Chagga King
JF-Expert Member
- Jul 6, 2011
- 1,866
- 1,076
nimekuwa nikipenda kutumia kiswahili sana kwenye simu hasa katika miongozo mbalimbali katika simu, katika hali ya kustaajabisha, hasa pale ninapochagua lugha, ni dhahiri kuwa lugha ni utambulisho wa taifa fulani, na hata kama lugha hiyo itatumika na taifa zaidi ya moja basi itaelezwa jina la lugha na taifa lenyewe mfano, kiingereza cha uingereza (British english) kiingereza cha Australia (Australia English) kiingereza cha marekani (American English) and e.t.c.
Hali ni tofauti kwa lugha ya kiswahili, unapochagua lugha ya kiswahili hasa kwenye simu, unakuta taifa la kenya ndilo linalowekwa kama wazungumzaji wa lugha hiyo. nimesikitika sana kwani kiswahili pamoja na kwamba kinazungumzwa pia nchini kenya, lakini ni lugha mama ya katika nchi ya Tanzania na ni fahari ya Tanzania, iweje fahari yetu imezwe na nchi nyingine?, yaani isitambulike kama ni lugha iliyochimbukia nchini Tanzania?, maana katika mitandao mbalimbali lugha ya kiswahili unakuta imewekewa BENDERA ya kenya, na hili nimeliona mara nyingi nikiwa naperuzi.
Pamoja na kwamba wakenya wamekuwa kimbelembele kujifanya kuwa wao ndiyo wazungumzaji halisi wa lugha ya kiswahili, hata kufikia hatua ya kuwa watafsiri wa maneno katika kamusi mbalimbali na pia kuweka maneno ya kiswahili katika vifaa vya kielektroniki kama vile simu, wamekuwa WAKIHARIBU MANENO YA KISWAHILI katika uandishi na matamshi yake, hivyo kupoteza maana kabisa na kufanya lugha ya kiswahili kuiona mpya na ngumu katika vifaa hivyo.
kwa kuwa mimi sijafanya utafiti rasmi, lakini ninaweza thibitisha haya, maana mifano na ushahidi vipo vya kutosha, ningependa wewe kama mtanzania, taasisi za kiswahili, na serikali kwa ujumla kuchukua hatua stahiki ili kutetea FAHARI yetu ya lugha ya kiswahili kwa heshima ya Tanzania.
tunyang'anywe madini na rasilimali nyingine, na kugha ya kiswahili tunyang'anywe vilevile?. haiwezekani.
.....ieleweke kuwa suala la Kenya kutangaza lugha ya kiswahili ni sahihi kwakuwa inasaidia katika ukuaji wake, tatizo ni kuwa inapotosha utaifa wa lugha hiyo ambayo inazungumzwa kwa ufasaha zaidi nchini Tanzania.
invisible kama utaona kuna umuhimu wa hili suala naomba ulitafutie namna hata kwa kuanza kuubandika (stick) huu uzi ingawa najua kuwa sijauandika vizuri kwa sababu ya uharaka.
cc: invisible