Mkuu, breki ya "kubinya" na mkono ina disadvantage ukifananisha na ya kukanyaga.
Ma engineer walienda Lab ndio wakaamua iwe hivyo. Usijione Vin Disel uka customize hiyo brake, ikawa ya mkono kama Bajaji, trust me utapata Ajali.
Kwanini?
Brake ya mkono pressure yake ndogo na ata nguvu za anae apply ni ndogo. Ndio maana inatumika kwenye baiskeli na bajaji sana sana ambavyo havibebi mzigo mkubwa na havina speed kali sana.
Guta na Pikipiki zinaweza beba mzigo mkubwa na/au vinaweza kua katika speed kali. Ndio maana wanaweka option ya brake ya mguu kwakua inatoa pressure kubwa.