Kwanini katiba bora ni muhimu na inaifanya taifa kuwa na maendeleo

Kwanini katiba bora ni muhimu na inaifanya taifa kuwa na maendeleo

Herr muller

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2018
Posts
1,017
Reaction score
1,210
Natarajia kila mtu na kitu mko swali kabisa, licha ya hii mambo ya new pension law ambayo si kutugusa tu ila imetuumiza ajabu,Leo nataka niongee tu machache kuhusu umuhimu wa taifa kuwa na katiba bora, Na sio tu nitaongea tu kwa kufikiria, LA nitaongea kaa mtu ambae ameishi mataifa ile iko na katiba sio tu bora lakini mataifa ambao inajulikana kama FIRST WORLD COUNTRIES, taifa letu la tanzania ni taifa linajulikana kaa THIRD WORLD COUNTRY, na kwa jina lingine, (lcd) or least developed countries, yaani mataifa yale masikini zaidi duniani.

Sasa nafikiri mtu amenielewa.Ukiangali hayo mataifa ya first world, mataifa kaa marekani, canada, germany, norway, britian, tofauti yake na hii taifa letu la tz sio ati sababu wao wengi ni wazungu, sio ati wao wana utaalamu wa hali ya juu, sio ati wako na viwada vya kisasa, sio ati wako na makampuni makubwa duniani jibu ni LA, sababu ni mbili , moja katiba yao, na pili viongozi wao,hii vitu mbili katiba na viongozi bora ndivyo zinaleta maendeleo, kwa lugha ya english, DEVELOPMENT IS JUST A BY PRODUCT OF GOOD LEARDERSHIP WHICH IS BROUGHT ABAUT BY GOOD CONSTITUTION,,katiba bora huleta viongozi bora, viongozi bora hutengeneza good policies ambazo zinafanya taifa kusonga mbele, ukiangalia taifa letu la tz sio ati ni masikini la, sio ati hatuna utajiri, la, ile kitu tumekosa ni uongozi bora, na hii kukosa uongozi bora inaleta taifa kuwa na viongozi ambao hawana any good policies, which in turn inaifanya taifa kukosa maendeleo,

Sasa wakati raisi wa taifa anasimama mbele ya umati wa watu na kuambia wanakijiji ati wafiatue watoto yaani wazae bila kuchoka, yeye anapinga kupanga uzazi, ila hali taifa inatoa watu kila waka zaidi ya 800,000 toka vyuo na hata hio taifa kuwapa ajira watu hata 150,000 ni shinda, niambie kaa huyu mtu anasitahili kuwa raisi, wakati hata shule elimu imeharibika na hospitali hata wamama wanajifungua kwa sakafu, nini anasema huyu raisi, wakati raisi nasimama na kusema yeye ni kichaa, na kwahivyo anachagua vichaa wenzake kaa mawaziri, hio tu kaa tz ingekuwa na katiba bora ni kupeleka hoja kwa jaji mkuu na huyu raisi ataondolewa madaraki, maana amekili yeye ni wenda wazimu.maendeleo na uongozi bora ni kaa gari na petrol, moja bila ingine gari haliendi popote, sasa viongozi wabovu huleta policies bovu, na bad policies ukijariu kuimplement ni kaa kuweka mango juice kwa gari ukifikiri itafanya kazi kaa petrol sababu mango juice ni liquid kaa petrol,HA HILO NDILO LINAFANYIKA SASA HAPA TZ.

Sasa mfano moja, raisi ameamru jeshi linunue korosho, kwa hela ya walipa kodi, sasa kusema ukweli serikali haina CAPACITY ya kuprocess hio korosho yote, swali ni hili watapeleka wapi hio korosho, pili je pia next year serikali itanunua pia korosho, jeshi leyewe limesha hata viwada vilivyo tz hazina uwezo wa kuprocess hio korosho yote, , THATS MY POINT, BAD LEADERSHIP EQUALS BAD POLICIES!na bad policies huangusha taifa,lakini kaa tungekuwa na katiba bora, ile kitu ingefanyika ni mtu yoyote kufika mahakama kuu, kupinga hio jambo la kununua korosho, kutoa sababu, na high court judge angeamuru hela za walipa kodi zizitumike kununua hizo korosho,katiba baya ndio inafanya ccm inunue wabunge wa upizani, kisha itumie mabavu kuwarudisa bungeni.

Katiba bovu ndio inafanya uwaja wa ndege ujengwe huko chato na hela nyingi ya wananchi itumike BILA indhini ya bunge,, na hakuna kitu tunaweza ifanya serikali, katiba bovu ndio inafanya tujenge dam ambao itatugarimu mabilioni ya dola za marekani ambazo tutakopa, na ila hali tuko na jua na upepo wa kutosha ambapo tunaweza kutumia kuzaliza zaidi ya 25,000 mw, ila hali hio dam inatoa 2,000 pekee, na wakati hakuna mvua inapungua, kaa tungekuwa na katiba bora ni mtu tu kufika mahakama kuu, kupinga hio ujenzi wa dam, kutoa sababbu za kitaalamu, na high court judge anaamuru hio project isiendelee.

Hio ni mambo machache tu ambao nimetaja umuhimu wa kuwa na katiba bora, so wakati nawasikia kina wabunge wa ccm, kina waitara, na wengine wakisema maendeleo haihitaji katiba, nashangaa sana, lakini siwalaaumu, ni njaa na vyeo vinawafanya waseme hivyo, na pia ni vile hawajawahi tembea nje ya tz waone vile mataifa hutawaliwa na umuhimu wa kuwa na katiba bora, na kwa kumalizia, samahani kwa swahili bovu kidogo, na pia kaa utatoa maoni, pls try and have INTEGRITY and CHARACTER in your contribution pls,

Wish you all nice week ahead,
 
Back
Top Bottom