Kwanini EPL, LaLiga, Serie A na Bundesliga zinaingiza timu 4 moja kwa moja UCL?

Natafuta matibabu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2020
Posts
262
Reaction score
301
Katika nyanja ya kandanda kwa kiwango cha vilabu vya mpira ulimwenguni, bara la Ulaya linaongoza kwa umaarufu likipambwa na ligi 5 bora kutoka mataifa 5 ya Uingereza, Ujerumani, Uitaliano, Uhispania na Ufaransa.

Kutokana na umaarufu huo wa hizo ligi, kukawepo ligi kubwa inayoshindanisha vilabu mbalimbali katika nchi zao barani Ulaya ambao wanaiita Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA Champion League).

Katika kushiriki hiyo ligi (UCL) timu lazima ifanye vizuri katika ligi yake ya nyumbani ndio iweze kufuzu kucheza UCL.

Kati ya ligi 5 bora, ligi 4 tu kutoka Uingereza, Uhisapania, Uitaliano na Ujerumani ndizo zinazoingiza timu 4 moja kwa moja kwenye UCL ambapo hizo timu lazima ziwe top 4 kwenye ligi zao baada ya msimu kumalizika.

Hii imekuwa tofauti na ligi ya Ufaransa ambayo ni bora pia lakini inaingiza timu 2 tu moja kwa moja, timu 1 inaingia kwa kupitia kucheza qualification.

Timu zingine kutoka mataifa mengine lazima zicheze qualification hata kama imebeba ndoo kwenye timu yao ndio iweze kuingia UCL.

Ni kanuni zipi zinazibeba ligi za Uingereza, Ujerumani, Uitaliano na Uhisapania katika kufuzu UCL?
 
Hao waitaliano wameanza juz kuingiza Tim 4. Hapo nyuma walikua wanapeleka 3 tu na hii n kutokana na ligi Yao kutofanya vizur kwenye mashindano ya uefa hapo nyuma.

Ufaransa hawez peleka Tim 4 maana anaboronga Sana kwenye hii michuano hata nusu finally hawafiki mara mbili au hata moja.
 
Kwa hiyo wanaangalia kigezo cha timu kufika mbali kwenye hiyo michuano?

Kama Ligue 1 imekuwa ikiboronga basi iko overrated kuwa miongoni mwa ligi bora
 
Matibabu ulipata lakini?

Nadhani kuna scale ya ubora wa ligi na perfomance ya kwenye UCL..ni kama Simba tulivyowabeba utopolo na kuingiza wanne kwenye mitoano ya CAFCL
Bado, hii naona ishakuwa disability.

Ivi FIFA ndio wanahusika kutambua ubora wa ligi?
 
Kwa hiyo wanaangalia kigezo cha timu kufika mbali kwenye hiyo michuano?

Kama Ligue 1 imekuwa ikiboronga basi iko overrated kuwa miongoni mwa ligi bora
League 1 bado Sana sema Tu inabebwa na
Ukubwa wa nchi Yao Ila Kwa performance
Ya UCL bado hawajafkia kuingiza Tim hata
3

Bado hii league 1 n ya wakulima
 

Wanaboronga kweli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hata wakipewa simba ama yanga hawatoboi.. ..



πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Wanaboronga kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hata wakipewa simba ama yanga hawatoboi.. ..



[emoji1033][emoji1033][emoji1033][emoji91][emoji91]
Daah, mambo yako tofauti kweli, Ufaransa ina mafanikio kitaifa tu ila ngazi ya vilabu ni hoi. Hii ni tofauti kwa Uingereza ambayo ina mafanikio ngazi ya vilabu ila kitaifa ni hoi
 
Daah, mambo yako tofauti kweli, Ufaransa ina mafanikio kitaifa tu ila ngazi ya vilabu ni hoi. Hii ni tofauti kwa Uingereza ambayo ina mafanikio ngazi ya vilabu ila kitaifa ni hoi

Kweli kabisa mkuu Natafuta


πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…