Wadau, kwa namna waliowengi tulivyoshuhudia namna Jaji Warioba alivyolihutubia Bunge Maalum la Katiba jana 18 Machi 2014 kwa kutamka kwa ufasaha bila woga, unafiki wala upendeleo historia ya Muungano wetu, tulipotoka, tulikopitia, tulipo na tunapopaswa kuelekea, ni dhahiri kwamba Jaji Warioba anastahili kuingi kwenye Vitabu vya Historia ya nchi kwa kuweka sahihi historia ya nchi yetu. Jaji Warioba amesema yasiyoweza kuzungumzwa na baadhi ya viongozi wengi walioko madarakani. Ametetea Utaifa, akaweka nyuma maslahi ya chama chake CCM, akatetea watanzania, watanganyika na wazanzibari kwa pamoja ili kuwa na Taifa moja ambao watu wanaishi kwa amani ya kisiasa na amani ya kiuchumi na kijamii. Hii ndiyo kwanini hotuba hii inastahili kuingia kwenye kumbukumbu na historia ya nchi hii!