Kwanini eneo la Mashariki ya Kati lililopo baina ya mito ya Euphrates na Nile limekuwa likipiganiwa sana tangu enzi?

Kuna baadhi ya mambo mtoa mada umeyaeleza walau yana mantiki fulani lkn kuna mambo ambayo huna elimu nayo ukayaeleza matokeo yake umetoka nje ya mstari labda wasio fahamu tu ndio utawalisha matango pori.

Kaaba ile ndio nyumba ya kwanza na kale zaidi kwa ajili ya kuabudiwa Mungu, Ilikuwepo hata kabla ya kusimamishwa tena na Ibrahim na mwanae Ismail.

Waislamu wanaenda kuhiji wale wenye uwezo kwa kufuata maelekezi ya Quran katika kutekeleza nguzo ya tano ya uislamu, hawaendi kule sijui kuvuna nguvu za asili laa, wanaenda kumwabudu mola wao tu.

Na hicho kipande sijui cha kimondo unachosema kipo kwenye kona ya kaaba ni uongo mwingine pia, kile kilikuwa ni kipande cha jiwe jeupe kabisa mfano wa maziwa, na kila kilivyokuwa kinashikwa au kuguswa kilibadilika na kuwa cheusi hii inasemwa ni kutokana na dhambi za wanadamu.

Point ya muhimu kuiweka akilini, waislamu hawaendi kule kuvuna nguvu za asili wala nini bali wanakwenda kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu inayowataka kwenda kuhiji katika nyumba ya kwanza na ya kale zaidi ambayo Mungu aliabudiwa
 
Ndg umetisha kwa makala ndefu. Uliposema Bendera ua Israel ina mito miwili nilirudi haraka kwenye bendera sijauona hata mto moja zaidi ya rangi nyeupe na bluu na nyota.

Lakini pia kama issue ni Nyota mbona hata Bendera ya Ethiopia ina nyota, ya Segegal ina nyota, ya camerron in nyota na hata ya Morocco ina nyota. BINAFSI HAPA NIMEPATA HARUFU YA MLETA MADA KUTAKA KUIKWEZA ISREAL KWA SABABU ZA KUITUMWA.
 
Thank you very much sir!!!,,,,nilipoanza kusoma nilijikuta nimetekwa na mtiririko wa maelezo yako,umenifungua sana kifikra!!! mno!!! da!!!,kumbe ndo manake kuhani MUSSA wahubiri wenzake wanamchafua sana kwani jamaa anachanganya imani ya kikristo na hiki ulichokieleza kwa kiasi fulani,amekuwa akisisitiza matumizi ya chumvi ya mawe,mafuta na mambo mengi ya asili akiita ni vifaa vya kiroho,mimi nilikuwa nafikiri jamaa ni mpigaji,lakini unaona watu wakizidi kuongezeka mpaka wenzake wanamuonea wivu jamaa!!!!,,,,ila kasoro yake ndogo ni kusisitiza mambo ya udongo kutoka huko ulikosema hawatupendi na kuacha mambo ya afrika kama kwenda kuhiji misri na kimondo cha mbozi,milima ya oldonyo lengai,mlima meru na mlima wa kilimanjaro,akibahatika kusoma huu uzi atazidi kuwa balaa!!! da!!! stay blessed mwamba !!!!!
 
Hii Post Nimeiona Leo, nimeisoma yote na Nimependezwa nayo sana.
Mwenyezi Mungu akujalie upate Nguvu ya kuendelea kutufundisha Mambo ya Nguvu kama haya.
 
Aisee nimeoga sana kwenye hiyo mito euphrates na nile kuna siku walinikuta euphrates naoga wakawa wanajiuliza hii ni aina gani yq kiboko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…