Kilimo katika nchi hii ni duni sana kutokana na serikali kutothamini wananchi wake hasa wengi wanaoishi vijijini. Sisi ndo wapiga kura lakini kamwe serikali yetu haina habari na maendeleo ya wakulima. Nitoe mifano michache tu kuelezea hii hoja yangu.
- Serikali imekuwa ikitoa miongozo mizuri sana kuhusu kilimo lakini haya yote hayana uendelevu. mfano kilimo cha kufa na kupona, kilimo kwanza. Kongamano zinatayarishwa, posho nyingi zinalipwa kwa ajili ya kuelezea dhana ya miongozo hii lakini mwisho wa siku miongozo hii yote huwekwa kabatini.
- Halmashauri ndo kuna watu na fedha nyingi zinatakiwa zielekezwe huko lakini cha ajabu kule kwenye Halmashauri fedha wanayopelekewa ni wastani wa Tshs 3 millioni kwa miezi mitatu na fedha hii ndo inatakiwa kufanya shughuli zote za maendeleo ya kilimo ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji lakini posho ya Mhe. Waziri wa Kilimo kwa mwezi ni mamillioni.
- Kuna skimu nyingi sana nchi hii kwa ajili ya umwagiliaji yote haya yaligharimu mamilioni ya fedha lakini yote haya yametelekezwa na kubaki mapori. Niiombe Serikali iwaite Mzee Seif wa Kagera Sugar na Mzee Bakressa izungumze nao wapewe maeneo makubwa ya uwekezaji ili waweze kuwekeza katika kilimo na wenyewe pia watakuja kuwasaidia outgrowers ili nchi ipate kujitosheleza kwa chakula, mafuta etc.