitaji katika viwango vya juu vya ujuzi. Tofauti baina ya elimu
inayotolewa na kiwango kinachotakiwa katika soko la ajira huchangia kwa
kiasi kikubwa katika ukosefu wa ajira kwa wahitimu, inayozidi asilimia 20
katika nchi 9 kati ya 23 zenye data za soko la ajira lililopo.

Ufadhili duni wa tafiti na kupuuza maendeleo ya kitaalamu kumeibua
mgogoro katika kupata watumishi wanataaluma pale walimu wanapohitajika sana kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi. Pamoja na mishahara duni, mzigo mkubwa wa kufundisha unaosababishwa na ukosefu wa uwiano sahihi wa mwalimu kwa mwanafunzi, ukosefu wa ujuzi wa utawala wa rasilimali watu, na ukosefu wa nafasi za utafiti husababisha watumishi kudumu kazini na hivyo zoezi la kuajili kuendelea kuwa gumu. Mara kwa mara, viwango vya nafasi wazi za kazi kwa watumishi vyuoni ni kati ya asilimia 25 na 50 na mara nyingi ni za sehemu za fani za uhandisi, sayansi, na biashara zimekuwa zikihusishwa na uvumbuzi na ukuaji wa uchumi.

Taasisi za elimu ya juu za Afrika zimekuwa zikizembea katika kusaini
msaada wa “misheni ya tatu"kwa ajili ya uchumi ambao umewaimarisha
wengine katika sehemu nyingine. Uchumi wa kiushindani wa utandawazi
Kuongeza kasi ya Maendeleo
na maarifa umebadilisha mitazamo ya awali juu ya jukumu la taasisi za
elimu ya juu na kufasili “ufundishaji" na “utafiti"kupanuka kwa haraka kwa
maarifa na teknolojia kumepunguza muda wa matumizi ya maarifa na
kupelekea uhitaji wa kuendeleza watumishi na elimu isio kikomo

Kadiri upatikanaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano
unavyoongezeka Kunaufanya upatikanaji wa maarifa kuzagaa, mafunzo
ya ana kwa ana yanazidi kukosa umuhimu mkubwa. Hivi sasa utafiti
unafanywa katika mifumo ya kiuvumbuzi ya kitaifa iliyounganishwa
ambapo dola inakuwa ni muwezeshaji wa kifedha zaidi na sio mtoaji wa
fedha moja kwa moja. Kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoingia
katika vyuo vya elimu ya juu kumetoa msukumo wa mfumo wa utoaji
elimu wenye gharama ndogo, uanzishaji wa vyanzo vya mapato vya taasisi,
na uwajibikaji wa kitaasisi, ikizingatiwa mchango wake katika maendeleo
ya kiuchumi na kijamii. Msukumo wa mwisho kabisa umeibuka na
kuwa kama “dhamiri ya tatu" ambapo mafunzo, utatuzi wa matatizo, na
uhamishaji maarifa katika kusaidia uchumi unakuwa ni tafsiri mpya ya
huduma kwa jamii.

Sekta binafsi ya elimu ya juu inakuwa kwa kasi sana kama suluhisho la
kushuka kwa ubora katika sekta ya umma, na njia muafaka ya kukidhi haja
ya soko la ajira zenye kuhitaji ujuzi. Tangu 1990 vyuo vikuu, na taasisi za
kitaalamu za viwango vya elimu ya juu zinazoendeshwa na watu au taasisi
binafsi vimeanzishwa kwa kasi sana kuliko vile vya umma. Wakati vyuo
vya umma vimeongezeka takribani toka 100 hadi 200 kati ya miaka ya
1990 na 2007, idadi ya taasisi za elimu ya juu za binafsi zimeongezeka
katika kipindi hichohicho toka dazani mbili hadi kufikia takribani 468.
Hata hivyo, mifumo ya uwekezaji isiyokuwa na sheria zenye ufanisi,
utambulisho rasmi, na uhakika wa ubora, na uhaba wa nyenzo kutokana na
mfuko wa fedha za utafiti na uvumbuzi wenye ushindani, vimekwamisha
uwezo wa sekta binafsi kushindana na taasisi za umma na kupanua wajibu
wao katika kukuza ukuaji na ushindani.

Elimu ya juu inatofautiana pia. Mwaka 2004 ilikadiriwa kuwa
kulikuwa na vyuo ambavyo sio vyuo vikuu 1,000 katika nchi zilizo kusini
mwa jangwa la Sahara ikilinganishwa na vyuo vikuu 300. utofauti huu
umepunguzwa kwa kupandisha hadhi vyuo vya kawaida na vyuo vya
ufundi na kuwa vyuo vikuu bila kujaza mapengo yaliyoachwa na vyuo
vilivyopandishwa hadhi. Kwa hali hiyo, kutozingatia kwa serikali katika
16 Kuongeza kasi ya Maendeleo

