kwanini jamii zetu hatuna umoja?

kwanini jamii zetu hatuna umoja?

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,476
Reaction score
11,659
habari wana jf,
kuna kitu kinanikwaza na kunipa shauku ya kujua.
nimezaliwa kwenye jamii ya kitanzania..nimekulia mji wa dar na elimu yangu nimeipata hapahapa.katika malezi yangu haya nimeshuhudia mengi kwa watoto na hata vijana wa rika langu wanavyosuffer na kusota majumbani na kuishia njiani elimu zao kisa mzazi au mlezi kukpsa ada ya kumsomesha.
kuna makundi amuai kwenyw jamii..kuna vibati..sijui vicoba na ndugu wengi ukoo mmoja lakini mbona hawa walezi hawana umoja katika elimu za watoto wao kwa manufaa yao ya baadaye?yani maisha wanayoishi ni changu ni changu..chako ni chako!
utaskia binti wa fulani hapa mtaani babake anafanya biashara lakini serikali imeiua..kwahyo shule ndo bas sababu wazaz wake hawana uwezo wa kupata laki tano arudi shule..mtaona binti anavosugua gaga mtaani.
lakini hebu tangaza kesho binti anaolewa watakuja kwa makundi na wakisisitiza umoja kufanikisha send off hadi kamati wanaunda na vikao hawakosi..na baada ya mda itapatikana si chini ya million tano yote kwa ajili ya ule usiku wa kula na kusaza
MLISHINDWA VIPI KUKUTANA KAMA NDUGU NA MARAFIKI KAMA HIVO KWA MANUFAA YA BINT ALIPOFUKUZWA SHULE??
nawaomba iwe ndugu wa ukoo ama marafiki..kuweni na upendo..mwenzio akikwama mshike..ndo mana tukapewa amri kuu mpende jirani yako kama unavojipenda.
mfano mtoto anadaiwa laki saba arudi shule..mkapatikana watu 100 wenye vipato kwenye ukoo wenu..kila mmoja akatoa 7000.atakosa shule?
imagine elfu saba tu unaombwa kwa ajili ya ada unashindwa?
tuache umimi jamani!
ingekuwa hivi usingekuta vilaza wa kujaa mtaani..
hata panya road wameamua kuwa hivi sababu ya umaskini.
inawezekana mkiamua!
 
1st to reply,,,,umeongea jambo pana sana ila ukitaka kujua roho za watanzania tunamwacha mgonjwa anaehitaji matibabi ya milion moja lakin akifa tunachanga badget ya milion kumi kufanya mazishi,,, tuna matatizo na malez nadhan,so sisi tumerithi tu,tunapoteza ving na muda mwngi kwa visivyo na msingi ila yale ya maana tuna ya ahirisha
 
1st to reply,,,,umeongea jambo pana sana ila ukitaka kujua roho za watanzania tunamwacha mgonjwa anaehitaji matibabi ya milion moja lakin akifa tunachanga badget ya milion kumi kufanya mazishi,,, tuna matatizo na malez nadhan,so sisi tumerithi tu,tunapoteza ving na muda mwngi kwa visivyo na msingi ila yale ya maana tuna ya ahirisha
upo sawa kabisa..hii tabia itatowekaje?
 
It's all about Priorities, Preferences and choices..

Wanadamu wanapenda vitu vya kukonga moyo kwa muda mchache tu huku vya maendeleo wanasuasua...


UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU
 
Back
Top Bottom