Kwanini historia ya dunia inaonyesha watu wa visiwani huwa wana uwezo mkubwa wa utawala kuliko watu wa bara?

Kwanini historia ya dunia inaonyesha watu wa visiwani huwa wana uwezo mkubwa wa utawala kuliko watu wa bara?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
mfano

1: JAPAN Ilikuwa na uwezo mkubwa na ikatawala kuanzia China, Korea, na viunga vyote vya maeneo jirani na nchi hizo. Hakuna aliyefurukuta.

2: Watu wa Visiwa vya uingereza, enzi zao walitawala karibu dunia nzima. Hadi kukawa na msemo, Uingereza jua halizami, wakimaanisha likizama huku hata linakoibukia ni kwa waingereza.

3: Watu wa kakisiwa kadogo ka Taiwan, wamekuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia na ushawishi mkubwa kiasi China na ukubwa wake hawawezi tena kuilazimisha ijiunge nao.

4: Shelisheli ni moja ya sehemu yenye maendeleo makubwa sana afrika wakati ni visiwa vidogo tu.

5: Moja ya miujiza mikubwa ya kihistoria ya kiuchumi ilifanyika katika visiwa vya Singapole. Brilliant Diktator mwenye asili ya china Lee Kuan Yew alifanya mambo makubwa hadi china ikatuma watu kujifunza. Hadi leo ni moja ya nchi tajiri yenye watu wenye iq kubwa wakati huko nyuma tuliwahi kukaribiana nayo kimaisha.

Chanzo ni nini?
 
Si unaona wa Bara wanavyotokwa na mapovu Kwa Sasa Kwa vile Wana uwezo mdogo sana wa kujitambua.
 
Kwanza unatakiwa kujua Taiwan haina uwezo wowote kuizidi china, ila imetaka kuwa huru kama zilivyokuwa Nchi nyingine zilizotaka kujitenga..

Pili umeongelea visiwa vya ushelisheli (Seychelles), hivi visiwa hata kwenye Top 10 ya nchi zenye uchumi mkubwa Africa Haimo.

Pia umezungumzia Uingereza ambayo kwa asilimia kubwa mtaji wake wa uchumi pia imeutoa Africa.

Lakini miongoni mwao hayo yote Dunia ina nchi zaidi ya 150, lakini kwenye orodha yako umetaka visiwa vitano ambavyo ni sawa na 3% ya nchi zote Duniani, vipi kuhusu 97% zilizobaki....

Kuwa nchi ya kisiwa haimaanishi ndio utafanikiwa, mafanikio utokana na rasilimali ulizonazo na jinsi unavyozitumia kuzalisha uchumi.

Umetaja visiwa vyenye mafanikio, lakini pia kina visiwa ambavyo ni nchi na vina umaskini wa kutupwa Duniani. Hivi ni kati ya visiwa maskini Duniani; Kiribati, Solomon Islands, Papua New Guinea, Vanuatu, Micronesia, Marshall Islands, Tuvalu, Samoa, Tonga, Nauru.

Hitimisho: Uchumi uchangiwa na Raslimali za nchi, idadi kubwa ya watu pia inaweza kupelekea umaskini endapo pato la taifa halitokidhi... Nigeria ni nchi namba moja yenye uchumi mkubwa Africa, lakini Raia wake ni maskini, ukilinganisha na Nchi kama Morocco ambayo inazidiwa na Nigeria.
 
mfano

1: JAPAN Ilikuwa na uwezo mkubwa na ikatawala kuanzia China, Korea, na viunga vyote vya maeneo jirani na nchi hizo. Hakuna aliyefurukuta.

2: Watu wa Visiwa vya uingereza, enzi zao walitawala karibu dunia nzima. Hadi kukawa na msemo, Uingereza jua halizami, wakimaanisha likizama huku hata linakoibukia ni kwa waingereza.

3: Watu wa kakisiwa kadogo ka Taiwan, wamekuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia na ushawishi mkubwa kiasi China na ukubwa wake hawawezi tena kuilazimisha ijiunge nao.

4: Shelisheli ni moja ya sehemu yenye maendeleo makubwa sana afrika wakati ni visiwa vidogo tu.

5: Moja ya miujiza mikubwa ya kihistoria ya kiuchumi ilifanyika katika visiwa vya Singapole. Brilliant Diktator mwenye asili ya china Lee Kuan Yew alifanya mambo makubwa hadi china ikatuma watu kujifunza. Hadi leo ni moja ya nchi tajiri yenye watu wenye iq kubwa wakati huko nyuma tuliwahi kukaribiana nayo kimaisha.

Chanzo ni nini?
Chanzo ni nini?

Chanzo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom