Mwamba 3
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 253
- 285
Tunashukuru Rais wetu Mtukufu ameridhia hitaji la katiba mpya .
Na itapendezwa zaidi Rais atakapong'olewa baadhi ya meno kuepusha utawala wa kibabe
Binafsi baadhi ya mambo ambayo natamani yawepo kwenye Katiba ni Rais kuchunguzwa na kushtakiwa baada ya Urais wake endapo kulikuwa na ubadhilifu wa mali za umma , Kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani endapo kama kulikuwa na dosari zozote za usimamizi , Kuhusu Tume huru ningependekeza ingekuwa inaundwa na Bunge ili iwajibike chini ya bunge ( bahati mbaya bunge lenyewe halina upinzani ), Serikali kutoingilia mihimili mingine hasa mahakama .n.k
Lakini nirudi kwenye mada tajwa hapo juu. Najua mchakato wa kuandaa katiba mpya una mambo mengi na gharama nyingi na huenda figisufigisu nyingi . Ili kuepusha hayo kwa nini isingechukuliwa Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba kutokana na sababu zifuatazo
Kwanza ; Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba ilipatikana kipindi ambacho walau kulikuwa na vugu vugu la upinzani hivyo ilibeba mambo mazuri tofauti na hali iliyopo sasa
Pili ; Kwa asilimia kubwa ya Watanzania walipendezewa na ile Rasimu , hivyo hakuna haja mambo ya kuunda tume jingine ni kupoteza hela tu . Maana mambo mazuri yalikuwemo mule .
Tatu ; Inasemekana mchakato wa kudai katiba mpya haujaanza leo wala jana . Ulikuwepo na tume zikaundwa likini wenye nchi hawakosi kuleta vikwazo mambo yanaishia tu kwenye kupata rasimu basi. Mambo ili yasiwe hivyo na kama tuna dhamira ya dhati ya kuipatia Tanzania katiba mpya basi tuitumie ile Rasimu ya Warioba
Nne; Watanzania tulikuwa na imani sana na rasimu ya Jaji walioba kwa sababu Ilibeba matakwa ya kweli ya Watanzania. Huyu Mkandala ni tofauti na Warioba maana Mkandala hana kabisa msukumo wa ndani wa kuwapatia Watanzania katiba ya kweli
Je, ni nini tunakitafuta , kwa nini tusiitumie ile Rasimu ya katiba ya Jaji Warioba , ina dosari gani ?
Karibuni ili tufumbuane macho maana wengine huenda hatuna jicho la tatu