Elections 2010 Kwanini gazeti la RAI lisifungiwe?

MzeePunch

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2009
Posts
1,412
Reaction score
203
Gazeti la rai katika toleo lake la leo limeendelea kuandika habari zinazomhusisha mgombea wa chadema katika nafasi ya urais (dk slaa) na maaskofu.

Eti sasa wanadai wabunge waislamu wa chadema walimsusia dk slaa kwenye mikutano yake baada ya kuchukua fomu. Habari hii ya kutungwa ni ya hatari sana kwani inaweza kuchochea uhasama wa kidini na kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko.

Gazeti hili linaloendelea kupoteza umaarufu kwa kasi kubwa linamilikiwa na mtu anayesadikiwa kuwa ni raia wa iran aitwaye rostam aziz. Huyu hana uchungu na nchi hii kwani anajua sio nchi yake, hivyo hata yakitokea machafuko atakimbilia kwao.

Ni matumaini yangu kuwa waziri wa habari, afande mkuchika ameliona hili na atachukua hatua za haraka kulifungia gazeti hili haraka. Tunasubiri.
 
Bado ROSTAM na vibaraka wake wanaamini kuwa njia nzuri ya kuwagawa waTz ni kupandikiza mbegu ya udini.

Katika gazeti la ROSTAM la RAI toleo la leo, mbegu iliyorushwa kuwagawa waTZ, inasomeka hivi; "Wabunge WAISLAMU chadema wamgomea Dr. Slaa'!!!...
 
siku tifu linalipuka ni kuwafuata New Habari Corporation na RA na kuwapa kipigo humohumo ofisini mwao
 
Mi ntamsaka Rostam nitamkwida mpaka basi, make anaongoza kwa uchonganishi
 
Gazeti la rai katika toleo lake la leo limeendelea kuandika habari zinazomhusisha mgombea wa chadema katika nafasi ya urais (dk slaa) na maaskofu.

Eti sasa wanadai wabunge waislamu wa chadema walimsusia dk slaa kwenye mikutano yake baada ya kuchukua fomu. Habari hii ya kutungwa ni ya hatari sana kwani inaweza kuchochea uhasama wa kidini na kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko.

Gazeti hili linaloendelea kupoteza umaarufu kwa kasi kubwa linamilikiwa na mtu anayesadikiwa kuwa ni raia wa iran aitwaye rostam aziz. Huyu hana uchungu na nchi hii kwani anajua sio nchi yake, hivyo hata yakitokea machafuko atakimbilia kwao.

Ni matumaini yangu kuwa waziri wa habari, afande mkuchika ameliona hili na atachukua hatua za haraka kulifungia gazeti hili haraka. Tunasubiri.

Kwa mtaji huu Rostam anadhihirisha si raia wa Tanzania na vibaraka wake wa Habari Corporation wamekuwa kama watumwa wake. Nasubiri maoni ya KIRANGA kuhusu hili
 
Mpeni kura
Dr. W.P. Slaa pekee

icon1.gif
Re: Kwanini gazeti la RAI lisifungiwe?

quote_icon.png
Originally Posted by Kiranja Mkuu
Nani mwenye nguvu ya kumfungia ROSTAM AZIZ

Dr. W.P. Slaa pekee​
 
CCM imekosa sera. Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akishakosa sera anakimbilia kwenye ubaguzi; nakubaliana kabia na mzee yule. Utaona mtu anajinadi kwa wapiga nkura akisema tusimchague fulani kwa sababu ni Mpemba, tusimchague fulani kwa vile ana asili ya bara, tusimchague fulani kwa vile ni mnyamwezi. Ubaguzi mwingi wa aina hiyo umekuwa hauna nguvu sana nchini kwetu kutokana na misingi imara iliyoachwa na Nyerere, na vile vile wingi wa makabila yetu kiasi kuwa hatuna vuta nikuvute ya dominance ya kabila moja. Hata hivyo tukishaanza kubaguana kwa mtindo wa dini, kwa vile hiyo itakuwa inahusu block kubwa sana ya watu, na ni jambo ambalo ni explosive sana, basi nechi inaweza kuwaka moto. Sijui kama serikali ina viongozi kweli kwa sababu hili ndilo jambo la kitaifa la kukekemea zaidi kuliko kukemea kuwa waziri akizungumzia ngono asiandikwe.

Mwanzoni mwa utawala wake Kikwete aliwahi kuzungumzia kurudisha misingi ya utaifa iliyojengwa na Nyerere ikiwa ni pamoja kuimarisha mfumo wa elimu isiyojali dini wala kabila kama yeye alivyosomea kwenye shule za wakatoliki akiwa mwislamu. Sasa naona kwa vile karata hiyo ya udini inaweza kumsaidi kisiasa, huenda serikali yake ikakaa kimya kuhusu hilo.
 
Haliwezi kufungiwa lipo upande wa wanamtandao. Mkuchika akilifungia na yeye kazi kwisha! Kutochukua hatua ndiyo ulinzi wake pale alipo. Rweyemamu alifanya kazi nzuri kwa wanamtandao, akabadirishwa idara kwenda ikulu.
 
Gazeti lilishapoteza dira kitambo hata wasomaji nchini hawafiki 1000.!!!!!!!!
 
