Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Kiini cha kesi ya Raila na CORD dhidi ya tamko la IEBC kuwa Uhuru Muigai Kenyatta alishinda Uraisi wa Kenya ni kuwa zilikuweko mbinu chafu za kuhakikisha mitambo ya IEBC haifanyi kazi hivyo hesabu za kura hazikufanywa na mitambo ila watu ambao walitumia mwanya huo kutengua ushindi wa Raila.
Ili kuthibitisha dhana hiyo Raila & CORD waliomba ifanyike forensic auditing ya kuhakiki kila kilichofanyika IEBC. Supreme Court ya Kenya jana ilikataa kufanyika kwa zoezi hilo kwa sababu zifuatazo:-
1) Maombi hayo hayatekelezeki kwa kuwa yanahitaji muda mwingi zaidi ya siku 14 za kikatiba za kuusikiliza mgogoro tajwa.
2) CORD walikuwa na nafasi ya siku 16 tangia IEBC imtamke Uhuru kuwa kashinda uraisi sasa walikuwa wapi siku zote hizo kudai haki hizo mahakama Kuu ambako ndiyo wenye haki ya kiawali ya kusikiliza madai ya namna hiyo.
3) Maombi yao mahakamani hapo hayakuzingatia taratibu za kiufundi za uendeshaji wa suala hilo katika SUPREME COURT.
4) Maombi yao yaliwahusisha makandarasi wa IEBC ambao hawakuwashitaki na hivyo sheria hairuhusu kuwashurutisha watu au makampuni ambayo siyo sehemu ya mgogoro kutekeleza amri za mahakama bila kushirikishwa watajwa hao katika suala zima lililoko mahakamani.
5) Maombi hayo hayakuonyesha ni jinsi ipi mahakama itazitumia taarifa hizo na hivyo kunufaisha uendeshaji wa kesi husika. CORD walishindwa kuonyesha jinsi itakavyotumia manufaa ya maombi hayo na hivyo kuonekana walikuwa wanafanya kitu kinachoitwa ni utafiti au "fishing expedition." Mahakama siyo mahali pa kufanyia utafiti ila kuamua mashauri tu kulingana na ushahidi ambao upo mahakamani hapo.
6) Fomu namba 34 na 36 zilitosha kulitathmini zoezi zima la uchaguzi kama ulifanyika kwa haki na tayari SUPREME COURT ilikuwa imetoa amri uhakiki wa zoezi zima ufanyike kwenye FOMU namba 34 na 36 ikiwa ni pamoja na vituo 22 vya kupigia kura ujumlishwaji kura urudiwe. Hivyo kufanya maombi haya kuwa yamepitwa na wakati.
7) Ratiba ya kulisikiliza na kuliamua shauri lenyewe lazima ufanyike ndani ya siku 14 kulingana na katiba ya Kenya hivyo hapakuwepo muda wa kulifanya zoezi la "forensic auditing" tajwa ndani ya muda huo.
8) CORD walishindwa kuonyesha ni nani aifanye kazi hiyo ya "forensic auditing" na kwa muda gani na atakuwa hana upendeleo kwa upande wowote na hivyo matokeo ya uchunguzi wake kuweza kupewa na nguvu ya sheria na mahakama ya kileleni.
9) CORD walishindwa kuonyesha mapungufu ya Fomu na. 34-36 na hivyo kuhitajika uhakiki wa ziada kupitia "forensic auditing" tajwa.
10) Siku ya Jumatano na Alhamisi zilipangwa kusikilizwa kesi kama maombi ya CORD yangelisikilizwa basi ingebidi kesi ianze upya kabisa hata hivyo muda wa kufanya hivyo haupo kulingana na katiba.
Baada ya haya maelekezo ni wazi kuwa bila ya hiyo forensic auditing FOMU 34, 35 na 36 hazitakuwa na msaada kwa CORD maana kama zingelikuwa na msaada wasingewekeza sana nguvu zao kwenye forensic auditing ambayo hata matunda yake hawayafahamu yangelikuwaje.
Hivyo kauli za Raila kuwa alimshinda Uhuru kwa zaidi ya kura 1.3m alizitoa mfukoni mwake! Kama Raila angelikuwa ni mkweli basi angelianza kuutumia ushahidi tajwa leo na kesho na kuishinda kesi badala ya kuendelea kudai apewe ushahidi mpya ili athibitishe madai yake ambayo sasa imethibitika ni utapeli mtupu amekuwa akiufanya.Tegemea Raila kwenda Kibera Jumapili na kuanza kujenga mazingira ya rabsha ya kupinga uamuzi wa mwisho wa kupinga matokeo ya Uraisi wa kenya.