Uchaguzi 2020 Kwanini kampeni za mwaka huu zimepooza sana?

Uchaguzi 2020 Kwanini kampeni za mwaka huu zimepooza sana?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Pamoja na kufunguliwa kwa dirisha la kampeni, lakini dalili zote zinaonyesha Wananchi hawana hamu na kampeni, wanaofuatilia kampeni ni wachache ukilinganisha na mwaka 2015.

Nimejaribu kuangalia ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai. CHADEMA wao wanategemea watu wasio na kazi maalumu na ndiyo kinachowafanya waanze kampeni muda wa saa 11 ambapo watu wanatoka sehemu za kazi.

CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni? Anyway, mwaka huu watu wengi wanafatilia siasa wakiwa wanapambana na maisha yao.

NB: WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE ILA HAWADHANI KAMA ITAWEZEKANA
 
Magufuli ameharibu siasa za Tanzania yaani watu wamechoka siasa
Zamani kulikuwa na ruhwa kuanzia uteuzi mpaka miwsho.wa kampeni kwa hiyo mambo yalikuwa moto.
Pia kipindi hicho watu walikuwa na pesa zinazokosa kazi kwa hiyo kuwapa wanasiasa haikuwa shida ila sasa mambo ni ngumu kila mtu anajua thamani ya pesa.

Hapo nyuma nakumbuka nilinunua gari yangu ambayo town hii nilikuwa peke yangu,
Sasa ukiingia kwenye gari tu utashangaa mtu anagonga kioo ukishusha tu ana anza kutoa sifa anazungumza kisha anaomba na pesa, unachomoa unampa, ila kwa sasa hata wakija na sifa zao nawaangalia tu,
Mpaka wameamua kuomba hata mia tano sitoi.
 
Pamoja na kufunguliwa kwa dirisha la kampeni, lakini dalili zote zinaonyesha wananchi hawana hamu na kampeni, wanaofuatilia kampeni ni wachache ukilinganisha na mwaka 2015.

Nimejaribu kuangalia ufunguzi wa kampeni za CCM, wao walinufaika zaidi na wanachama wao hai. CHADEMA wao wanategemea watu wasio na kazi maalumu na ndiyo kinachowafanya waanze kampeni muda wa saa 11 ambapo watu wanatoka sehemu za kazi.

CCM ndo usiseme, wako slow kweli kweli au kwakuwa wana akiba kibindoni? Anyway, mwaka huu watu wengi wanafatilia siasa wakiwa wanapambana na maisha yao.

NB: WATU WENGI WANASUBIRI UTOKEE MUUJIZA LISsU ASHINDE ILA HAWADHANI KAMA ITAWEZEKANA
Sababu
1. Vyama vilifungiwa muda mrefu havikujitanua kupata wanachama
2, ccm hawana jipya zaidi ya ndege na reli
3. Vyombo vya habari vimefungiwa zisitoe habari za kampeni ya uchaguzi kwa upinzani
4. uoga wa maambukizi ya Corona
5 vitisho vya polisi kwa vyama
6.nec imevuruga kwa kuwakataa wagombea
7.ukata wananchi wako hoi kiuchumi
 
Kanuni yetu ni hii "Hapa kazi tu"
Hivyo, ushindi kwetu CCM ni asubuhi mapema jioni tunakunja mkeka huku tukitoa chenji kwa vibaraka.

Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Mafuguli
 
Kwa sababu CCM baba lao na hana mpizani ndio maana yake, hawa machepe watulie tu.
 
Rushwa ya kununua Madiwani na wabunge wa upinzani ili wakaunge juhudi zimetuvunja nguvu.
Michezo michafu ya kisiasa imetugawa na kutuondolea uhuru, umoja na furaha
 
Mkuu umeniwahi sana kutupia huu Uzi. Ila Mimi ninavyoona, umesababishwa na upinzani kuwa disorganized, maan kila mmoja anapambana kivyake, na insu ya Amsterdam
 
Back
Top Bottom