Kwanini hii hali inawatokea baadhi ya wasanii?

bandeko andeko

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2021
Posts
1,080
Reaction score
2,143
Baadhi ya wasanii imeonekana kuwa wana maisha mazuri sana ila tatizo linaanza wakiugua miongoni mwao wameshindwa kumudu gharama za matibabu kupelekea kutembeza bakuli ili wapate misaada ya kugharamia matibabu yao.

Nimejiuliza hili baada ya kuiona habari ya msanii mr. Ibu wa Nigeria.

 
Sijamjua huyo msanii navyofahamu wasanii wengi huwa wanaumwa na wanajitibu wenyew unapotokea ugojwa mkubwa ndipo inapolazimu kuomba michango

Kuchanga michango mimi huwa naona ni kama ni utamaduni wetu waafrika haijalishi hata kama mtu ana pesa.

Hata wabunge bila kugharamiwa na serikali wangerudi mtaani kuomba mchango.
 
Nakazia
 
Sijamjua huyo msanii navyofahamu wasanii wengi huwa wanaumwa na wanajitibu wenyew unapotokea ugojwa mkubwa ndipo inapolazimu kuomba...
kuchangia si jambo baya ila ukilinganisha ni vipato vyao ni sawa wao kuhitaji michango ya kugharamia matibabu?
 
DeepPond samahani naomba nikutolee mfano hypothetically lile life lako na michepuko halafu ikitokea umeugua ushindwe kujigharamia, ni sahihi kwa wewe kuchangiwa?
 
Kuna magonjwa mengine mkuu yanatafuna pesa zilizopo ndani, bank mpaka kuuza mali ulizonazo na Bado huponi ndipo hapo unakumbuka Kuna jamii ulikuwa unaiburudisha Kwa kazi zako hvyo huna budi kuirudia nakuomba ikusaidiee japo c wt watakusaidia ila wachache wataguswa na kuchangia na wengine wasioweza kuguchangia watakuombeaa piaa..

Mf.profesa jay.

Ommy d
 
Gharamaa za matibabu huwa ni kubwa snaa Just imagine mr Ibu ilikuwa zaidi ya naira Milion 10 kwa Wiki na amelazwa zaidi ya miezi mitano...
So hata ukiwa Waziri lazima utashindwa gharama..

Kama ulimsikiliza Vizuri ProffJ Pia alisema alikuwa akichomwa sindano moja kwa Tsh 10 na gharama za mayibabu ni kubwa sana..
Just imagine amekaa ICU for 127 Days na akifanyiwa Dyalisis unajua ghrama zake.?
 
Mr ibu,my best comedian,
 
DeepPond samahani naomba nikutolee mfano hypothetically lile life lako na michepuko halafu ikitokea umeugua ushindwe kujigharamia, ni sahihi kwa wewe kuchangiwa?
Kuomba kuchangiwa haimaanishi mtu hawezi kujimudu kimatibabu,

Ni utamaduni TU waafrika tumezoea kuishi kijamaa zaidi.

Ni Kama ilivyo kula msibani,
sio kwamba tunakua na njaa Sana ,
Bali ni sapoti tu kwa wafiwa

Au kuchangiana harusi, mi ukinialika nije kwako kula na kunywa bure,kiukweli siji.

Ila ukitoa kadi,nikachangia apo NTAKUJA.
 
sawa ndugu.
 
Surgery mara 7 jamaa kajigharamia hio ya 8 ndio imemshinda Pesa zimekata kwenye hizo surgery 7 za mwanzo
Daaaah unaona hapo mkuu..
Hawa watu wanapitia magumu sana aiseee..
Ukishakua maarufu tuu kuna mambo yanatokea adi unashangaa
 
Wanaishi expensive life lakini ukiwashauri wanatukana mpaka yakiwafika ndio wanarudi kwa jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…