BASIASI
JF-Expert Member
- Sep 20, 2010
- 9,732
- 5,006
Wiki mbili zilizopita nimefanikiwa kulala hotel nne tofauti. Lengo si kuwasema lengo ni watu walipe kodi nchi iendelee. Katika hotel zote hakuna hata moja inayotoa risiti za TRA na unalipa 85000+.
Nikianza na hii ya five star hapo Darajani nyingine kule Nungwi. Nyingine iko pale Kilimani opposite na faya ya Zanzibar. Tena wanakujibu makavu hatuna risiti za TRA, nawaza tu hivi nayo si Tanzania ama. Mbona hivi eti sisi ni nani bara tulipe kodi wao wasilipe, nashauri serikali ya Zanzibar muwe makini na hili mtapata hasara sana.
Hizi mnazoona fly-over bara hazijengwi na maji ni kodi za wananchi, ni vyema mkawa serious kukusanya kodi. Nimepita pale bandarini kuna baadhi ya ofisi wanapokea mpaka laki mbili na hawatoi risiti za TRA. Hii ni hatari sana msiturudishe tullipotoka.
Kampuni hiyo hiyo ya usafiri ukitokea Bara ukilipa unapewa na risiti za TRA, why?