kuimarisha na kuboresha vyuo vya ufundi katika inatia mashaka hasa
ikizingatiwa kuwa vyuo hivi vitoa mchango mkubwa katika utatuzi wa
matatizo yanayohusiana na uchumi wa taifa.
Kwa muktadha huu, kugharamia elimu ya juu kumekuwa na matatizo
makubwa na changamoto – na ni chanzo cha ubishani katika majukwaa
ya kisiasa. Gharama za umma katika nchi nyingi bado hazipelekwi katika
maeneo yanayohitaji fedha sana, gharama hizo hazisaidii kutoa nyenzo
kwa ajili ya usimamizi mzuri na wenye ubora unaotakiwa, na haina ufanisi
katika kusaidia tafiti. Kadiri taasisi za elimu ya juu zinavyoongezeka na
uingizaji wa idadi ya wanafunzi unavyozidi kupanda, ugharamiaji bado
unaendelea kuwa kikwazo kinachokabiliana na maendeleo ya elimu ya
juu ya nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara hapo baadaye.

Katika miaka ya hivi karibuni, kuongezeka kwa uchangiaji gharama
kwa wanafunzi na wazazi umeongeza chanzo kingine muhimu cha fedha
katika mfumo wa elimu ya juu. Katika bara la Afrika, hali hii imetumia
utaratibu wa programu zinazoenda pamoja, wanafunzi “wanaojigharamia�?,
wanaochangia kiasi fulani cha ada, au baadhi ya vitendea kazi “kwa
kutumia ada�?. Lakini maendeleo ya uchangiaji wa gharama na uzalishaji
wa mapato bado ni mdogo sana ili kuziwezesha taasisi hizi kujiwezesha
kifedha, kupunguza utegemezi wa kifedha toka serikalini, na kupata
rasilimali mara moja moja kwa ajili ya utafiti na uvumbuzi.

Ili kutoka hapa kunahitajika mjadala wa kitaifa juu mabadiliko ya
kifedha ambao unapaswa kwenda zaidi ya elimu ya juu. Kwa hivi sasa,
nchi zilizo kusini mwa jangwa na Sahara zinawekeza wastani wa asilimia
4.5 ya pato la nchi katika elimu kiwango cha juu kulingana na viwango
vya kimataifa. Matokeo yake, mataifa haya yanakaribia mwisho wa uwezo
wao katika kugharamia maendeleo ya sekta ya elimu. Hali kadhalika, nchi
nyingi zinakaribia kufikia kikomo katika kutenga kiasi cha asilimia 20 toka
katika bajeti zao za taifa kwa ajili ya elimu ya juu kiasi kinachodaiwa
kuwa ni sahihi katika nchi zenye kipato kidogo. Katika ngazi ya taasisi,
zimekaribia kufikia kikomo katika uzalishaji wa kipato. Aidha, mapitio
ya tafiti za matumizi ya fedha za umma na za jamii katika sekta ya elimu
zinadhihirisha kuwa katika nchi nyingi, mgawanyo wa rasilimali za umma
kwa misingi ya kiwango cha mapato na michango inayoombwa ya wazazi
una upendeleo kwa kiasi fulani.

Ili kuyashughulikia masuala haya, kuna haja ya kuzingatia zaidi
matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo na kubuni vyanzo vingine ya
Kuongeza kasi ya Maendeleo 17


mapato. Kuongezeka kwa viwango vya ufanisi katika utumiaji wa rasilimali
utahitaji utashi wa kisiasa, ukubalifu wa kisera, na busara. Kuongeza ufanisi
pia kunamaanisha kushughulikia taratibu zilizozoeleka ambazo bado
zipo katika nchi nyingi zinazozungumza Kifaransa zinazo na kawaida ya
kupewa misaada, na kupinga fursa mbalimbali zinazotolewa kwa wasomi
ambazo mara nyingi zinatolewa kwa uficho zinazohusisha fedha nyingi
sana zinazotolewa kama msaada. Mkabala sahihi ni ule ambao ungeweka
kipaumbele kutoa udhamini wa serikali kwa wanafunzi kusoma taaluma
zile zenye umuhimu tu kwa taifa katika siku za usoni.

Jitihada nyingi za kufanya mabadiliko ya elimu ya juu zimefanywa
katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara katika miaka ya hivi
karibuni, lakini matokeo yake bado yameonekana kuwa hafifu. Ili kuokoa
umuhimu wa taasisi za kanda kuchangia vilivyo katika maendeleo ya
kiuchumi na kijamii katika nchi zao na katika kanda kwa ujumla, taasisi
za elimu ya juu zitapaswa kujibadilisha kwa umakini mkubwa zenyewe
ili ziwe taasisi tofauti za kielimu: zilizounganishwa, zilizotofautishwa, na
taasisi zinazokidhi haja zinazolenga katika kuzalisha watu wenye ujuzi
unaohitajika na matumizi ya tafiti zinazolenga katika kutatua matatizo.

Kama haya yatafanikiwa, hii itaonyesha namna “maendeleo ya vyuo
vikuu�? vya Kiafrika yanavyopaswa kufikiwa. Baadhi ya utendaji mzuri
umeanishwa katika kipengele kinachofuata umewasilishwa katika kusaidia
utendajikazi wa serikali.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom