Kwanini Jezi za Kilimanjaro Stars hazikuwa na jina la nchi?

Kwanini Jezi za Kilimanjaro Stars hazikuwa na jina la nchi?

Kimbojo

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2009
Posts
387
Reaction score
54
Mashindano yanayoendelea ya cecafa timu zote kwenye jezi zao zimeandikwa majina ya nchi. Amavumbi (Rwanda), Harambe stars (Kenya), The Flames (Malawi), Intamba mrugamba (Burundi), Zanzibar heros (Zanzibar), zimbabwe woriors (Zimbabwe), The Cranes (Uganda), Ocean Boys (somalia), Djibout(Djibout) haya majina ya kwenye mabano yaliandikwa kwenye jezi za nchi husika, Je The Kilimanjaro kwanini jezi hazikuandikwa jina la nchi? au hizo ndizo kero za muungano? mbona Zanzibar waliandika Zanzibar? sisi tulipaswa tuandike Tanzainai bara? lakini TZ bara haiwekani mbona Zanzibar hawakuandika TZ visiwani? tulipaswa tuandike Tanganyika ambayo ni jina la nchi yetu tunajivunia nchi gani kwanye mashindano haya? TFF waliwaza haya mambo? au waligonga na kero za muungano?
 
ohhhh yeah sasa nimepata picha kwanini Kilimanjaro Stars walikuwa wanazomewa na mashabiki, ni kwasababu Timu ikuwa haijulikani inawakilisha nchi gani Nakumbuka nahodha Juma Kaseja aliwahi kulalama kuwa uhenda mashabiki sio watanzania, nakubaliana nae kwa msingi wa mashindano haya mashabiki wengi walikuwa ni wa- Tanganyika. Walitumia vyema haki yao ya kudai Timu yao ya Tangayika. TFF kazi ni kwako Amka na chukua maamuzi magumu iliuje uheshimike mbele ya safari.
 
Naona wana-JF wamechoshwa kabisa na 'kili star' sijui hata huko uwanjani kuna washabiki wangapi, yani sijaona hii michuano ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Tanganyika na sudan kufunguliwa thread maalumu,
 
Naona wana-JF wamechoshwa kabisa na 'kili star' sijui hata huko uwanjani kuna washabiki wangapi, yani sijaona hii michuano ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Tanganyika na sudan kufunguliwa thread maalumu,

hivi hilo game limeshachezwa?..duh,,,,,,jamani wadau, fainali itaonyeshwa na TBC au ndio uhuru wa miaka 50 tu kwa kwenda mbele
 
Tumefungwa goli moja na mechi imeisha, kuhusu majina ya nchi sio Kili stars peke yake hata Falcon haikuwa na jina la nchi yake nadhan ni uamuzi tu.
 
Back
Top Bottom