Kwanini hayati Magufuli hakupenda ushindani wa shirika la ndege la Fastjest dhidi ya ATCL?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Hapo zamani nauli za ndege hasa kwa upande wa fast jet zilikuwa nafuu sana hadi mnyinge kama mimi nikapanda kama mara tatu hivi.

Lakini alipoingia hayati magufuli akawafukuza fast jet nchini.

Akanunua ndege za kutisha lakini mpaka anafariki nauli hazishikiki.

Kwanini hayati Magufuli aliiogooa sana fast jet?
 
Kwa sababu alitumia ubabe kuliko akili.
 
Magu hakuwa mfanya biashara au kiufupi ushindani na upinzani hauwezi , ndio maana hata siasa,hoja,kazi zilikuwa zinamshinda. kuna watu walibahatika kusoma naye msingi ,sekondari mpaka chuo ni mbinafsi na mwenye husda sana
 
Fastjet ila basi tu.
 
Magufuli mwenyewe alichagua kugombea ubunge na urais.

Hakulazimishwa kuwa public figure.

Atajadiliwa tu.

Watu wanajadili maisha ya ma farao na wafalme wa Kirumi mpaka leo.

Wanamjadili Caligula na Hitler mpaka leo.

Wanamjadili Pol Pot mpaka leo.

Wanamjadili Idi Amin mpaka leo.

Ili wasirudie maovu yao.

Usitake kutuletea censorship kuziba watu midomo.

Magufuli was a country bumpkin.
 
Kiufupi ni kwamba alitumia nguvu nyingi kuliko akili.
Serikali hii hii ya maccm haiwezi shindana na setka binafsi kwenye maswala ya kibiashara. Ina wafanyakazi wajinga na mbumbumbu mno ambao hata hawajawahi kuuza mchicha Sokon.
 
Labda alitaka ndege zibaki kuwa anasa tu ili msichezee pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…