Kwanini Kenya wamefuta Mitihani ya Taifa kwenye Mtaala mpya?

Kwanini Kenya wamefuta Mitihani ya Taifa kwenye Mtaala mpya?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Kenya Mwaka jana mwanzoni au Mwaka juzi walizindua mtaala wao mpya wa CBC yaani Competetive Based curriculum.

Huu mtaala wao mpya mtoto anapimwa kwa uwezo alio nao na si kwa uwezo wake wa kukariri na kuja kujibu mtihani.Kipaji binafisi cha mtoto ndo kinapimwa, hakuna kushindanisha mashule tena.

Kingine ni kwamba kwenye mtaala huu hakutakuwa na kitu kinaitwa mitihani ya Taifa ya kushindanisha wanafunzi.

Kwenye Mtaala huu wanafunzi watapimwa uwezo wao na walimu wao kwa vigezo vilivyo wekwa.

Sisi huku tunaabudu mashindano ya Div 1 sujui 10 bora na kadhalika, tunaabudu wa kwanza na Wa mwisho ilihali tukijua fika tuna mitala ya ajabu balaa hii mitala ndo unakuta mtoto yuko Secondary ila hajui kusoma wala kuandika na amefaulu

Ndo maana hizi 10 tena sijui huwezi zikuta mtaani zikifanya mambo ya kitop 10.

Siku tukiwa na mitaala mipya na kufuta mitihani ya Kitaifa ndo hapo ubora wa elimu utakapo onekana.

Kenya sio wajinga kuondokana na hii biashara ya mitihani ya Taifa wamefanya utafiti wakaona uhuni na usanii wa mashule.

Jiulize hizo 10 tena nje ya Darasana kuna kitu zinaweza fanya? Top tena wana exceptional tofauti na hii ya kuwa wamesolve Past paper mwaka mzima na wanaingia wanakutana na maswali yale yale?
 
Japo sio kila jambo ni la kuigwa, hili linastahili kuigwa.

Tunahitaji elimu ambayo ni ya vitendo zaidi kulingana na mahitaji halisi ya jamii.
Ndo maana kwa sasa huwezi kushangaa kuona mtu kamaliza shahada ya Maabara lakini akarudi nyuma kusoma short course ya refrigeration.
 
Tanzania elimu imefanywa kua biashara. Wanaomiliki shule hawawezi ndio hao wasimamizi wa elimu, hawawezi kutaka mtaala mpya ambao utaondoa mashindano ya ufaulu halafu wao wale nini?

Najua ni jambo la muda tu tutahamia huko maana Dunia inahamia huko.
 
-Wamiliki wa shule za binafsi za Tanzania Kama nawaona wanavyo Sonya kwa hasira
-Ukweli Ni kwamba watoto wanafundishwa kujibu mitihani na sio maarifa,
-Mashindano ya shule huku Tanzania yamekuwa Biashara
 
Elim inahitaji reshaffle kubwa sana hii tabia ya kumpima mtoto na mitihan ya taifa ifeee!!!!!

Ulaya USA hakuna hii kitu chek kipaji cha mtoto mpeleke huko huko
Ronald,mess,pogba,na wengine ni mabilionea lakn hawana hata masters degree
 
Mtoto some shule ya msingi ila akifika olevel achague fani akishindwa tutamchagulia tena kwa fimbo

Huko sasa anapewa kazi ya ubunifu kwa lazima kwanza. Unapewa assignment unda au tengeneza ant virus ya computer kwa wale watakao somea mambo ya computer ukishindwa viboko.

Mechanical engineer atutengenezee engine ya piki piki au bajaji tena aeleze na mechanism yake akishindwa viboko vya mgongoni yaan kama China tu.

Dunia ya sasa ni mwendo wa technolojia lazima tuende nayo

Elon musk ni scientist mzur sana mzee wa space X kwa nn sisi tusiweze?

Mtoto akipenda history asome vzr yaaan awe deep na history ya sehem fulan atapimwa kwa kuandika vitabu.

Kiswahili hivo hivo ukishindwa viboko
 
Halafu wamewekeza sana hii miaka ya uhuru kujenga technical and technology colleges nyingi kila kata kama sio kijiji maana wanataka wakenya wawe na ujuzi wa aina mbalimbali ili kukabili masuala ya ajira na changamoto nyingine nyingi kwenye maisha,
 
Kenya Mwaka jana mwanzoni au Mwaka juzi walizindua mtaala wao mpya wa CBC yaani Competetive Based curriculum.

Huu mtaala wao mpya mtoto anapimwa kwa uwezo alio nao na si kwa uwezo wake wa kukariri na kuja kujibu mtihani.Kipaji binafisi cha mtoto ndo kinapimwa, hakuna kushindanisha mashule tena.

Kingine ni kwamba kwenye mtaala huu hakutakuwa na kitu kinaitwa mitihani ya Taifa ya kushindanisha wanafunzi.

Kwenye Mtaala huu wanafunzi watapimwa uwezo wao na walimu wao kwa vigezo vilivyo wekwa.

Sisi huku tunaabudu mashindano ya Div 1 sujui 10 bora na kadhalika, tunaabudu wa kwanza na Wa mwisho ilihali tukijua fika tuna mitala ya ajabu balaa hii mitala ndo unakuta mtoto yuko Secondary ila hajui kusoma wala kuandika na amefaulu

Ndo maana hizi 10 tena sijui huwezi zikuta mtaani zikifanya mambo ya kitop 10.

Siku tukiwa na mitaala mipya na kufuta mitihani ya Kitaifa ndo hapo ubora wa elimu utakapo onekana.

Kenya sio wajinga kuondokana na hii biashara ya mitihani ya Taifa wamefanya utafiti wakaona uhuni na usanii wa mashule.

Jiulize hizo 10 tena nje ya Darasana kuna kitu zinaweza fanya? Top tena wana exceptional tofauti na hii ya kuwa wamesolve Past paper mwaka mzima na wanaingia wanakutana na maswali yale yale?
Huu mfumo wetu usha pitwa na wakati na ni too late sana
 
Back
Top Bottom