Kwanini hawa matajiri wa dunia wanazushiwa na kuchukiwa sana?

Kwanini hawa matajiri wa dunia wanazushiwa na kuchukiwa sana?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
1. Bill Gates
Huyo ametoa sehemu kubwa ya utajiri wake kusaidia sekta muhimu za Afya, Kilimo, Mazingira na Elimu kote duniani. Amechangia pakubwa kumaliza tatizo la polio kwenye mataifa kama Nigeria na India. Amezipa nchi nyingi masikini mabilioni ya pesa kupitia miradi mbalimbali kwa ajili tu ya kuboresha maisha ya wanadamj. Hata hivyo kuna watu wengi duniani kote wanamchukia na kumuona kama shetani!

2. George Soros
Huyu ni billionea Myahudi aliyehamia Marekani akitokea Hungary na survivor wa NAZI. Ametoa dola bilioni nyingi sana kusaidia Demokrasia, vyombo vya habari na elimu kote dunia lakini zaidi sana katika nchi yake ya Marekani. Hata hivyo hapendwi kabisa na wafahidhina wa Magharibi. Republicans wanamtupia lawama kwa mambo yote ya kisiasa wasiyoyapenda. Hata kushitakiwa kwa Trump na makosa yake wamekuwa wakimtupia yeye lawama!

3. Familia ya Rothschild
Familia ya Kiyahudi ambayo ndio watangulizi wa mfumo wa benki kimataifa na watu mahiri sana katika sekta ya fedha na benki duniani ni walengwa wa kila conspiracy theory mbaya inayohusu mifumo ya kifedha duniani, kuna watu wamefikia kusema benki kuu zote duniani zinamilikiwa na familia ya Rothschild!
 
Hili somo refu sana hasa kama unataka amani kwenye maisha yako, usitegemee mtu akujali au akupende, jipende na jijali wewe tu kwanza.

Mie nimeshasaidia watu na nikajuta, ila sikukoma kusaidia baadae nikaona huo ni upuuzi, https://jamii.app/JFUserGuide 'em I live my life.

Mtu ukimsaidia bora hata asilipize, lakini yeye analipiza negative kabisa. Bora usaidiwe upotee tu, ila mtu unamsaidia ndo anakuja kukuzunguka baadae. Imenitokea sana yaan kuliko kumsaidia mtu bora nikashinde bar nipoteze hela kwenye vinywaji vya bei ghali.

Niite mbinafsi, sawa. Lakini binadam ana nature ya ubinafsi tena ukutane na mtu mwenye zimwi la umasikini, hawasaidiki hao wapuuuzi na wana roho mbaya sana.

Kuna mzee mmoja mwaka juzi aliumwa lkn watu wake wa karibu including watoto wake wakamsusa hata kumpeleka hospitali. Mimi nilikua nmepanga nyumba full jirani nae, Yule mzee tulikua tumezoeana sana kila siku asubuhi/jion nikimkuta nje lazima nipaki tusalimiane. Sasa ikakaa kama wiki moja kuelekea mbili mzre haonekan nje.

Siku moja nashangaa nagongewa na mtoto mdg alokua anakaa nae pale kwamba mzee kazidiwa, nikamchukua nikampeleka hospital nikalipia kila kitu hadi akaanza huduma. Yule dogo akanipa mawasiliano ya ndugu zao nikawatafuta keshokutwa yake nikawakabidhi mgonjwa wao nikaendelea na mishe zangu.

Sasa nlipokuja kuona masikini ana upuuzi sana, huyo mzee ikafikia atolewe hospital lkn wakawa hawana hela na hawakunijulisha. Narudi zangu mtaani nimetoka safari nakuta story eti nimemtelekeza mgonjwa hospitali na wananisemea maneno ya kipuuzi na huyo mzee eti anaanza kunilaumu. Nikasema sitokuja kusaidia masikini tena na nikahama ule mtaa.

Kazini napo hvohvo, epuka kusaidia mtu mwenye roho ya kimasikini, ni wapuuzi tu. Na wanaowalalamikia hao ulowaandika hapo juu ni watu wenye roho au mapepo ya kimasikini, na dalili ya mtu wa hivo ni mtu anaependa kulalamikia watu kwa makosa au upuuzi wake mwenyewe.
 
Bill Gates hazushiwi amenukuliwa mara nyingi sana anasema vaccines zitumike Ku control idadi ya watu duniani.....halafu kampuni zina zo deal na vaccines kanunua hisa nyingi.

