Uchaguzi 2020 Kwanini haukuongeza mishahara kwa miaka mitano mfululizo?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Washauri wa chama tawala na serikali mna majibu ya swali hili? Nimemsikia mgombea wa CCM akisema angeongeza mshahara nauli, unga, mchele, mafuta na sukari vingepanda.

Lakini sukari mwaka 2015 ilikuwa 1,800/= kwa kilogram na sasa hivi ni 2,600/= ni kina nani waliopandishiwa mishahara na kusababisha bei ya sukari kupanda?

Lakini pia,
Nimemsikia akitoa ahadi kwamba akichaguliwa tena kabla ya kumaliza muda wake ataongeza mishahara...je, mbinu gani itatumika kuhakikisha bidhaa zilizosababisha mishahara isiongezeke zisipande bei baada ya kuongeza mshahara kwa wafanyakazi?

Nimesikia suala la kupunguzwa kwa PAYE, hata hilo ni moja ya stahiki za mfanyakazi na hiyo asilimia mbili si lolote wala si chochote kwakuwa serikali ilivunja utaratibu wa kimkataba kwa wafanyakazi waliosomeshwa na HESLB katika kurejesha kutoka 7% mpaka 15% hivyo makato yaliongezeka wakati mshahara umedumaa!

Wengi wangependa kufahamu, Mzee Kikwete katika miaka kumi yote alikuwa akizingatia sana stahiki za wafanyakazi na kila Mei Mosi aliitwa Shemeji na walimu...waliomshauri Rais kutokumuiga JK katika hili walilenga nini?

Wengine wanasema ndege zimenunuliwa, ni jambo jema lakini unaamini barabara za lami zilizojengwa awamu ya nne huku mishahara ikiongezwa na zile zilizojengwa awamu ya tano bila mishahara kuongezwa...awamu ipi ilitumia gharama kubwa katika miundombinu?

La mwisho wengi wanatamani kuona kifungu mkakati katika ilani ya CCM kuhusu kuboresha stahiki za wafanyakazi AU NDO ZOEZI LA KUSIMAMIA NIDHAMU LITAENDELEA?

TUJADILIANE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…