Kama ni ushamba wacha niwe mshamba! Na kama ndo upendo wacha nionekane sina! Kama yeye ana upendo mbona hakumwambia tangu mwanzo?! Kama unampenda mwenzako utamficha kuhusu mambo hata yasiyofichika?! Mwambie huyo bidada akubaliane na ukweli aendelee na maisha yake, kama huyo N ana mtazamo kama wangu hatarudi ng'o! Ninajichunga sana, sijawahi kumpa mtoto wa mtu mimba. Na msimamo wangu ni kuwa hata iweje sitaoa mdada mwenye mtoto, ndivyo nilivyochagua kwa utashi wangu. Hapa nilipo kuna wadada wa aina mbili 'ninaowaogopa' mke wa mtu na mdada aliyekwishazaa! Nikikutana na mdada wa hivyo hata kama nimemzimikia vipi akitaja mume au mtoto, kwa heshima kabisa atabaki kuwa best, mambo ya mapenzi asahau. Jamani watu tupo wa aina nyingi na kila mtu ana vigezo alivyojiwekea. Kuna mtu huko juu kauliza kama kuwa na mtoto ni dhambi! Jibu liko wazi, neno dhambi amelitoa wapi?! Kitendo kinachosababisha kupata mtoto kabla/nje ya ndoa kinaitwa dhambi. Ikiwa nina dhambi hainipi haki ya kuzihalalisha kuwa siyo dhambi, hata dhambi iliyozoeleka bado ni dhambi!