Kwanini hatuwathamini 'celebrities' wetu?

Msukuma wa dar

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
1,160
Reaction score
1,195
Kifo cha mwanamasumbwi mwenzangu (Thomas Mashali) kimenisikitisha sana.

Inawezekana vipi kwa mtu mashuhuri kama yule kuuawa kikatili vile, tena kwa kupigwa kama nyoka, kwenye nchi yake, mkoa anaoishi, mitaa jirani?

Hii inajenga picha gani kwa sisi undergrounds? Kwamba Tanzania ili uthaminike basi ushindanie Umiss hata kama ni mwanaume, Ujiunge WCB, 'umdiss' Diamond kwa Mgongo wa TeamKiba au 'umdate' Binti Sepenga ndio jamii itaona mchango wako?

Bado kifo cha Mashali kinachukuliwa kama kifo cha mmoja wa nguvu kazi ya Panya Road, hakipewi uzito kabisa. Ndio Tanzania yetu hii.

Rest In Peace Jembe!
 
Jamii haiangalii umaarufu wa mtu ukifanya ujinga watakuadhibu vikali sana huyo marehemu Mashali watu wake wa karibu wanadai alikuwa na sifa mbaya!

-Nyerere-
 
Haikuwa rahisi kwa raia kumjua,kwani kawaida yake muonekano wake ni wa rasta, sasa hivi karibuni rasta alinyoa haikuwa rahisi kwa raia kumfahamu yeye ni nani.
 
Unataka celebrity kibaka mkabaji athaminiwe??
..hovyooo
 
kwa hiyo wakati jamaa wanambonda alishindwa kujitetea kwa ngumi zake kali?!

wanasemaga wanacheza ngumi kwa ajili ya self defence?
 
kwa hiyo wakati jamaa wanambonda alishindwa kujitetea kwa ngumi zake kali?!

wanasemaga wanacheza ngumi kwa ajili ya self defence?
Walimpigia kelele ya mwizi halafu alikuwa amelewa, nimeangalia 5sport ya EATV shuhuda anasema alimtetea mtu alipwe pesa yake kwa matibabu 20,000.

Ngumi za mtaani hakuna refa, hakuna foul. Walitumia mawe na magongo
 
Walimpigia kelele ya mwizi halafu alikuwa amelewa, nimeangalia 5sport ya EATV shuhuda anasema alimtetea mtu alipwe pesa yake kwa matibabu 20,000.

Ngumi za mtaani hakuna refa, hakuna foul. Walitumia mawe na magongo
na hiyo wanasema ni mitaa yake sasa walishindwaje kumtambua mcheza ngumi Mashuhuri?!
 
Hakua mtaan kwake,jamaa alizidi utembo,anaweza akapanda boda boda toka mbezi haadi mabibo kitaan kwake alaf halipi anaxema yy staff
Samahani wafiwa, ila dah, kama hii ni kweli, jamaa alizidi utembo. Staff kwenye bodaboda yangu, tena mbezi to mabibo. Loh!!! Acha kabisa.
 
Anyway, nafikiri ni wakati muafaka sasa, kila fani lazima iwe na sifa za kuingilia, elimu kuanzia kidato cha sita, ujue kuzungumza, kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza kwa ufasaha.
Lazima uwe na angalau certificate ya marketing, ili ujue namna ya kujibrand.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…