Kwanini hawa Mama N'tile karibu na Kituo cha Polisi wanaongea kwa amri kama Polisi?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Siku moja nikapita maeneo karibu na kituo cha Police. Hiyo sehemu ya kituo kwa karibu kidogo kuna mama ntilie wanauza chai na chakula cha mchana.

Kufika pale yaani si unafahamu zile tabia za Polisi walivyo vituoni kama kujibu kwa zadhau, shurta, kujiskia sana wakiona uwanyenyekee.

Basi nikakuta kwa mama ntilie huyo, sikupenda kwa kweli.

Swali nililomuuliza :"Hivi wewe kuwa karibu na kituo cha Polisi unajiona kama Polisi vile. Je, ukiwa karibu na makaburi utajiona kama nani".
 
Hajui biashara, Kaulita nzuri muhimu ili mteja audio.
 
by "mutual induction" nao wamekuwa pongoz.
 
Ukiona ndege analeta fujo barabarani ujue ana kiota karibu ambacho anaweza kukimbilia na kujificha.
 
Sema wateja na wenyewe huwa wanazidi kukera
 
Kiotuo kipi cha Polisi unachokiongelea?

Halafu kwani umelazimishwa kwenda kula hapo?
 
Mpe vitasa halafu mwambie nenda kaseme halafu chukua kiti kaa au kama kunakaduka pendeni agiza soda takuja kulipa
 
Hii nchi inazidi tu kuwa ngumu siku hadi siku! Hebu tuambie basi hao mama ntilie wanapatikana karibu na kituo gani cha polisi ili tuje na sisi tushuhudie.
 
Alikujibu nini kwenye ilo swali ulilomswalika?
 
itakuwa ulikuwa na masharti mengi kama upo kwa mkeo ndio maana akakujibu nyodo.
Halafu ukute hapo umeagiza wali na mchuzi mtupu bila nyama wa buku.
 
Ukiona kifaranga kunaruka ruka jua mama yake hayuko mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…