Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,047
CHADEMA wanafahamika kwa mipango madhubuti na makini. Viongozi wa JUU KABISA ndani ya chama wana sifa ya usiri na umoja. Mara nyingi pale wanapotoka hadharani kuiweka mipango yao huonekana kama maamuzi ya ghafla. Lakini huwa na mafanikio makubwa kama yalivyopangwa kutokea na hutokea kama walivyopanga yatokee. Kiufupi hakuna ughafla. Kwa wapinzani wao mafanikio haya hufanya madhara makubwa sana na huwafika ghafla bila kutarajia. Hata ndumila kuwili ndani ya CHADEMA hupigwa na bumbuwazi jinsi mipango hii inavyofikia hatua za kutekelezwa bila wao kushiriki au kufahama uwepo wa michakato yake. Moja ya bao la karne na mfano mzuri wa mikakati hii ni uteuzi wa Dr. Slaa kuwania Uraisi wa mwaka 2010. Jina lilifahamika siku iliyopangwa lifahamike hadharani na kuwaacha waasi wa ndani na wapinzani wa chama midomo wazi! Yaliyofuata ni historia ambayo wewe msomaji pia unaijua.
Kwa anayefanya tafakari vizuri atagundua kuwa wapinzani wa CHADEMA wanafamu fika kwamba hiki chama hakiwezi kumulengesha mapema mgombea wao ajaye au kuruhusu kwa namna yeyote ile akae pahala atakapolengwa na mashambulizi ya mara kwa mara kirahisi. Na yeyote anayeonekana kwa sasa wamemtengeneza tu ili wapinzani wa CHADEMA wapoteze risasi kwa kulenga wrong target. Watajichosha na kupoteza rasilimali zao wakidhani wanamdhohofisha mgombea ajaye kumbe wasijue wanajichosha wao wenyewe! Hii ni sababu ya kwanza. Hizi beti hazikuandikwa kwa kuwalenga "spoon-feeding readers" bali Great Thinkers! The later already knows what I mean. Alright?
Sababu ya pili, ni kanuni ya kawaida kwamba ukitaka kulitawanya kwa urahisi kundi ambalo uimara wake na umoja wake unachangiwa kwa kiasi kikubwa na umahiri wa uongozi wa mchungaji wake, basi piga mchungaji wao na wengine wote watatawanyika! CHADEMA inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa ndani ya chama. Hakuna dalili zilizowazi zinazoonyesha taswira ya safu ya Uongozi ujao. Katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika ndani ya CHADEMA kwenye ngazi yoyote ya juu zinadhihirisha kuwa ni vigumu kupenyeza mamluki au kuwavuluga kwa kutumia mamluki. Hii ni historia njema na inaweza kutumika kutuaminisha kuwa hata zamu hii watavuka salama. Kwa hiyo nafasi pekee kwa wapinzani wa CHADEMA kuleta mtikisiko ni kumuondoa Mchungaji wa kundi kabla ya muda wa ratiba ya kuondoka kwake.
Siamini kama kweli Freeman Mbowe amekuwa Mlengwa No. 1 wa dola ya CCM kwa pigo moja la ghafla na la bahati mbaya. Jipe muda kidogo kutafakari utaona jinsi pigo lilivyokuwa limepangwa kitambo na lilivyotakiwa kuwa moja tu lenye kufikia malengo makubwa kwa mkupuo bila kutikisa sana wala kuhamasisha hasira ya umma. Dondoo hizi zikusaidie:
Wikendi njema!

- Bomu maalumu na la teknolojia mpya kabisa kutoka kiwandani-China likaingia nchini na kulipuliwa ulinganishe na nguvu/jitihada inayowekwa na yombo vya usalama kujua liliingiaje nchini
- Walenga shabaha (snipers) waliotayari kumalizia kazi iwapo bomu halikuleta madhara yaliyopangwa
- Wapiga risasi wenye bunduki za kivita na zenye risasi za kutosha kuhakikisha blusters wanaondoka salama kwenye eneo la tukio
- Mawasiliano kutokuwepo katika eneo la tukio nusu saa kabla na nusu saa baada ya tukio
Wikendi njema!