Hadi mkutano kuhusu maandalizi ya dunia kukumbwa na pandemic amefanya before Corona outbreak....
Alijuaje yote hayo??ana akili sana?
 
Ukishakuwa tajiri, viongozi katika serikali husika itakutumia katika kutimiza malengo yao; kwa hiyo hao wote wanazushiwa kutokana na kutekeleza sera za viongozi wa nchi husika.​
 
1.Chanjo ku control idadi ya watu ni somo pana sana. Katika historia jambo mojawapo linalowafanya binadamu kuzaa watoto wengi ni ili kubakiwa na baadhi yao(wasikose watoto) kunapotokea ajali au mlipuko wa wagonjwa, wajinga hawakumuelewa.

2. Hakuna kampuni inayotengeneza chanjo peke yake, chanjo zote zinatengenezwa na kampuni kubwa za madawa zinazotengeneza dawa nyingine. Kampuni kubwa za madawa huwa zinachapisha financial statements zake kila mwaka, hakuna uthbitisho wa Bill Gates kuwa na share nyingi huko. Pia hata kama angekuwa na share huko tatizo ni nini??

3.TED Talk aliyozungumza kuhusu pandemic haikuwa mkutano kuhusu maandalizi ya dunia kukumbwa na pandemic. Amekuwa akijuhusisha na Polio, Ebola, minyoo n.k anaujua vizuri ulimwengu wa magonjwa na anaweza kufanya predictions zinazohusu magonjwa duniani.

4.Uko serious unapouliza Bill Gates ana akili sana? Kama uko serious jibu ni NDIO.
Bill Gates hazushiwi amenukuliwa mara nyingi sana anasema vaccines zitumike Ku control idadi ya watu duniani.....halafu kampuni zina zo deal na vaccines kanunua hisa nyingi..
Hadi mkutano kuhusu maandalizi ya dunia kukumbwa na pandemic amefanya before Corona outbreak....
Alijuaje yote hayo??ana akili sana??
 
Huo ni uzoefu wako kwa Tanzania, labda na nchi za zamani za Kikomunisti. Ni tofauti sana huko West.
Ukishakuwa tajiri, viongozi katika serikali husika itakutumia katika kutimiza malengo yao; kwa hiyo hao wote wanazushiwa kutokana na kutekeleza sera za viongozi wa nchi husika.​
 
Huo ni uzoefu wako kwa Tanzania, labda na nchi za zamani za Kikomunisti. Ni tofauti sana huko West.
Jaribu kufanyia utafiti kwenye majanga ya kidunia, anza na korona pamoja na mengineyo
 
1. Bill Gates
Huyo ametoa sehemu kubwa ya utajiri wake kusaidia sekta muhimu za Afya, Kilimo, Mazingira na Elimu kote duniani. Amechangia pakubwa kumaliza tatizo la polio kwenye mataifa kama Nigeria na India. Amezipa nchi nyingi masikini mabilioni ya pesa kupitia miradi mbalimbali kwa ajili tu ya kuboresha maisha ya wanadamj. Hata hivyo kuna watu wengi duniani kote wanamchukia na kumuona kama shetani!

2. George Soros,
Huyu ni billionea Myahudi aliyehamia Marekani akitokea Hungary na survivor wa NAZI. Ametoa dola bilioni nyingi sana kusaidia Demokrasia, vyombo vya habari na elimu kote dunia lakini zaidi sana katika nchi yake ya Marekani. Hata hivyo hapendwi kabisa na wafahidhina wa Magharibi. Republicans wanamtupia lawama kwa mambo yote ya kisiasa wasiyoyapenda. Hata kushitakiwa kwa Trump na makosa yake wamekuwa wakimtupia yeye lawama!

3.Familia ya Rothschild.
Familia ya Kiyahudi ambayo ndio watangulizi wa mfumo wa benki kimataifa na watu mahiri sana katika sekta ya fedha na benki duniani ni walengwa wa kila conspiracy theory mbaya inayohusu mifumo ya kifedha duniani, kuna watu wamefikia kusema benki kuu zote duniani zinamilikiwa na familia ya Rothschild!
Kwahiyo wamekutuma uje uwatetee hapa JF au siyo?
 
Utafiti kuhusu nini katika hayo majanga?
Pia mbona majanga yamekuwepo duniani kwa karne nyingi sana na makubwa kuliko ya karne hii kabla hata hawa watu hawajakuwepo duniani?
Jaribu kufanyia utafiti kwenye majanga ya kidunia, anza na korona pamoja na mengineyo
 
Back
Top Bottom