Hivi Kikwete na ccm yake wanaposema watailinda AMANI ya taifa hili,huwa wanamaanisha kwa mtindo huu?
 
sijaliona bado ila ni kitu kibaya sana ktk nchi hii, akumbuke kua cuf hawakupata mbunge hata mmoja bara baada ya kuanza kuleta za namna iyo, ina maana anaanza kutuambia kua wakristo wote kumbe waanze kuangalia viongozi wa kuwachagua kwa dini zao maana kumbe wa dini ya kiisalma hawatamchagua slaa kwa sababu ni mkristo? je kwa kauli yake ina maana sasa makristo irrespective of chama waanze kuchagua wakristo wenzao si kwa sababu ya uwezo au vigezo vingine ila ni dini tu? maana kwa habari iyo theme kubwa ni suala la dini, maana hajazumgumzia suala lolote la kisiasa bali dini! this is terrible, tunaenda wapi, to be honest i never knew wako desperate kiasi ichi kumzima slaa! wao si wanauhakika na kucheka wao, si wasubiri!
 
Kwa nini waandishi wa habari wasiandamane kumshinikiza waziri? au wakishindwa sisi wanajamii inabidi tulione hili na kufanya maandamano ya amani kufikisha ujumbe, au tunasubiri Israel wawapige wapalestina ndo tuandamane? Hii ishu inahusu taifa letu na ni hatari kwa usalama wa Taifa. Mkuchika akisikia waziri simba kasemwa ndo utasikia anasema anataka maelezo. Tutaendelea kuangalia mpaka lini ili tuchukue hatua? Panapo umoja mabomu na virungu vya polisi havisaidii.
 
CCM imekosa sera. Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akishakosa sera anakimbilia kwenye ubaguzi; nakubaliana kabia na mzee yule. Utaona mtu anajinadi kwa wapiga nkura akisema tusimchague fulani kwa sababu ni Mpemba, tusimchague fulani kwa vile ana asili ya bara, tusimchague fulani kwa vile ni mnyamwezi. Ubaguzi mwingi wa aina hiyo umekuwa hauna nguvu sana nchini kwetu kutokana na misingi imara iliyoachwa na Nyerere, na vile vile wingi wa makabila yetu kiasi kuwa hatuna vuta nikuvute ya dominance ya kabila moja. Hata hivyo tukishaanza kubaguana kwa mtindo wa dini, kwa vile hiyo itakuwa inahusu block kubwa sana ya watu, na ni jambo ambalo ni explosive sana, basi nechi inaweza kuwaka moto. Sijui kama serikali ina viongozi kweli kwa sababu hili ndilo jambo la kitaifa la kukekemea zaidi kuliko kukemea kuwa waziri akizungumzia ngono asiandikwe.

Mwanzoni mwa utawala wake Kikwete aliwahi kuzungumzia kurudisha misingi ya utaifa iliyojengwa na Nyerere ikiwa ni pamoja kuimarisha mfumo wa elimu isiyojali dini wala kabila kama yeye alivyosomea kwenye shule za wakatoliki akiwa mwislamu. Sasa naona kwa vile karata hiyo ya udini inaweza kumsaidi kisiasa, huenda serikali yake ikakaa kimya kuhusu hilo.

Kikwete ametangaza hadharani hivi karibuni kuwa atashughulika na watu wanaoigawa nchi kwa misingi ya kidini. RAI wameandika habari za kugawa nchi. Kikwete ataanza kushughulika na Rostam na Habari Corporation? Au ataacha kwa kuwa ni habari ya kuisambaratisha Tanzania lakini kwa manufaa yake Kikwete? Hata iweje, Dr. Slaa amempita mbali sana Kikwete. Tofauti yao ni kama anga na nchi kavu. Nilishasema kuwa Dr. Slaa ameongoza nchi hii kama Rais kwa mawazo yake mengi mazuri ya kujenga nchi hii katika bunge. Dr. Slaa ndiye pekee aliyeona makosa kwenye sheria ya uchaguzi mbayo Rais Kikwete alisaini kwa mbembwe bila kusoma. Dr. Slaa alichukua uongozi wa urais hata kabla hajawa rais kwa sababu ya ombwe la uongozi lililopo sasa. Akiwa rais kiofisi atafanya mengi zaidi ya kujenga nchi. Mabadiliko ni SASA, kumpeleka Slaa ikulu ni SASA.
 
Sasa hapo anaijenga hiyo CCM yake au anabomoa?? "watanzania sio mabwege kama zamani":
 
sijaliona bado ila ni kitu kibaya sana ktk nchi hii, akumbuke kua cuf hawakupata mbunge hata mmoja bara baada ya kuanza kuleta za namna iyo, ina maana anaanza kutuambia kua wakristo wote kumbe waanze kuangalia viongozi wa kuwachagua kwa dini zao maana kumbe wa dini ya kiisalma hawatamchagua slaa kwa sababu ni mkristo? je kwa kauli yake ina maana sasa makristo irrespective of chama waanze kuchagua wakristo wenzao si kwa sababu ya uwezo au vigezo vingine ila ni dini tu? maana kwa habari iyo theme kubwa ni suala la dini, maana hajazumgumzia suala lolote la kisiasa bali dini! this is terrible, tunaenda wapi, to be honest i never knew wako desperate kiasi ichi kumzima slaa! wao si wanauhakika na kucheka wao, si wasubiri!

Umesema yote, haujabakiza kitu.
 
...Eti sasa wanadai wabunge waislamu wa chadema walimsusia dk slaa kwenye mikutano yake baada ya kuchukua fomu. Habari hii ya kutungwa ni ya hatari sana kwani inaweza kuchochea uhasama wa kidini na kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko...
.

majibu haya hapa: gonga hapa
 
Back
Top Bottom